Nimeumwa na nyuki jichoni

Nimeumwa na nyuki jichoni

New Nytemare

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Posts
3,419
Reaction score
2,640
msaada wataalam,

Nimeumwa na nyuki mchana huu jicho limevimba sana naomben msaada kwa anayejua dawa ipi ya asili au ya dukan itakayonisaidia kupunguza uvimbe maana kesho nnasafari kwenda kwenye interview.

Msaada wenu wakuu
 
Umenichekesha, lakini pole zangu.

Eti unasafiri kwenda kwenye intavyuu, ingekuwa intavyuu ya ubondia ungepata moja kwa moja.
 
Hio ni baraka na ninakwambia kuwa kwa JINA la YESU umeshapata kazi,

kuna watu watakuja kuomba picha, just ignore them hio ndio JF

asante lakin interview yenyewe ni ya udereva sasa jicho moja limefunga kwa uvimbe nahis hii itafanya wenzangu wanipiku...
 
Nenda tu hivyohivyo katika intavyuu, wala haitakuwa na athari katika hiyo.
 
msaada wataalam..nimeumwa na nyuki mchana huu jicho limevimba sana naomben msaada kwa anayejua dawa ipi ya asili au ya dukan itakayonisaidia kupunguza uvimbe maana kesho nnasafari kwenda kwenye interview...msaada wenu wakuu

dah pole sana.sasa umewezaje kuona na kuandika post?au ndo unautaalam wa kupiga chabo kwa kutumia kajicho kamoja?
 
mh kisaikolojia sijawa poa tokea niumwe na huyu nyuki ukizingatia interview
 
sometimes huwa inasaidia paka chumvi hilo eneo litapoa,
 
ebhane bado sijaona changes..wengine wanasema nikilala usiku ntakavo amka limezidi sijui kuna ukwel????
 
Pole kaka, ni kweli utakavyoamka asbh litakuwa limezidi.

Isingekuwa interview ya udereva isingeathiri kitu lkn kwa post hiyo napata wasiwasi huenda ni mpinzani wako amefanya mambo maana hutaweza kupewa gari uendeshe na jicho moja.
 
mh kisaikolojia sijawa poa tokea niumwe na huyu nyuki ukizingatia interview

Mkamate huyo nyuki kesho uende naye kama evidence (jokes)

nakuomba usiache kwenda, we nenda tu na nina imani utapata kesho utatupatia majibu hapa.
 
ebhane bado sijaona changes..wengine wanasema nikilala usiku ntakavo amka limezidi sijui kuna ukwel????


pole sana, muda mfupi baada ya kuumwa na nyuki, ungekata kitunguu maji kisha upakaze pale alipokuuma, sehemu inakua haivimbi, ila naona kama kwa muda huu umeshachelewa,
 
Bro. chukua kipande kidogo cha KITUNGUU maji. Kisha sugua kwenye hiyo sehemu aliyokung'ata nyuki. ungefanya hivi punde ulivyong'twa pasingevimba. Hii ndio dawa kwa wale wanaong'atwa na Nyuki na Nge. Kitunguu husaidia kuondoa sumu na kufanya uvimbe usitokee
 
Twanga kitunguu saum upake. Nunua na wild tiger ktk duka la dawa upake kuondoa na sumu pia
 
Back
Top Bottom