kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,120
- 24,395
Wakuu, leo nimeamka na nyuzi za mambo yangu binafsi yanayonisibu.
Wakuu mimi na mke wangu ndoa yetu ina miaka kadhaa, ipo hivi huyu mwanamke tunajuana nae na tulikua marafiki tokea tukiwa chuo.Baada ya kumaliza chuo nikaoa mwanamke mwingine lakini tukashindwana nae (Niliwahi kuleta uzi hapa)
Basi nikaja kumuoa huyu rafiki yangu huyu dada tulijuana nae tokea chuo yaani alikua ni zaidi ya rafiki kwangu akinisapoti nami nikawa namsapoti hadi home walikua wanajua tulivyokua tumeshibana nae in fact alikua kama ndugu yangu kabisa kwa jinsi tulivyoelewana.
Baada ya kuachana na mke wangu wa kwanza nikaamua kumuoa huyu rafiki yangu sasa. Namshukuru Mungu katika huyu mwanamke ni maisha yangu kabisa, yaani huyu ni wife material kabisa kwangu mimi na toka niwe naye tumepiga hatua kubwa kiuchumi yaani tumefanya mambo mengi sana.
Sasa kinachoniuma aisee nilijikuta nimetembea na dada mmoja ambaye alikua nilikua napenda sana kununua vitu dukani kwake tukazoeana nikajikuta nimemtongoza nikalala nae na tangia hiyo siku nikawa na uhusiano naye!!
Picha limeanza huyu mchepuko alibeba ujauzito wangu na akajifungua mtoto wa kike sasahivi mtoto ana mwaka na miezi miwili, mtoto kafanana na mimi balaa.
Wife hajagundua chochote kile ila roho inaniuma sana, nafsi inanisuta natamani nimweleze mke wangu ukweli sijui nitaanza vipi kumweleza.
Nawaza nimwelezeje wife,tumetoka naye mbali sana ananipenda na ananijali sana na ni mama bora kwa watoto wangu sio hivyo tu ananiamini sana.Kingine huyo mtoto nawaza nitaendelea kumficha hadi lini.
Naombeni ushauri wakuu kiukweli sijui nianzie wapi