Credit kwa huyo manzi wako sijui alisomea wapi namna ya kuacha. Akili kumkichwa ndugu yangu, unaweza usiamini kuwa mapenzi yamefika mwisho lakini ndio hali halisi. Hatuwezi kubisha kama unampenda & kiukweli am sorry for you sababu naweza kuguess ni namna gani unaumia, nakushauri tu chukua hayo maumivu kama sehemu ya experience itakayokusaidia in the future then anza kusahau. Mapenzi ni mazuri pale panapokuwa na mutual affection and respect, kinyume na hapo ukiforce utakuwa unayatafuta makubwa kuliko hayo maumivu unayoyapata kipindi hiki cha mpito. Haingii akilini kabisa kwa mtu mwenye fikra zake timamu kukubaliana na hicho anachokisema bibie huyo. Just walk away coz huijui kesho na nini kipo kwa ajili yako. Hukuzaliwa naye huyo na wala haikuandikwa mahali kwamba yeye mi maji ya uzima kwamba ukimkosa utakosa ufalme wa Mungu (japo inauma, maumivu yana mwisho wake). Ndio changamoto hizo katika mapenzi.