Duh kuna watu wakatili humu!
Watoto wa vishua wanatusanifu tu hapa... Haya!
Duh kuna watu wakatili humu!
Nimempenda mshua wako
Habari wadau.
Mzee wangu ni wale wazee wa miaka ilee maisha ya soft tach ( Maisha rahisi). Yaani enzi zilee za mashirika kwa hiyo wao maisha ni marahisi tu. Pia anasehemu zake za biashara maeneo ya ilala kama landlord mwisho wa mwezi anazikinga nyingiii.
Mzee mzima baada ya kuona hali hii nikaona ni neema kwangu hivyo oviaz nilijua nikimwomba goli mojawapo hatoninyima asilani.
Nikaanza tafuta mtaji kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali pia tukishauriana aina ya biashara ya kufanya.
Wakati mchakato ukiendelea vyema ghafla mshua akawapangisha wafanya biashara wengine. daah imeniuma sana.
Kiukweli siwezi ku afford kulipa karo sehemu kama hii ambayo very market place, na kodi yake iko higher sana.
Nahisi kudata sasa nifanyeje? wadau nao hawanielewi kabisa wanaona dizaini kama nilikua nataka niwatapeli vile baada ya kuwaona other guys wana operate sehemu ile.
Nimemshukia mshua amenijibu simpo tu. 'what i need is money'!
Daah maisha haya we acha tu.
Mzazi ni kimsapoti mwanae, unaona mtoto anabugi ramani na kazi hana si ushukuru Mungu ana idea ya biashara, vijana wengi tumeshawapoteza kwa madawa na mambo mabaya kisa stress na kuendekezwa. Hapo mzazi alipoona fremu hawezi kupa basi angekuchoresha ramani nyingine ufanye mambo,
Mimi namjua mshua na naelewa hali ndo maana sikutaka kurudi hata mambo yalipokua mlimani. Baada ya muda mambo yanajipa
Khe!...sjui kama ni mimi sijakuelewa vizuri au wewe haujaeleza vizuri, maana nilijua unazungumzia chumba cha biashara, mara ]tena unasema karo ndiyo unanichanhanya! Kama unazungumzia biashara nakushauri kwanza ungeihamisha hii thread kwenda jukwaa husika. Tukija kwenye point yenyewe sasa, mzee yuko sahihi, ile na yeye ni biashara yake, haina maana na wewe kuanza kuleech! kama wewe na hao wadau wako mlikuwa mnakokotoa gharama za kuanzisha biashara pango mnaliacha nje mjue mlikuwa mmebugi vibaya, biashara haina undugu jamaa yangu mzee yuko sahihi, nyumba ni yake na wewe ulitakiwa kulipa pango kama wapangaji wengine, ONDOA MAMBO YA FAVOR NA UNDUGU KWENYE BIASHARA, ukifungua hiyo biashara, mfano umeweka bar, utamruhusu baba kuja kugida bure? No way, hata wewe hauruhusiwi kujihudumia bure, UNALIPA! Mwisho wa siku na wewe unakokotoa faida UNAJILIPA posho kama wafanyakazi wengine, hivyo ndivyo biashara ilivyo, HAINA MAMBO YA UNDUGU! Haya toka sasa kwenye hilo lindi la giza tafuta pesa.
mkuu CYBERTEQ napingana na wewe uyo mshua ni bandidu tu by nature uyo ni mwanae alipaswa amsaidie mbona kuna wazazi wanawapeleka watoto wao ughaibuni? sasa uyo ana akili ya biashara na vip kama angekuwa anakula ngada? alichofanya uyo mzee si sawa there is something wrong somewhere!
tunaongelea fact mkuu, siyo ukatili wala kulishana upepo, hebu pata picha hii, mna nyumba kariakoo au posta, nyumba ya baba yenu, kwenye nyumba hiyo kuna frames za biashara ambazo watu wanalipia pango la milioni moja na nusu kwa mwezi, hivi kweli ndugu yangu unaweza kuweka biashara ambayo inazalisha laki sita kwa mwezi kisa unapewa frame ya bure?!!! utakuwa unatia hasara tu hiyo siyo biashara na utakuwa unarudi kinyumenyume na kujifariji unajongea!! tafuta chumba lipia kodi acha biashara za kujibana kwenye nyumba za familia, UNATAFUTA LAWAMA, hebu pata picha baba yako kaingia jf na kukuta hii thread, hiyo heading peke yake anaweza kwenda kuripoti polisi! anza kidogokidogo tafuta chako, CHA BABA SIYO CHAKO!