Nimewachangisha michango ya ndoa/harusi ili nipate mtaji.

Kayoka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
2,389
Reaction score
2,217
"Habari Wakuu,

Kama mjuavyo jinsi maisha yalivyo magumu kwa sasa huku mtaani, lazima akili na maarifa yaongezeke.
Nilimaliza chuo tangu 2015 ila mpaka sasa sijabahatika kupata kazi ya kueleweka na kila ndugu mwenye uwezo niliyemwomba msaada hakuwa tayari kunisaidia (niliwaomba mtaji tu wa kuanzia).
Nikaondoka home na kwenda kujitafutia maisha mwenyewe mbali na nyumbani ila bado nikapigika nikaamua kurudi tena nyumbani kwa baba na mama kujipanga upya.

Kuja tu hapa nikapata wazo la kutangaza kuoa na kufunga ndoa na mpenzi wangu wa siku nyingi huku nikimpa taarifa kila ndugu, rafiki, jamaa na watu wa karibu na wao pia wameniunga mkono na kutangaza kuchangia kiasi kikubwa cha pesa, mpaka sasa tayari nimechangiwa 5.4M na ahadi zingine kibao.

Ndoa inataarijiwa kufungwa 10/08/2019 ila dhumuni langu nikipata tu hiyo hela natokomea huko Msumbiji kutafuta maisha machimboni kwani tayari mtaji nitakuwa nimepata.

Ushauri wenu wakuu katika hili ninalotaka kufafanya, Je niko sawa au najitafutia laana na kufungwa mbele ya sheria?"
 
Hakikisha ukifika msumbiji tafuta rafiki wa kuwapa habari kama umekufa na wanahitaji hela ya kukuzika. Hapo itatumwa 5.4 million nyengine mtaji umekuwa mara mbili yake. Usisahu kujilaza kwenye coffin na kuwatumia picha zako za maiti.🤣🤣

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hujui tu ila hii idea umewafungua watu wengi jobless

Kuhusu swali lako sijui...ila usikimbie mwenyewe huko Msumbiji,kimbia na bi harusi
Mkuu upo sahihi,na huna aja ya kukimbia kwani hakuna atakae kufunga ,ongea tu vizuri na kamati funga ndoa ,ila kwenye vyakula na manywaji kila mtu apate wali na soda moja ,watachonga sana ila hakuna watakachofanya bali wewe utakuwa umebaki na boom la maana
 
Kupanga upange wewe kutapeli.. kupokea pesa upokee wewe.. uamuzi unao.. sikuelewi kwanini unakuja kuuliza now.

Kwanza wewe unaonyesha huna akili za kujisukuma kutafuta hata kuanzia na kidogo.. unafikiri hizo pesa utaweza kuzitumia vizuri!!!

Nenda kanisani ukasali na kuombewa.. niklngekuelewa kama hata ungekuwa umepanga kufunga ndoa na sherehe ndogo nyumbani..huku ukiwa umepanga uwaambie nini.

Tapeli mvivu.. unajua kuna matapeli wanaotumia akili hadi mtu unawapa 5.. ila wewe ni bomuuu.
 
Ushauri mzuri
 
Hakikisha ukifika msumbiji tafuta rafiki wa kuwapa habari kama umekufa na wanahitaji hela ya kukuzika. Hapo itatumwa 5.4 million nyengine mtaji umekuwa mara mbili yake. Usisahu kujilaza kwenye coffin na kuwatumia picha zako za maiti.[emoji1787][emoji1787]

Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Halafu amtafute wa kumfufua
 
Mkuu tatizo nini?
Mimi sio tapeli ila nimetafuta njia ya kupata mtaji toka kwa watu wangu wa karibu ambao kila nikiwalilia wananipotezea.
Naomba ushauri wako nifanye nini badala ya hili.
 
Safi sana. Wabongo kwenye sherehe na misiba wanajua sana kutumia pesa kama ni bia zitanyweka mpaka basi. Ila sasa kuwezeshana kwenye maswala ya Maendeleo kila mtu anapambana na hali yake.
 
Kama ni hivyo huyo mpenzio usimuache kama vipi tambaa nae mkanzei huko huko mgodini
"Habari Wakuu,

Kama mjuavyo jinsi maisha yalivyo magumu kwa sasa huku mtaani, lazima akili na maarifa yaongezeke.
Nilimaliza chuo tangu 2015 ila mpaka sasa sijabahatika kupata kazi ya kueleweka na kila ndugu mwenye uwezo niliyemwomba msaada hakuwa tayari kunisaidia (niliwaomba mtaji tu wa kuanzia).
Nikaondoka home na kwenda kujitafutia maisha mwenyewe mbali na nyumbani ila bado nikapigika nikaamua kurudi tena nyumbani kwa baba na mama kujipanga upya.

Kuja tu hapa nikapata wazo la kutangaza kuoa na kufunga ndoa na mpenzi wangu wa siku nyingi huku nikimpa taarifa kila ndugu, rafiki, jamaa na watu wa karibu na wao pia wameniunga mkono na kutangaza kuchangia kiasi kikubwa cha pesa, mpaka sasa tayari nimechangiwa 5.4M na ahadi zingine kibao.

Ndoa inataarijiwa kufungwa 10/08/2019 ila dhumuni langu nikipata tu hiyo hela natokomea huko Msumbiji kutafuta maisha machimboni kwani tayari mtaji nitakuwa nimepata.

Ushauri wenu wakuu katika hili ninalotaka kufafanya, Je niko sawa au najitafutia laana na kufungwa mbele ya sheria?"
 
Hakikisha ukifika msumbiji tafuta rafiki wa kuwapa habari kama umekufa na wanahitaji hela ya kukuzika. Hapo itatumwa 5.4 million nyengine mtaji umekuwa mara mbili yake. Usisahu kujilaza kwenye coffin na kuwatumia picha zako za maiti.[emoji1787][emoji1787]

Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Aje nimuuzie jeneza kabisa
 
Mkuu upo sahihi,na huna aja ya kukimbia kwani hakuna atakae kufunga ,ongea tu vizuri na kamati funga ndoa ,ila kwenye vyakula na manywaji kila mtu apate wali na soda moja ,watachonga sana ila hakuna watakachofanya bali wewe utakuwa umebaki na boom la maana
😅😅😅😅
 
Hiyo ndio akili huhitaji tena ushauri, siku ukiwa tajiri utasifiwa tuu regardless what happened ila usipofanya cha maana vise versa is true.. Kuwa na hela is 1 thing kuikuza ziwe nyingi ndio kazi kubwa
 
Hakuna mwalimu mkali kama walimwengu, usiombe kukutana nae, hayupo shule kama wazungu, hatoi nafasi ya pili, hana msamaha wala aibu yeye ni vitendo tu.

Mkuu achana na pesa za watu, zina mambo mengi sana. Jasho la mwanaume haliliwi, utazitapika hizo hela

Thank me later
 
Back
Top Bottom