Hello wana FJ.
Mimi ni mwanamke Wa miaka 25-30 . Kama miezi kadhaa nimejuana na huyu Kaka ni mkarimu kwa Kweli na ni mcha Mungu , hii ndio sababu kubwa ambayo imenivuta kwake. Kitu ninachokipenda kingine yaani ananifanya na kuwa free kutania na kuchekeshana kwa sana ma hii Mimi huwa Napenda sana.
Okay sababu iliyonileta hapa ni hivi tuna week ya pili sasa inakwenda hela mawasiliano. Ninakuwa Nina wasiwasi kuhusu hali yake kwa maana si kawaida yake . Nimepiga simu lines zake zote moja inaita ni ya kikazi Inakata tuu haipokelewi na nyingine ni private haupatikaniki. Ikabidi nimtafute Rafiki yake ambaye akishawahi kunitambulisha mwake na wanafanya kazi pamoja . Nimemuuliza akaniahidi kunifuatilia. Alichoelezwa kawa Huyu MTU amekwenda likizo. Kumbuka hajawahi kuniambia kuhusu hilo na si kawaida yake. Mimi Bado sikuachia hapo nikaendelea kupiga simu ile ya kikazi kuna MTU alipokea mwanamme akaniambia kuwa huyu MTU hayupo. Elewa Mimi Niko nnje ya Tz kidogo. Nimeandika SMS nyingi hazijibiwi. FB messages pia hazijibiwi . Nimemuomba msamaha nilipomkosea kwenye FB messages na kwenye SMS lakini wapi Bado kimya . Anajibu messages za wengine FB lakini sio zangu. Leo nimeingia FB kutizama kama messages yeyote lakini Bado hamna lakini niliona aliingia . Baadae tena nikaingia FB tena kwenye kukaa , nikamuona online nikaita jina lake kwenye messenger Wala hajajibu chochote na hakukaa sana akatoka online. Hebu niambieni wanaume na wanawake wenzangu nifanyeje? Na Je nimemkosea nini Huyu jamaa yangu? Nia yake ni nini ? Je Kweli anania nzuri na Mimi? Saa nyingine natamani nichukue tuu ndege nije lakini siwezi . Je niwe na subira nae au niendelee na maisha yangu? Kusema Kweli Nina connection nae moyoni . katika mahusiano yetu, pamoja si ya muda mrefu tumeongea mengi sana kuhusu maisha na familia pamoja na maendeleo . Hata sijui nifanyeje. Na kama amepata mwingine aniambie tuu ili nijue kuliko kuumia moyoni . Mchepuko Mimi siwezi . Nawasikiliza ndugu tafadhali . Asante
hiyo nguvu uliyotumia heri ungeitumia kutafuta hela.....
Wadada mlioko abroad mnapata shida sana likija swala la mapenzi. Jamaa kakosea kutokuwa muwazi kwako. Kwani angesema muachane angekosa kitu gani?
Pole, ukimya nao ni jibu. Anza upya. This time angalia usiende mbali na hapo unapoishi, unless kama unarudi home hivi karibuni.
Naomba nikuulize:Asante dear kwa uelewaji . Nakuwa mzito Wa Ku move on mapema , kwa sababu naona kama nitakuwa nimevunja ahadi zetu na kumsaliti . Nitafikiria kwa hili kama akiendelea ukimya zaidi . Niweke kwenye ndugu ili mungu anisaidie na kunionyesha njia sahihi. Asante sana .
wewe umepigwa kibuti cha kimyakimya!
Bora kipi, kimyakimya au live mezani??
Naomba nikuulize:
1. Uhusiano wenu una mda gani?
2. Mmewahi kuonana au ni mawasiliano ya mtandao tu?
Bora kipi, kimyakimya au live mezani??
Kitu live kinapendeza kweli kuliko kukaa kimya unakuwa unahisi unapendwa kumbe hakuna kitu
Kitu live kinapendeza kweli kuliko kukaa kimya unakuwa unahisi unapendwa kumbe hakuna kitu
Kwangu Napenda live ili tusije kulaumiana baadae , kwa Kweli . Ukiniambia sikufai moyo/ roho vitauma eehee lakini Nitashukuru na Ku move on na maisha yangu. Tena nitakuheshimu kwa ukweli ulioniambia . Asante .
Patience is the ultimate test for everything!
Mchepuko Mimi siwezi .
Nawasikiliza ndugu tafadhali.
Asante
Nahisi wewe ni mwenyeji humu ila umekuja na ID nyingine, siyo mbaya. Jipe muda, muda ni tiba ya kila ugonjwa hapa duniani. Ila in short huyo kaka mpole ameona hakuna jipya kwako, hivi anajipa muda ili aone kama yupo sahihi au lah.
Na wewe kaa kimya endelea na maisha yako tu, kama ipo, ipo tu!
Patience is the ultimate test for everything!
Nothing good will ever come out of you pushing him. Pia kumjazia messages sio move nzuri. Ungemtumia chache tu kumuuliza kulikoni, kwa sababu;
a) Kama hakupendi / kapata mwingine ukimsumbua haitosaidia. Muda wako ungeimvest kujifunza kuendelea bila yeye kuwa karibu kimawasiliano.
b) Kama anakupenda ataanza kukuogopa, kwa sababu atakuona too clingy and pushy. Saa nyingine kiasi cha kuweza kuahirisha mipango yake na wewe. Pia kwenye maisha kuna muda hamtokuwa karibu kimawasiliano. Haina maana hampendani hivyo ni vizuri kujifunza kukabili hali hiyo bila neno "Michepuko" kukupitia akilini. Wiki mbili tu ushaanza kutafuta uwezekaniko wa michepuko? Wenzio miaka inapita na wanakutwa wanasubiri...