mwandandila999
Member
- Jul 29, 2015
- 22
- 16
Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa Chadema kuwa wamelidhia KATIBU mkuu wetu Dr Slaa, kupumnzika kwa mda usio Julikana. Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyo yapata ktk kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya.... Naomba nitumie fursa hii kumuomba mh😀r Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na ukawa kwa ujumla tafadhari nakuomba lejea kambini kwa masirahi ya chama na Taifa.
Inaskitisha na inanisononesha kwa uamuzi wako dr slaa.Hata kama umeingia kinyongo hukupaswa kuamua katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi,naomba urudi tuendelee kuiokoa nchi hii
Kwani hata Dr. Slaa angesimamishwa kugombea urais kupitia ukawa angeshinda? Mm nahakika asingeshinda. Nguvu alionayo Lowasa na uwingi wa wafuasi wake ni dhahiri atashinda.Dr Slaa angeungana na wapambanaji wengine kuing'oa ccm.maana nia ni kuiondoa ccm madarakani
Tawashangaa CCM kama hawatomfuata Slaa kumshawishi arudi ccm kusaidia chama kusafisha mafisadi. Slaa ni mtu muhimu sana, ccm inatakiwa isilale hadi impate dk Slaa, mpambanaji wa kweli wa mafisadi.
Kwa kweli pamoja na ujio wa mwamba wa kaskazini, kuleta amsha amsha, Lowassa hakutakiwa kupewa nafasi ya juu kiuongozi. kwanza hajakijenga chama. Yeye alitakiwa kuandamana na MTU ambaye angeteuliwa kugombea urais kwenye mikutano yote ya campaign.
Kwa kweli Dr upo sahihi sana kwa maamuzi yako. Naomba tuheshimu maamuzi yake.