Ni binti niliekuwa nae kwenye mahusiano karibu mwaka sasa mda wote tukiwa chuoni (mie nikiwa mwaka wa mwisho yeye wa kwanza). Nilimpenda sana kwa moyo wangu wote, kumjali, kumsikiliza, kumsaidia pale anapokwama iwe kifedha, ushauri au kwa namna yoyote ile.
Ni binti pekee katika mahusiano yote nilopita ya nyuma nilieamua kumtambulisha kwa ndugu zangu kwa kuwa nilimuamini sana na kuona anafaa kuwa mke. Alikuwa mkristo lakini akaamua abadilike sababu yangu kuswali, kufunga, kujifunza uislamu, kuvaa mavazi ya kusitiri mda wote, yote haya ni kumuandaa kuwa mke.
Kipindi tukiwa chuoni alikuwa akisumbuliwa sana na wanaume, hakunificha kila aliyekuwa akimsumbua alikuwa akiniambia na kuwablock wote au kuongea nao wasimsumbue kuna jamaa mmoja anasoma nae darasa 1 alikuwa akimsumbua sana nishakuta SMS kibao za mapenzi kwenye simu yake nikamshauri amwambie kuwa yupo na mie pia amblock akakubali na kufanya hivyo.
Kuna wakati flani jamaa alipata matatizo ya kufiwa na mzazi wake hivyo mpenzi wangu ilibidi awasiliane nae kwakuwa ni mwana darasa mwenzao. Hapo ndipo mawasiliano na jamaa yakaanza tena hakumblock tena wala kuacha kuwasiliana nae baada ya msiba nilimuuliza kwanini anaendelea kuuwasiliana nae akaniambia kuwa jamaa hamsumbui tena anamuheshimu na anafahamu pia binti yupo na mie kwenye mahusiano.
Nilikuta tena SMS za mapenzi za jamaa kwe simu ya bibie kwa mara ya pili japo mpenzi wangu alikuwa hajibu nilikasirika sana na kumuuliza kwanini ulinidanganya kuwa jamaa hakusumbui tena akanambia alianza siku moja ya nyuma alitaka kuniambia ila niliwahi kukuta SMS za jamaa kwenye simu yake.
Nikamwambia sitaki kuona urafiki tena na huyo jamaa nilimwambia kuwa nikaongee nae huyo mwanaume anaemsumbua alikataa akaniambia atamwambia na kuacha kabisa kumtafuta. Nikapotezea wakati wote huo nikiwa naendelea kuchunguza simu ya mpenzi wangu kweli hakuwa anawasiliana nae tena na alinionyesha mpaka namba amemblock.
Baada ya kufunga chuo mie nilielekea mkoa mwengine kufwata cheti kwani ndo nilikuwa nishamaliza chuo yeye alitangulia Dar. Baadae nikarudi Dar tukapanga tuonane jumamosi nimsindikize hospitali, nilimpeleka hospitali aliingia kufanya ultrasound akaniachia simu yake kubwa (smartphone) alikuwa na simu nyengine ndogo ambayo nilimpa atumie pia tukiwa chuoni hakuitoa kwenye handbag.
Nikawa naangalia picha WhatsApp nikakuta SMS za yule yule jamaa na picha ambazo mpenzi wangu alikuwa akimtumia japo sio picha mbaya.Nikanyamza kimya. Jioni baada ya kurudi nyumbani nilimpigia simu na kumuuliza kwanini alinidanganya kuwa hawasiliani nae tena alilia sana kwani nilimshambulia sana, nilishikwa na hasira.
Mpaka dada yake akanipigia simu kumuombea msamaha. Nikamkanya na kumwambia nikikuta tena SMS zozote za jamaa ntachukua maamuzi magumu. Sikiushia pale nikapata wasiwasi ikabidi nimtumie jamaa anaemsumbua SMS kali kwenye namba yake.
Jamaa alishangaa sana kwani hakuelewa lolote na hakujua kabisa kuwa binti tuna mahusiano nae alisikitika sana na kujiuliza kwanini anakufanyia hivi wakati mna malengo ya kuja kuwa kwenye ndoa kumbe mpenzi wangu alikuwa akinitambulisha kwa jamaa kama rafiki tu.
Darasa lao wote walikuwa wakijua ana mahusiano na mshikaji mpaka room mates, rafiki zake walikuwa wakifahamu japo hawakutaka kuniambia. Jamaa alinitumia SMS zote walokuwa waki chat na mpenzi wangu kumbe bibie alikuwa akifuta msg alizokuwa akimjibu jamaa.
Tukapanga na mshikaji tukutane mahali halafu nimpigie mpenzi wangu pamoja na dada yake waje. Jamaa alijificha sehemu dada yake alifika ye alikuwa kwenye daladala kwa bahati mbaya alimuona jamaa akapitiliza kituo na kumtumia jamaa SMS kuwa anamchukia na hataki kumuona tena.
Jamaa alinionyesha SMS nikampigia simu mpenzi kumuuliza upo wapi mbona hujafika akawa anatoa sababu nyingi za uongo kwani ni kamaalichanganyikiwa. Tukaamua kuondoka jioni nilimtumia SMS nyingi sana bibie za hasira kwanin aliamua kunifanyia vile nikamtumia msg zote alizokuwa aki chat na jamaa akabaki kuomba tu msamaha.
Dada yake akanipigia simu kuniomba msamaha na kunisihi nisiwaambie ndugu zangu kwani tulikuwa kwenye mipango ya kwenda kwao kujitambulisha. Kweli binti kaomba sana msamaha, anapiga simu sipokei huko kwao wote wanahuzunika, jamaa kanieleza ukweli wote kuwa binti ni walikuwa marafiki japo walikuwa waki chat msg za mapenzi kwani jamaa alikuwa akimtaka na alikuwa akimfukuzia hakujua kuwa binti alikuwa na mahusiano ananiambia hawajakutana kimwili japo siamini.
Wana JF wenzangu nimekuja kwenu kupata ushauri, kweli binti huyu anafaa kuwa mke kaamua kunificha mda wote huo, kanidanganya pia kinachoniuma zaidi ni kumkataza kuwasiliana nae ila aliendelea mpaka tupo hospitali alikuwa akiendelea ku chat nae kwa simu ndogo wakati yupo kwe chumba cha ultrasound mie nikiwa nje na simu kubwa ya smartphone.
Nilimuamini sana, nilijitoa sana kwake leo amenifanyia hivi kweli? Je nisingejua angerudi chuoni si ndio angejiachia kabisa na jamaa? Hivi wadada nini mnataka hasa mkiwa kwenye mahusiano mume anakujali, anajitunza, hakusaliti vyote utakavyo anakufanyia.