Nimeuza 15000 kwa debe viazi mviringo shambani

karue

Senior Member
Oct 31, 2018
191
347
Bila shaka mko salama,

Nina miaka 7 nalima viazi mviringo uku nyanda za juu kusini mkoa wa Iringa. Kwa miaka yote bei ya shambani ilikua inacheza sh 5000_8000 kwa debe shambani.

Lakini ilipofika mwezi wa tano mwaka huu bei ilibadilika Sana na kufikia 15000. Wanunuzi wanatafuta kiazi mviringo kwa gharama ya 15000 na kuendelea kwa debe. Kama mkulima moyo wangu umemwagiliwa furaha kwani misimu mingine ilikua ni masikitiko na maumivu kutokana na wanunuzi kujipangia bei.

Niliyobaini kama mkulima hadi bei ya kiazi kupaa juu ni

1: Pembejeo zilikua juu Sana msimu wa kilimo watu wengi hawakulima kiazi ( mbolea)
2: Mvua zilikata mapema wale waliopanda kwa Mara ya pili mwezi wa tatu viazi vilikosa mvua ya kutosha

Vipi hapo ulipo kiazi mviringo ni shilingi ngapi kwa kilo, debe, roba?

IMG_20220602_175044_396.jpg
 
Bila shaka mko salama
Nina miaka 7 nalima viazi mviringo uku nyanda za juu kusini mkoa wa Iringa.
Sawa umeuza/utauza viazi vyako kwa bei kubwa. Ila na wewe jiandae kununua mahindi, mchele, mafuta ya kupikia, na bidhaa nyingine za chakula kwa bei ya juu zaidi.

Kufa, kufaana!
 
Sawa umeuza/utauza viazi vyako kwa bei kubwa. Ila na wewe jiandae kununua mahindi, mchele, mafuta ya kupikia, na bidhaa nyingine za chakula kwa bei ya juu zaidi.
Kufa, kufaana!
Hapo ambacho silimi ni alizeti tu mkuu
 
Back
Top Bottom