Nimewanyima pesa nyingi Madaktari. Wanisamehe bure tu!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Sijui kama watanielewa, nahisi watachukia. Ila kama posho zao zimeongezwa, labda watacheka tu. Lakini ukweli ndio huu, na nimeamua kuusema wazi hapa JF -where we dare to talk openly! Kila nikikumbuka niliyofanya, najua kabisa madaktari wana kila sababu ya kunikazia macho. Lakini kabla wewe msomaji hujanihukumu, soma hadi mwisho, kisha uniambie kama nimekosea kuwanyima pesa madaktari au la.

Iko hivi: mimi nikiona dalili za magonjwa mwilini, sikimbilii kwa madaktari kuomba wanipime naumwa nini. Badala yake naweka mkono wangu sehemu inayouma na kukemea dalili za ugonjwa kwa Jina la Yesu. Kwa njia hii na kwa kumuomba Mungu, nimepona magonjwa mengi bila kulipa pesa ya kumuona daktari au kununua dawa. Jana nilisikia maumivu makali sana mwilini. Nikayakemea kwa Jina la Yesu. Instantly, nikapona. Jambo hili nimelifanya mara nyingi sana. Hivyo kwa sehemu kubwa nimewanyima pesa madaktari. Najua, kuna madaktari wanaofurahia kuona 'nyomi' la wagonjwa wakiwa wamejipanga foleni hospitali kusubiri huduma. Hivyo watu kama mimi, wenye imani ya kupona kwa Jina la Yesu tukiwa wengi, ni huzuni kwao kwa sababu tutakuwa tunawanyima pesa ya kununua ugali.

Usininukuu vibaya. Sijasema madaktari hawafai. Nope. Ni watu muhimu sana. Wameokoa maisha ya watu wengi, na Mungu huwa anawatumia pia. Lakini mimi nimekuwa nikichagua shortcut, njia isiyo na gharama, sio kwa kiburi, bali kwa imani. Kama kwa kufanya hivyo nimewanyima riziki yao, basi wanisamehe bure tu. Maana sio kwa chuki, sio kwa dharau, ila kwa neema niliyopewa ya kutumia Jina lipitalo majina yote. Kama nimefanya makosa, basi ni imani yangu. Na kama ni kosa kuamini kwamba Yesu bado anaponya, basi sina la kujitetea, ila nitasimama na ushuhuda wangu hadi mwisho, kwamba Yesu anaponya hata leo!

NAKAZIA: Kwa bandiko hili, sikuambii usiende hospitali. Kama imani yako ni haba, ukisikia dalili za ugonjwa, fanya haraka uende ukapimwe, upewe dawa. La sivyo, utakata moto. Na kama hujaokoka, ukiondoka duniani, utaenda kuteseka zaidi jehanam.

Hata mimi huwa naenda hospitali mara moja moja, ila nikienda, siweki matumaini yangu kwa madaktari, kwa sababu na wao kuna wakati wanashindwa kujua chanzo cha ugonjwa ni nini. Na kuna wengine sijui ni kusahau waliyofundishwa chuoni au nini, mpaka wa-google kwanza websites za kitabibu ndio wanakuambia unaumwa nini.

Na wengine huwa wanatumiwa kabisa na Ibilisi, kuwakatisha tamaa wagonjwa. Kuna siku nilienda hospitali fulani ili kupata matibabu baada ya kupungukiwa damu. Swali la kwanza aliloniuliza daktari ni hili: "Wewe umepeleka wapi damu?" Hili ni swali la kishetani kabisa. Namshukuru Mungu aliyeiumba damu, aliiongeza mwilini mwangu ikarudi kwenye viwango vyake, kwa miujiza yake. Haleluya!
 
Narudia tena: Tafadhali usininukuu vibaya. Sio kwamba siwapendi madaktari. Natambua umuhimu wao. Ila natambua kwanza uwepo wa Daktari Mkuu, Yesu Kristo. Na hii ni moja kati ya faida za kuokoka. Ukiumwa, unamkimbilia Yesu una-save mapesa na gharama za kutibiwa hospitali.

Zab 103:2-3
"Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi."
 
Kila mtu aliyeokoka amepewa mamlaka ya kukemea pepo na kuponya maradhi . Itumie mamlaka hiyo utaona miujiza mingi ya uponyaji.

Lk 9:1-25
"Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa."
 
Sawa "ma mtu" tunakusubiri uje kufanya UPASUAJI
20250630_220619.jpg
 
Sawa "ma mtu" tunakusubiri uje kufanya UPASUAJI
View attachment 3392904
Hahaa. Ulisikia wapi Yesu anafanya upasuaji? Mkumbuke yule kipofu Bartimayo. Angekuja kwenu leo mngemwambia afanyiwe Ocular surgery/Cataract surgery/LASIK(Laser-Assisted In Situ Keratomileusis)/Glaucoma surgery/Vitrectomy/Corneal transplant (Keratoplasty)...upasuaji wenye gharama kubwa mno. Lakini Yesu ona alichofanya. Hadi raha!
Mk 10:46-52
Wakafika Yeriko;... Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu...Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.

Yesu alitamka tu: "Enenda zako, imani yako imekuponya." Instantly, kipofu akapata kuona!

Maumivu niliyoyasikia jana ningeenda hospitali, nafikiri kwanza ningelazwa kwa bed, halafu ningeambiwa nilipe mapesa, nipimwe kwa kutumia mojawapo ya mashine hizi au zote kabisa:
MRI(Magnetic Resonance Imaging), CT Scan(Computed Tomography), Ultrasound(Sonography), X-ray Machine, PET Scan(Positron Emission Tomography). Kwa neema ya Mungu nimepona kwa Jina la Yesu, bila kulipa hata senti. Tumsifu Yesu Kristo!!
 
Hongera I love ur consistence
I’m genuinely humbled by your gracious remark. Encouragement such as yours is more than a compliment; it is a gentle reminder that the labor of constancy does not go unnoticed. I think, consistency is the inaudible eloquence of unwavering conviction, a testament not shouted, but lived. Thank you DR HAYA LAND for recognizing what, to me, is a quiet pursuit of purpose wrapped in persistence.:HYPERCLAPHD:
 
Sijui kama watanielewa, nahisi watachukia. Ila kama posho zao zimeongezwa, labda watacheka tu. Lakini ukweli ndio huu, na nimeamua kuusema wazi hapa JF -where we dare to talk openly! Kila nikikumbuka niliyofanya, najua kabisa madaktari wana kila sababu ya kunikazia macho. Lakini kabla wewe msomaji hujanihukumu, soma hadi mwisho, kisha uniambie kama nimekosea kuwanyima pesa madaktari au la.

Iko hivi: mimi nikiona dalili za magonjwa mwilini, sikimbilii kwa madaktari kuomba wanipime naumwa nini. Badala yake naweka mkono wangu sehemu inayouma na kukemea dalili za ugonjwa kwa Jina la Yesu. Kwa njia hii na kwa kumuomba Mungu, nimepona magonjwa mengi bila kulipa pesa ya kumuona daktari au kununua dawa. Jana nilisikia maumivu makali sana mwilini. Nikayakemea kwa Jina la Yesu. Instantly, nikapona. Jambo hili nimelifanya mara nyingi sana. Hivyo kwa sehemu kubwa nimewanyima pesa madaktari. Najua, kuna madaktari wanaofurahia kuona 'nyomi' la wagonjwa wakiwa wamejipanga foleni hospitali kusubiri huduma. Hivyo watu kama mimi, wenye imani ya kupona kwa Jina la Yesu tukiwa wengi, ni huzuni kwao kwa sababu tutakuwa tunawanyima pesa ya kununua ugali.

Usininukuu vibaya. Sijasema madaktari hawafai. Nope. Ni watu muhimu sana. Wameokoa maisha ya watu wengi, na Mungu huwa anawatumia pia. Lakini mimi nimekuwa nikichagua shortcut, njia isiyo na gharama, sio kwa kiburi, bali kwa imani. Kama kwa kufanya hivyo nimewanyima riziki yao, basi wanisamehe bure tu. Maana sio kwa chuki, sio kwa dharau, ila kwa neema niliyopewa ya kutumia Jina lipitalo majina yote. Kama nimefanya makosa, basi ni imani yangu. Na kama ni kosa kuamini kwamba Yesu bado anaponya, basi sina la kujitetea, ila nitasimama na ushuhuda wangu hadi mwisho, kwamba Yesu anaponya hata leo!

NAKAZIA: Kwa bandiko hili, sikuambii usiende hospitali. Kama imani yako ni haba, ukisikia dalili za ugonjwa, fanya haraka uende ukapimwe, upewe dawa. La sivyo, utakata moto. Na kama hujaokoka, ukiondoka duniani, utaenda kuteseka zaidi jehanam.

Hata mimi huwa naenda hospitali mara moja moja, ila nikienda, siweki matumaini yangu kwa madaktari, kwa sababu na wao kuna wakati wanashindwa kujua chanzo cha ugonjwa ni nini. Na kuna wengine sijui ni kusahau waliyofundishwa chuoni au nini, mpaka wa-google kwanza websites za kitabibu ndio wanakuambia unaumwa nini.

Na wengine huwa wanatumiwa kabisa na Ibilisi, kuwakatisha tamaa wagonjwa. Kuna siku nilienda hospitali fulani ili kupata matibabu baada ya kupungukiwa damu. Swali la kwanza aliloniuliza daktari ni hili: "Wewe umepeleka wapi damu?" Hili ni swali la kishetani kabisa. Namshukuru Mungu aliyeiumba damu, aliiongeza mwilini mwangu ikarudi kwenye viwango vyake, kwa miujiza yake. Haleluya!
Kwa kweli umetunyima fedha mwanamke bahili wewe 😂 😂 😂
Tutakula tu kwa neema yake Mungu unayemuomba na kukuponya ipo siku ntakuwa na njaa ntaomba ugali atakupa ugonjwa ili uje unipe hela nipate ugali 😂

Mungu yu mwema

Ila toa chuki na sisi matabibu maana shatani humtumia mtu yeyote hata wewe ushatumiwa sana tu

Tunaishi kwa neema si kwa sheria
 
Na ntaendelea kuwanyima sana. Kwa sababu siku hizi badala ya kutoa huduma ya afya, mnafanya biashara ya afya! Kuna hospitali fulani nilienda, mfanyakazi mmoja alipoona mgonjwa ameingia, akamwambia mwenzake: "Changamkia tenda hiyo!" Kama wagonjwa ni tenda siku hizi, basi afadhali tuwanyime kabisa pesa yetu tunayoipata kwa neema na kwa kutoa jasho jingi.
 
Mungu yupo atatulisha , mbona ndege wa angani wanakula

Tutakula tu hata utunyime vip

Harafu nimekupenda tu ghafla 😂😂😂😂
 
Duh, kama wewe ni Daktari, pokea maua yako! Nafikiri wagonjwa wakija kwako wanapona wote. Una imani kubwa sana.
Harafu nimekupenda tu ghafla 😂😂😂😂
Umenipenda kwa upendo gani? Agape (ἀγάπη), Phileo (φιλία), Storge (στοργή) au Eros (ἔρως)???
 
Back
Top Bottom