Nimfanye nn jirani yangu huyu?

Hahahahaha! Inasikitisha na kuchekesha kwa pamoja.
Anaekupotezea mpotezee tu. Ujirani jirani ndio unazaa umbea. Mtaonana kwenye misiba. Kwenye sherehe hadi ualikwe.
 
Wanajamv, heshima mbele kama tai. Jamani naomba kuuliza hv kumjua hali jirani yako ni umbea au? maana cc kidini tunatakiwa tuwapende majirani zetu kama tunavyojipenda na bado Twanga pepeta wakaimba nyimbo kuhusu jirani. Sasa mie nilikohamia sasa nimezungukwa na ngozi nyeupe tupu,lkn kama kawa cwabagui naishi nao vzuri lkn leo nimepigwa na butwaa baada ya kumsalimia mmoja kati ya majirani zangu nikabahatika kumuuliza hv: MIMI:Jirani salama lkn? Nilikuona ukitokea hospital vipi unaumwa au? Akanijibu. JIRANI:mie mwenyewe nimekuona unatokea makaburini kwani umekufa au? Kwa kweli ckumjibu ila iliniuma sana mpaka nikajiuliza Jamani nimemkosea nn huyu jamaa au kwasababu mie ni Black?

acha kuwa na fikra hasi za kibaguzi kiasi hicho, kuwa mweusi kuna uhusiano gani na umbea wako...tatizo ujamaa umekuzidi! Dance according to the tune jombaa...
 
Sio kila swali unaweza kumuuliza kila mtu na akakuelewa nia yako. Nadhani alihisi unamsanifu na kufurahia matatizo yake. Hata hivyo kumbuka sio kila anayetoka hospital anaumwa yeye inaweza kuwa alienda kusalimia ndugu yake anayefanya kazi hospitalini au alienda kumwona mgonjwa. Acha maswali yasio na msingi
Ni kweli tupu mie lengo langu lilikuwa zuri tu ila yy kanichenjia
 
Ndio wale wanao uliza mademu wa kizungu umri wao . Huu ni umbeya , unamtakia nini jirani yako kujua mambo yake ? wewe kama umemuona anatoka hospitali hukupaswa kumuulzia ungemsalimia tuu, kwa kumjulia hali, halafu yeye ndioa afunguke kukuambia hali yake, sio kuanza kuuliza ooh umelalaje? umeamkaje, nyumbani hawajambo bla bla bla lol
Nashukuru kwa majibu yako
 
Back
Top Bottom