Nimfanye nn jirani yangu huyu?

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Wanajamv, heshima mbele kama tai. Jamani naomba kuuliza hv kumjua hali jirani yako ni umbea au? maana cc kidini tunatakiwa tuwapende majirani zetu kama tunavyojipenda na bado Twanga pepeta wakaimba nyimbo kuhusu jirani. Sasa mie nilikohamia sasa nimezungukwa na ngozi nyeupe tupu,lkn kama kawa cwabagui naishi nao vzuri lkn leo nimepigwa na butwaa baada ya kumsalimia mmoja kati ya majirani zangu nikabahatika kumuuliza hv: MIMI:Jirani salama lkn? Nilikuona ukitokea hospital vipi unaumwa au? Akanijibu. JIRANI:mie mwenyewe nimekuona unatokea makaburini kwani umekufa au? Kwa kweli ckumjibu ila iliniuma sana mpaka nikajiuliza Jamani nimemkosea nn huyu jamaa au kwasababu mie ni Black?
 
huko ulikohamia ni kila mtu na hamsini zake ndugu yangu Kama unashida ya salam ni Hello/hi, kwa ufupi hataki perepere nyingi tofauti na kule ulikotokea
 
Na wewe kama sio umbea ni nini???Kama mngekua na ukaribu wa kutosha yeye kuja kukueleza mambo yake angeshakwambia kilichompeleka hosp ila hakufanya hivyo.....sasa wewe uliuliza ya nini!!!Kwasababu tu ni majirani haina maana anataka ujue mambo yake!!!
 
Sio umbea dada yangu,ila kanichanganya kwa kweli maana weekend nikiwa nackiliza mnanda huwa na yy anakuja kuckiliza pia,halafu namtafsiria hizo nyimbo na tunapata ulabu pamoja hapa kwangu,sasa haya majibu yake ndio yamenichanganya au nisimruhusu kuja kwangu weekend hii?
 
huko ulikohamia ni kila mtu na hamsini zake ndugu yangu Kama unashida ya salam ni Hello/hi, kwa ufupi hataki perepere nyingi tofauti na kule ulikotokea
Hamna noma na mie nitamfungia vioo
 
Sio umbea dada yangu,ila kanichanganya kwa kweli maana weekend nikiwa nackiliza mnanda huwa na yy anakuja kuckiliza pia,halafu namtafsiria hizo nyimbo na tunapata ulabu pamoja hapa kwangu,sasa haya majibu yake ndio yamenichanganya au nisimruhusu kuja kwangu weekend hii?

Kunywa bia pamoja na kushea personal issues ni vitu viwili tofauti!!Hata mimi kuna watu hata pesa naweza kuwakopa ila mambo yangu siwaambii!!Jua kila mtu analimit yake.....sasa yeye anakuchukulia kama drinking buddy which is not necessarily a friend so mind your own business!
 
Hamna nöma atafurahi na mziki wangu ataomba ardhi ipasuke iwe pa kukimbilia
 
Issue hapo wala si ublack wako, issue ni jinsi ulivyouliza, labda ungemuuliza; jirani are you OK? hapo ungempa uwanja jirani yako ukuambie kama yu mzima ama yumgonjwa...pole kwa kupewa tit for tat ila uwesikika kama unamdadisi.
 
MIMI:Jirani salama lkn? Nilikuona ukitokea hospital vipi unaumwa au? Akanijibu.
JIRANI:mie mwenyewe nimekuona unatokea makaburini kwani umekufa au?
Mkuu samahani sana lakini hii hadithi inanipa mashaka kidogo. Si mara ya kwanza kulisikia kauli hii; sikumbuki wapi lakini ina"sound" kama "joke" vile.

Kwa nini ulipomuona anatoka hospital usifikirie kuwa kaenda kumwona jamaa yake anayefanyakazi pale? Kwa nini ukahusisha hospitali na yeye kuwa mgonjwa? Sasa ikiwa kila anayeonekana hospitali atakuwa anaumwa, kuna ubaya gani kwa anayeonekana makaburini kuwa amekufa?
 
Ehhhh uache umbea...kunywa pombe maliza anza mbele!!!
Sio umbea dada yangu,mie nilikuwa na nia nzuri inawezekana ugonjwa wake babu wa Loliondo anaweza kumtibu ndio maana nikamuingia na gea hiyo, kuhusu pombe yy huwa anakuja na ulabu wake na kunywa kwangu
 
MIMI:Jirani salama lkn? Nilikuona ukitokea hospital vipi unaumwa au? Akanijibu.
JIRANI:mie mwenyewe nimekuona unatokea makaburini kwani umekufa au?
Mkuu samahani sana lakini hii hadithi inanipa mashaka kidogo. Si mara ya kwanza kulisikia kauli hii; sikumbuki wapi lakini ina"sound" kama "joke" vile.

Kwa nini ulipomuona anatoka hospital usifikirie kuwa kaenda kumwona jamaa yake anayefanyakazi pale? Kwa nini ukahusisha hospitali na yeye kuwa mgonjwa? Sasa ikiwa kila anayeonekana hospitali atakuwa anaumwa, kuna ubaya gani kwa anayeonekana makaburini kuwa amekufa?
Hapana sio masihara mkuu ni vitu vilivyonitokea.
Na ili kujua nini kimempeleka pale hospital ndio maana nikamuuliza hivyo,yeye sasa alitakiwa anijibu hapana jirani siumwi ila nina mgonjwa/rafiki/ndugu yangu nilikwenda kumtembelea bac mie wala nisingehangaika
 
Issue hapo wala si ublack wako, issue ni jinsi ulivyouliza, labda ungemuuliza; jirani are you OK? hapo ungempa uwanja jirani yako ukuambie kama yu mzima ama yumgonjwa...pole kwa kupewa tit for tat ila uwesikika kama unamdadisi.
Nishapoa ndugu,hamna shaka nitakuwa nawauliza kulaini zaidi
 
Back
Top Bottom