Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Nawasalimu wanajukwaa wote! Kama alivyowahi kunena George Herbert kwamba, "The best mirror is an old friend". Kutokana na harakati za uchaguzi BAVICHA kushika kasi, nimeona ni vema mkamtambua mmoja kati ya Kamanda anayetajwa kugombea Uenyekiti BAVICHA-Taifa ndugu Patrobass Paschal Katambi. Tulifahamiana tangu mwaka 2010 katika harakati za uchaguzi mkuu jijini Mwanza tukiwa tunahamasisha wapiga kura kuwachagua viongozi kutoka udiwani,ubunge na urais kwa tiketi ya CHADEMA. Mwaka 2011 nilifanya naye kazi ya chama CHADEMA-SAUT akiwa Mwenyekiti, Nicholaus Kirunga akiwa Makamu Mwenyekiti nami nikiwa Naibu Katibu.Mhe.Patrobass ni kiongozi mzuri mwenye kuwasikiliza watu wanapomshauri.Ni katika uongozi wetu tuliivunja ngome ya CCM SAUT na kumweka Kamanda Godlisten Malisa kuwa Rais nami nikiwa Naibu Waziri katika wizara ya mikopo.Tulifanya kazi nzuri na kujenga jina lililowavutia hadi viongozi wa kitaifa.Tulikijenga chama kwa jina na hadhi ya kuwaogopesha CCM, mwenye swali/dukuduku aniulize nitamjibu!