Nimjibu nini huyu dada?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Wana Jf kuna dada yake na mdogo wangu ambaye ni mtoto wa baba mdogo. Nimefahamiana naye sababu ya mdogo wangu, tumezoeana na namheshimu kama ndugu yangu. Lakini cha ajabu ameanza kuonesha kila dalili za kunitaka. Majuzi kanitumia sms ikisema "je una mapenzi ya dhati kwangu?" sikumjibu kwan nilihis amekosea au anatania. Lakini jana akanipigia simu na kulalamika mbona sijamjibu, nikamwambia "nilidhani umekosea kutuma hiyo sms" akajibu "ni ya kwako kwanza sinaga wanaume, naomba uijibu". Jamani ameniachia maswali mengi, vilevile kanikosea adabu., lakini vipi nimjibu? Naomba ushauri wenu
 
Ni mtoto wa babako mdogo? kama ni mtoto wa baba yako mdogo tafadhari linda heshima yako mkuu
 
tunaangalia part 3/5 ya movie nzima,tupatie sehemu zilizosahaulika:dance::dance:
 
Kwani kuulizwa kama una mapenzi ya dhati ndio nini? sioni ulipokosewa adabu

hayo maneno cyo tatizo, ila vipi yanawasilishwa hapo ndipo penye tatizo, nimeshasema kaonesha kila hali ya kunitaka kimapenzi, hiyo kaul yake ilikuwa majumuhisho tu.
 
hayo maneno cyo tatizo, ila vipi yanawasilishwa hapo ndipo penye tatizo, nimeshasema kaonesha kila hali ya kunitaka kimapenzi, hiyo kaul yake ilikuwa majumuhisho tu.

naomba fafanua hapo unaposema kaonyesha kila hali ya kukutaka kimapenzi......
 
Ina maana undugu mnao upande wa dada yako ambaye hamjahusiana mama. Mpe anachotaka hamna tatizo hapo, umeunganishwa kutokana na baba yako. Mpe kitu anataka hakuna undugu na ukitaka mfanye mkeo!!!!!!
 
Back
Top Bottom