Nimetishwa, kushitushwa na kuogopeshwa na kauli hii ya Rais Magufuli. Alimaanisha nini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,339
120,843
Wanabodi,

Kwanza hebu sikiliza hii


Kwanza naomba kuanza na angalizo, kuwa kufuatia kazi nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, Watanzania wote, wenye mapenzi mema na ya dhati na taifa letu, na wenye nia njema na nchi hii, watamuunga mkono Rais Magufuli kwa asilimia 100% kwa 100% katika hatua mbalimbali anazochukua, kulisafisha taifa hili na uozo uliokuwepo, ukiwemo utumbuaji majipu, hivyo mimi namuunga mkono Rais Magufuli.

Ila pamoja na nia njema ya rais wetu kwa taifa letu, kuna baadhi ya kauli zake ni kauli za ukali toka moyoni mwake kuonyesha jinsi anavyochukizwa na rushwa, ufisadi na uzembe, na kule kutumbua majipu hadharani ni uthibitisho wa hili, ila kiukweli kuna baadhi ya kauli zake ni za ukali uliopindukia, na nyingine zinatisha!, kama kauli hii!, jee inaweza kuwa ni kauli tuu ya vitisho ili wahujumu hawa wasithubutu au inaweza kuwa ni kauli ya kweli?! na haya yanaweza kuwakuta wahujumu hawa?!.

Katika kuwakemea wafanyabiashara wanaoficha sukari, rais ametamka kwa ukali kuwa sukari sio sindano kusema kuwa wataificha, watawatafuta, wakiwapata, wataigawa bure sukari hiyo iliyofichwa, na wafanyabiashara hao watashitakiwa kwa uhujumu wa uchumi, na hawatafanya biashara tena nchini Tanzania katika maisha yao yote!. Yaani kumetungwa adhabu mpya ya kifungo cha maisha cha kutofanya biashara!, hili naliunga mkono!.

Ila katika kusisitiza hilo, kuna neno fulani rais Magufuli, amelitamka, kiukweli mimi neno hili limenishtua, kunitisha na kuniogopesha kidogo!. Kwa sababu kauli huumba, unaweza kutoa kauli kali, kauli hiyo ikaja ikaumba hili jambo, na jambo hilo likaja kutokea!, tatizo langu hapa sio utekelezaji wa hiyo kauli, bali matokeo ya karma za baadhi ya kauli za rais wetu!. Akitoa kauli za ukali namna hii, hizo kauli likaumba hilo jambo likatokea, unaijua karma yake ni nini?.

Naomba na wewe mwenzangu umsikilize vizuri rais na kwa makini, na unifafanulie alimaanisha nini?! au umemwelewaje?!, nisije nikawa nimeshtuka bure tuu, kutishika na kuogopesheka bure bila sababu, kumbe ni mimi ndio sikumwelewa vizuri rais wetu alimaanisha nini!.

Hebu tusaidiane, Jee kwa kauli hii ya Rais, wewe umeelewa nini?!.

Paskali.
 
Sometimes Bila viboko punda haendi hawa watu walidekezwaga sana enzi za jk hadi wakawa wanaidharau serikali actually sioni kama rais anakosea kwenye huu mwendo ila anachotakiwa kufanya ni kutengeneza mfumo wa kisheria utakaompa uhuru wa kudili na hizi incidents vizuri
 
Paskali huyu jamaa pamoja Na kuwa mwalimu kwa mda mrefu lakini bado ana mfumo dume ule wa Kanda ya ziwa .

Naomba washauri wake wasikate tamaa kumshauri huyu mwalimu kuhusu kauli zake awapo jukwaani Na maeneo mengine watu wa karibu Na huyu jamaa wanadai hashauriki anachokiamini ndo hicho hicho anacho address to the public. Kwenye hizi zama za kibepari Ngosha atashindwa vibaya.
 
Paskali huyu jamaa pamoja Na kuwa mwalimu kwa mda mrefu lakini bado ana mfumo dume ule wa Kanda ya ziwa .

Naomba washauri wake wasikate tamaa kumshauri huyu mwalimu kuhusu kauli zake awapo jukwaani Na maeneo mengine watu wa karibu Na huyu jamaa wanadai hashauriki anachokiamini ndo hicho hicho anacho address to the public. Kwenye hizi zama za kibepari Ngosha atashindwa vibaya.
Bepari ukimtisha anaondoa mitambo yake na pesa yake
 
Ni wewe Pascal?

Dalili zote za udicteta wa Hitler tunazishuhudia katika mazingira waliyokuwa nao Wajerumani enzi hizo.

Tofauti na enzi za Hitler sisi serikali yetu ni ya chama chetu haijabadirika ila kaingia Magufuli.

Shida za maovu yaliyosababishwa na awamu zilizopita ni zile zile na mahitaji ya kiuchumi ni yale yale. Cha msingi na cha ajabu hii ni serikali ya mtu si ya chama wala ya nchi.

TUTAFIKA TU
 
Back
Top Bottom