Nimevunja uchumba wa watu

Nimevunja uchumba wa watu

Heisenberg

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2017
Posts
1,688
Reaction score
2,981
Habari za eid

Kuna binti niponae kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa toka mwaka huu uanze. Nimekuwa nikimpenda sana kiasi cha kujitoa sana kifedha na ki hali kwa muda wote huu.

Lakini binti amekuwa akinisisitiza kuwa yeye ni mchumba wa jamaa fulani na wanasubiri ndoa tuu. Hiyo hali haikunirudisha nyuma kwa mapenzi niliyokuwa nayo kwake.

Juzi jioni Baada ya kutoka kutafuta Ugali wa watoto nikampigia bint kuwa niende kwake au yeye aje kwangu. Binti akasema niende. Basi bila kusita nilifunga safari nikaenda. Tukawa kwake akapika tukala

Hamad mida ya saa4 mlango ukagongwa. Sikuwa na wasiwasi kumbe ni mchumba wake. jamaa akaingia ndani akanikuta nimekaa kwenye sofa, jamaa akaniangalia akaniuliza hivi bado unaendelea na mchumba wangu?? Mm nikawa kimya jamaa akaingia chumbani kwa mwanamke akabeba vitu vyake na kuondoka. Mm nikabaki na yule mwanamke.

Amelia usiku kucha na kunitupia mm izo lawama. Asubuhi jana jamaa ameambatana na mshenga wake wameenda nyumbani kwa akina Binti kudai mahari. Ndugu wa mwanamke wameomba jamaa na mshenga waende Jumamosi ili kikao cha familia kilichopokea mahari kikutane. Baba na mama ya binti wameshindwa kumtuliza jamaa ili wayamalize. Jana jioni nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mzazi wa binti, niliongea nae aiwa analia sana. Nimeomba leo niende nyumbani kwa akina binti nikawasikilize wazazi wake.

Nimemuuliza binti kuwa niende kwao au nisiende binti hataki kusema. Nikampigia dada ake binti kuwa vipi niende kwao?? Dada yake akasema niende.

Hapa nilipo najiaandaa kwenda. Ni mkoa jirani. Ni mwendo wa masaa 4 tu ntakuwa nimefika.
 
Okay tunasubiri mrejesho
 
Back
Top Bottom