Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,420
- 33,982
Nilidhani music ni haraam katika UislamNIMKUMBUKAVYO BI. SHARMILA (1942 - 2025)
View attachment 3441682
Siku mbili tatu zilizopita kuliwekwa katika mitandao makala ya marehemu Shakila mwandishi akieleza historia yake.
Pamoja na makala ile kulikuwa na picha mbili ya Shakila na ya Sharmila.
Kwa bahati mbaya mwandishi wa makala akaandika kuwa picha zote hizo mbili ni za Shakila ilhali moja ya mwanamke aliyevaa baibui tena la ukaya ni Bi. Sharmila.
Nilifahamiana na Bi. Sharmila ndani ya Bandari ya Tanga jirani na ofisi ya Port Engineer, Abdallah Mwinyi.
Jirani na ofisi ya Port Engineer marehemu Bi. Sharmila alikuwa akiendesha biashara yake ya chakula.
Mara nyingi nilikuwa nikipita na kumuona pale nikienda kumuona Port Engineer lakini sikupata kuzungumza na yeye wala sikujua kama huyu ni Sharmila muimbaji maarufu katika miaka ya 1970.
Ikasadifu siku moja nikakutana na Mhandisi Abdallah Mwinyi pembeni Kibanda cha Bi. Sharmila na Abdallah akanifahamisha kwake.
Ikawa sasa kila nipitapo pale nitasimama kumtolea salamu.
Siku moja nilipopita akaniambia, "Bwana karibia usifanye haraka nimekuletea mchumba."
Akanijulisha kwa bint mdogo kiasi miaka 10 hivi.
Bi. Sharmila akanijulisha kuwa ni mjukuu wake shule zimefungwa kaja kumsaidia kazi katika biashara yake.
Nikamsifia bint kwa uzuri wake nikamwambia basi mie nataka awe mchumba wangu.
Bi. Sharmila akawa anacheka mjukuu wake akinyanyua mabega yake juu ishara ya kuniambia hanitaki.
Lakini kila nikipita pale na kumtazama Bi. Sharmila moyo wangu ukisononeka jinsi muziki nchini kwetu usivyowanufaisha wasanii.
Nikifikiria santuri zake zilizokuwa kwa miaka na show alizofanya nk. nk.
Mara ya mwisho kabla sijaondoka Tanga nilikutana na Bi. Sharmila kwenye soko maarufu Tanga likijulikana kama "Soko la Wazungu."
Ilikuwa asubuhi na Bi. Sharmila alikuwa amekwenda kununua vitu kwa ajili ya biashara yake ya chakula.
Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi.
Amin.
Elezea zaidi kuhusu muziki wake.
Asante Mkuu, wimbo maarufu sanaKuna wimbo mmoja ulikua matata sana " machoo yanachekaaa moyoooo unaliiiaaaaa nikimkumbukaaaa wangu maridhiaaaa, ala hapo inapoga turu turu turuuuu rohooo yaniumaaaaa sili nakwambiaa.............
Msolo,Elezea zaidi kuhusu muziki wake.
Kinyungu,Nilidhani music ni haraam katika Uislam
BASI HAPO TUNAPATA UTHIBITISHO KUWA MOHAMMED SAID SIO MDINI, KAMA WASEMAVYO WENGI, KWA SABABU ANGEKUWA MDINI ASINGEZUNGUMZIA KUHUSU MUZIKI. IKILETWA HISTORIA YA TANZANIA ANAAMBIWA MDINI HUYO MSIKIMSIKILIZE, MCHONGANISHI, SASA MTU KAMA HUYU MFANO MDOGO TUU HAPO LEO, UMETHIBITISHA KUWA YEYE ANAZUNGUMZA KWA KILE AMBACHO ALICHOKIONA AU KUKISIKIA KWA WATU ZAIDI YA MMOJA KUWA NI CHA KWELI. MNAMTIA KILA ILA MBAYA BABA WA WATU KWA VILE TUU WATU WASIFUATILIE HISTORIA YA NCHI YAO KWA KUSINGIZIO CHA UDINI.Kinyungu,
Jambo la kudhani huwa halina ithibati.
Acha kutukaripiaBASI HAPO TUNAPATA UTHIBITISHO KUWA MOHAMMED SAID SIO MDINI, KAMA WASEMAVYO WENGI, KWA SABABU ANGEKUWA MDINI ASINGEZUNGUMZIA KUHUSU MUZIKI. IKILETWA HISTORIA YA TANZANIA ANAAMBIWA MDINI HUYO MSIKIMSIKILIZE, MCHONGANISHI, SASA MTU KAMA HUYU MFANO MDOGO TUU HAPO LEO, UMETHIBITISHA KUWA YEYE ANAZUNGUMZA KWA KILE AMBACHO ALICHOKIONA AU KUKISIKIA KWA WATU ZAIDI YA MMOJA KUWA NI CHA KWELI. MNAMTIA KILA ILA MBAYA BABA WA WATU KWA VILE TUU WATU WASIFUATILIE HISTORIA YA NCHI YAO KWA KUSINGIZIO CHA UDINI.
JAMANI TUFUATILIENI MAMBO KWA UNDANI, UNAPOAMBIWA USIFUATILIE TAFUTA SABABU KWA NINI NISIFUATILIE? BINAFSI MIMI HUYU BABA HANIJUI WALA SIMJUI NAMUONA HUMU TUU KWENYE JF NA YOUTUBE, LAKINI NAMPENDA SANA TENA SANA KWA VILE ANACHAMBUA MAMBO TOFAUTI BILA YA UBAGUZI, ILA KWA KWELI ASIEMPENDA HUYU BABA ATAKUWA NA WALAAKIN.
NIMEMALIZA
Zipo Saheeh aKinyungu,
Jambo la kudhani huwa halina ithibati.
Kinyungu,Zipo Saheeh a
Ahadeeth zinazokataza music mkuu.
Tatizo langu ni wewe kuandika habari za wanamusic ilhali music ni haraamKinyungu,
Sasa tatizo ni nini?
Kinyungu,Tatizo langu ni wewe kuandika habari za wanamusic ilhali music ni haraam