Nimezaa nae naogopa kumuacha

Nimezaa nae naogopa kumuacha

NANGI NYANDA

Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
39
Reaction score
6
Kaka na dada zangu hapa Jamii forums

Naombeni ushauri wenu nimekuwa kwenye uhusiano dada mmoja kwa takribani miaka miwili, sasa na tumezaa mtoto mmoja mwenye miezi tisa sasa.

Kumetokea mizozo na migogoro kwenye uhusiano wetu na kiasi kwamba natamani tuachane. Najaribu kujishusha sana ili tuweze kulea mtoto wetu lakini hadi nimechoka.

Ninachoambulia ni dharau na kejeri tu kila siku yani hata hata kufanya mapenzi ni hadi atake yeye! Nilipanga kumtolea mahar tarehe 28 mwezi huu lakini kwa tabia yake nahc hakuna ndoa yenye amani kati yetu!

Kinachonitesa ni mwanangu ambaye ni mdogo nahisi atateseka sana. Lakini tabu ninazokabiliana nazo ni nyingi kiasi cha kuutesa moyo wangu.

Nipo njia panda wakuu nifanyaje
 
Tembo wakipigana au kugombana nyasi ndo zinaumia, utamtesa mwanao bure ebu endelea kuwa zoba ili hata cku zisogee ili mtoto nae asogee den utajua nin cha kufanya hapo baadaye...ushahuri wangu.
 
Hii iko complicated aisee! Lakini fanya kile kitakachoupa moyo wako faraja
 
One sided story

Natamani nisikie na upande wa pili pia. Naomba kuuliza haya

1. Ni vitu gani hasa ambavyo anakufanyia vilivyo kuchosha? Taja kabisa ili tujue uzito wake

2. Umesha kaa naye chini kuongea Naye ili ujue sababu ya Yeye kufanya hayo na kumuueleza madhara Yake kwa mtoto?

Jibu hayo halafu nikupe ushauri maana mimi nimepitia hayo unayopitia
 
xfactor

Moja yeye ndo mwenye maamuzi ya mwisho kwa kila kitu hataki ushauri! Pili kuna ushahidi wa yeye kutokuwa mwaminifu na ukimwambia anakuwa mbogo! Kasave jina la mwanaume anayetuhumiwa nae kifupi T na mawasiliano yao hayanibariki kabisa!

Tatu ni aina ya marafiki alionao na story wanazopiga bila kujari uwepo wangu! Somtym anakaa sebulen hadi saa tano usiku akiwa na rafiki yake (nyumba ya kupanga) huku mimi nimelala

Nne anajar marafiki kuliko mimi!Ameshamwambia mama mkwe vitu vingi vya uongo kuhusu mimi!
Anashindwa kuvumilia ugumu wa maisha tulionao na anapenda vitu vya bei kali kias kwamba haishi kukopa kwenye taasis za fedha japo mshahara ni wake!

Naumia sana basi tu
 
Last edited by a moderator:
Dah,pole ndugu ni wengi wanakumbana na kasumba hiyo.vumilia huenda ikawa ni kipindi cha mpito lakini mtoto wako kulelewa na mama/baba wa kambo ni changamoto nyingine.
 
NANGI NYANDA

Kama hivi ndivyo huyo sio mke kabisa kuhus mtoto unaweza kupanga kwamba akae nae utahudumia au umchukue ukamlee kwenu haipendez kum hadithia mama habari za ndan ya nyumba yenu hasa mabaya haipendezi na kama xfactor alivyosema hii imebase upande mmoja ingekua poa kama upande wa pili nao tungeusikia tungejua ni nn tukushaur zaidi. Pole mkuu ndo maisha hayo.
 
Last edited by a moderator:
Chagua kati ya haya,tafuta cha kukuweka busy na usijishughulishe nae kabisa, siku mmoja mtandike makofi na umwambie heshima ikae kati
mvumilie tu huku ukimbembeleza abadilike na ujifanye zoba haswaa.
 
Fuata moyo wako unavyokuelekeza ili nafsi yako ifarijike
 
Kama hivi ndivyo huyo sio mke kabisa kuhus mtoto unaweza kupanga kwamba akae nae utahudumia au umchukue ukamlee kwenu haipendez kum hadithia mama habari za ndan ya nyumba yenu hasa mabaya haipendezi na kama xfactor alivyosema hii imebase upande mmoja ingekua poa kama upande wa pili nao tungeusikia tungejua ni nn tukushaur zaidi. Pole mkuu ndo maisha hayo..

Somtym najuta kwa nn nilikutana nae! Na kumuacha itakuwa shida kwa mwanangu lakin kwa hali hii si mbaya nahc sitakuwa wa kwanza
 
Last edited by a moderator:
chagua kati ya haya.
..tafuta cha kukuweka busy na usijishughulishe nae kabisa
... Siku mmoja mtandike makofi na umwambie heshima ikae kati
....mvumilie tu huku ukimbembeleza abadilike na ujifanye zoba haswaa

Kuhusu kumchapa makofi naona ndo itakula kwangu wanawake nowdays wana msaada mno ukishamchapa makofi utaishia polisi tu naona bora nitafute cha kuniweka busy nimpe ruhusa aende zake
 
Hii iko complicated aisee! Lakini fanya kile kitakachoupa moyo wako faraja

Haipo complicated.

Hapo hajaongea nae kama baba,wa familia ana ng'ata ng'ata vidole tu na kumwambia aii wewe mwe.zangu usifanye hivyo.
 
NANGI NYANDA

Pole Sana kaka ila kuna nyakati ambazo maamuzi magumu yanahitajika ili kuokoa madhara makubwa yanayoweza jitokeza mbeleni.
 
Last edited by a moderator:
Haipo complicated.

Hapo hajaongea nae kama baba,wa familia ana ng'ata ng'ata vidole tu na kumwambia aii wewe mwe.zangu usifanye hivyo.

Hahahahaaaa maybe kuna ukweli katika hili
 
Maudhi yakizidi sana take action mkuu ili uonyeshe uthubutu wako katika jambo wewe kama mume.
 
Ndo taabu ya kuanza maisha ya kinyumba mkiwa watoto, u sound like school boy, mimi nakushauri ufanye mambo mengine beside ukikua utampata mke O.G automatically!
 
Kuhusu kumchapa makofi naona ndo itakula kwangu wanawake nowdays wana msaada mno ukishamchapa makofi utaishia polisi tu naona bora nitafute cha kuniweka busy nimpe ruhusa aende zake

Nyumba ndogo mkuu suluhusho la yote
 
Back
Top Bottom