Nimsaidiaje mtu huyu?

Hebu nipm namba yake,mimi nitampa pa kukaa na atakula na kusaza.
 
Halafu wewe bado unajiita Mama mwenye nyumba?. Ukicheka na nyani utaishia kuvuna mabua!.
 
Hebu ngoja sasa nikusaidie chakufanya: wewe nenda kutana na dada yake mwambie maneno haya; "shosti samahani unakumbuka majuzi uliniomba mdogo wako nimuhifadhi kwa muda ili mpango wa kutafuta chumba ukamilike, sasa baada ya kuondoka kuna tabia ambayo kwakweli sijapendezwa nayo anayoiendekeza, amefanya mazoea makubwa kwenye nyumba yangu yaani kila wakatia akijisikia tu anakuja anaingia ndani. Kumbuka mimi naishi na mme wangu na ndoa yangu naiheshimu na sipendi mtu aje kuniingilia kwenye himaya yangu. Kwakuwa yule ni mtoto wa kike na wajua wanaume hawaaminiki basi naomba umwambie asiweke mazoea kama hayo yasije yakatokea tuliyokuwa hatutarajii." Nadhani kama ni mtu wa kuelewa atakuelewa na atakusaidia mambo ya kuzungumzia bajeti ya chakula na chai achana nayo wewe linda kwanza heshima yako na familia yako.
 
Wabongo tupunguze hizi aibu aibu hako ni kasichana tu kaweke chini kaeleze ukweli tu huna haja ya kumueleza dada ake wala nn muambie ukweli wa mambo kua bajeti hazisomi na yeye ilikua ni kwa dharula tu hayo ni maradhi na maradhi hayafichwi!tafakari chukua hatua!
 
Hivi anajua ID yako hapa JF? Kama hajui mpe aje ajisomee anavyokukera uone kama atatia mguu tena kwako
 

Ndugu yangu wewe ndiye mwenye nyumba, wewe ndiye unayepanga jinsi nyumba yako inavyotakiwa kuwa na watu unaotaka waje kwako na husiotaka. Sasa hapa tatizo ni nini? muite mwambie ukweli na hali halisi ana chumba chake akae kwake... Unaweza kuwa unaona aibu/unaogopa kuwa watu watasema hivi na vile. Ishi unavyotaka kuishi usiumie rohoni kwa kumuonea aibu binadamu mwenzio..
 
Unashindwaje kuweka mipaka nyumbani kwako?

Akija mweke kitako mueleE

Nyumba yako sio kisimani wala guest kusema aje kuoga tena hiyo ndo piga marufuku

Hiyo ya kula siimind sana ila sio kila siku

Ukishindwa si umfanyie vitendo tu siku akija muda wa menu mwambie hesabu yake haipo? Mjini mipango, kwako sio hoteli

Ila nashangaa unashindwa kumwambia mtu ilhali ni nyumba yako na ina mipaka yake
 
Tatizo wabongo ni kutojiamini. Yaani hapo unajiuliza hivi nikimsema watu (au labda dada yake) watanifiriaje?!! Yaani unawaza watu watakuonaje kama vile huwa mnasaidiana kutafuta hela. Mimi ukinizingua nakupa live na wala sijali watu wanafikiria nini. Wafikirie vyovyote vile wala hainiumizi kichwa.

Mtu kama anakukera, tupa kule Jane akisema we mchoyo, John anaweza kusema we ni mtu mwenye msimamo. Mwisho wa siku haijalishi Jane na John wanasema nini bali wewe unataka nini katika maisha yako. Ndio maana nikasema ni ishu ndogo sana hii.
 
MamaBeata
Wakati mwingine kama mama wa nyumba inakubidi uwe na ujasiri fulani;
Mwambie hivi ......... Nataka upunguze mazoea na mimi .... mimi ni mke wa mtu......

Ya Annastacia yepi? Mamndenyi. Kiukweli nahitaji ushauri mi mazoea siyapendi. Kwa nini hela yake atengenezee kucha akitegemea kuja kula kwangu? Hivi hajui maisha magumu au anajitoa ufahamu?
 
Last edited by a moderator:
Kikubwa hapa ni kuogopa kuporwa mmeo au bajeti yako hairuhusu jiamini mwambie tu ukweli ili asije kwako hata siku moja..
 

mwambie ukweli watoto wa siku hizi hawana adabu kumsaidia umemsaidia inatosha ajitegemee mi sipendi vijana wanaokuja nyumbani bila sababu maluumu ila kuja kukaa tu mara kufua nk hapana timua asizoee mi nimeona mengi kuna mama moja aliporwa mume na mdogo wake wa tumbo moja alukuwepo tu nyumbani na vijanafunzi vya sasa macho juu tunaviona makazini vikija field vinabeba mababu yani fukuza asizoee nyumba yako wewe ni mama unapo ona hatari chukua hatua na wanaume wenyewe mimacho kodo siku haupo unakuta manyoya mwambie ni bora uonekane mbaoya nyumbani pawe na amani
 
Ongea na dada yake kwanza kabla hujaongea naye. Labda kama unayosema kweli kuwa anapewa hela akisikia hvyo huyo dada yake atamkalisha na kumpa yake
 
jf safi sana tunaficha ID zetu ila si tabia zetu mama pamoja na hayo unamkono wa birika
 
Ukimuonea Aibu soon atakuwa mke mwema! Ambalo nina shaka nalo na pia naweza kukushauri ni hlo la kuhofia kumchukua Mumeo kwa hilo muambie tu bila aibu!au mwambie dadake amfahamishe,kwa hlo BE MAKINI,ila hilo la kuvizia madiko mmmmh acha uchoyo .

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
binafsi sijakupenda kivileeee, sijakataa ndoa ni changa ila una katabia kauchoyo kishkaji. usimind mambo ya misosi tunakula na kunyw*. lalamika huna amani atakuibia mume lakini sio msosi. share ya mtu mmoja haiwezi kukuharibia bajet kihivyoooo

Huyu dada si mchoyo, si mbinafsi vinginevyo asingeanzisha uzi huu badala yake angeishamtoa nduki huyo binti. Waingereza walishasema "too much of anything is harmful". Kila jambo likizidi kiasi lina madhara yake. Ukarimu ukizidi una madhara, uchoyo ukizidi pia una madhara.
Kimsingi kila jambo lapaswa kufanywa kwa kiasi na kwa kufuata utaratibu na makubaliano. Mfano kwa nini dada ya huyo binti aombe mdogo wake kukaa kwa wiki 3 halafu akae miezi 3? Kwa nini hakuomba miezi 3?
Pili huyu dada anawajibika vipi kumtunza huyo binti? Wakoje? Kama anapewa hela ya matumizi kwa nini asinunue chakula ajiandalie mwenyewe? Kwa nini amtegee mtu mwingine kumtunza? Halafu zingatia yeye ni binti ambaye anahitaji kufundishwa maisha. Maana na yeye atakuja kuolewa siku moja. Je akizoea kula kwa watu badala ya kupika akiolewa itakuwaje? Atakuwa anakula kwa watu? Si hajazoea kupika au atadai aletewe house girl ili ampikie?
Kwa mimi hili sio suala la bajeti tu ni suala la kuwa na utaratibu na mipango. Hata kama wewe ni tajiri, kila kitu kina mipango yake, huwezi kutunza mtu bila sababu maalum.
Je hata kama ni ndugu yako unaweza kuendelea kumtunza badala ya kumtia moyo au kumsaidia ajitegemee? Utakuwa unamtengenezea future ya aina gani?
Mimi naona kwa manufaa ya huyo binti na kwa manufaa ya muanzisha mada ni bora huyo binti akae naye kama ndugu yake aongee naye amshauri ajifunze kujitegemea kwa kuwa kujitegemea hakuepukiki lazima ajiandae mapema.
 
Ninauhaika huyu binti ni kama mdogo wako. Mueleze kwa uwazi kabisa kuhusu hali halisi ya maisha na matumizi sahihi na ya busara juu ya pesa. Isitoshe bado ni mwanafunzi, ajue kubudget na ku save pesa anayopata....... Kwa suala la ndoa yako, ni vema kuwa karibu sana na mumeo na kujitahidi kuepuka mikwaruzano inayoweza kuepukika..aah! bwana, u know how to handle ur husband
 
Km kun apahali nakukwaza mwambie, kuliko ukimwona wamchekea huku roho yako imejikunja c vizuri
Ww ndo mama mwenye nyumba mwambie asije kwako!! inatosha
 
mwambie hivi weekend hii tutakuja kula kwako so akae huko apike na mle huko kwake, ha watu hawa wanachosha sana, mi ilikuwa ni ndugu yangu kabisa mtoto wa cousin wangu, alikuja kwangu kutembea akakaa miezi miwili, kisha akapata kazi akiwa kwangu, akaendelea kukaa miezi minne ila ndo hivyo hela yake yake peke yake hanunui hata sabuni ya kufulia nguo zake, na siku nilichelewa kuacha pesa ya mahitaji ndani lol mwenyewe akaenda kula hotelini halafu bint yangu wa kazi akashinda njaa mpka saa kumi nilipoludi,nikaona isiwe tabu nikamtafutia nyumba mbali kabisa na ninakoishi ila karibu na kituo chake cha kazi, nikamwambia nimekutafutia nyumba na nimelipia miezi minne so utakawa uhamie huko hapa si unaona tunabanana, alikubli ki shingo upande tu, akahama, eh akanishangaza tena kila siku jioni anakuja kula home yaani kwake hapiki, nilivyoona kumbe hataki kunua vyombo, nikamwambia week end moja tutaenda kula kwake, basi akanunua vyombo na akapika, since then anajipikia mwenewe na ameshazoea kujitegemea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…