Nilimaliza chuo mwaka 2012. Baada ya kumaliza chuo nikajishikiza kwenye kikampuni kimoja kazi za temporary.
Baada ya miezi kadhaa mzee akaniita nisimamie miradi yake kipindi hicho kutokana na uzee maduka yalikuwa yameisha kwa kuibiwa.
Mwanzoni nilisita sana kwasababu nilikuwa namjua mzee wangu alivo. Mwishowe nikakubali baada ya kuona huku nyuma kuna mlolongo wa wadogo zangu waliohitaji kwenda shule na mimi ndo nilikuwa firstborn.
Mwaka wa kwanza ulikuwa mgumu sana kulingana na mazoea ya biashara aliyokuwa amezoea. Baadae nikamshauri tujiingize kwenye usindikaji wa unga.
Hatimaye baada ya muda tukafanikiwa kufungulia kiwanda mkoa mmoja nchini Mozambique (naomba nisitaje sababu ya privacy) nilifanikiwa kuikuza kampuni na kupata wateja wengi Sana na masupplier wa uhakika wa mahindi.
Mwaka juzi, baada ya kuona mambo yametiki mzee akanishauri nioe ili niweze kutuliza akili na kuachana na michepuko ila nikaomba nikishaoa ningeomba nijitegemee (ila nikamwambia itabidi nijitegeme kwahiyo itabidi aniandalie au anipe kianzio kwa kazi ambayo nilikuwa nimeifanya, kwasababu alitoa kwenye ajira).
Nikafanikiwa kufunga ndoa mwaka jana mwezi wa kumi. Baada ya kufunga harusi akaniaambia nipumnzike na mke wangu mpaka Januari mwaka huu nikamtii. Nikabaki na wife mzee akabaki na mdogo wangu na mama yangu mzazi, baadae mama akaugua akarudi nyumbani.
Mwezi wa kwanza niliporudi ili nikapewe hela aliyokuwa tuliyokuwa tumekubaliana ( 40mil) , nikakutana na mziki wa madeni ya masupplier wetu wengine wakiwa na miezi zaidi ya mitatu hawajalipwa.
Pia hakukuwa na balance hata ya kuweza kununua hata tonne moja ya mahindi. Na wadeni wote waliambiwa mimi ndo nina hela, waliposikia nimefika wakaja kunikaba. Kiukweli nilichanganyikiwa.
Mzee wangu alipoona hivo akasafiri kwenda South Africa, kwa kisingizio kuwa kuna vitu aliagiza havijafika akaniachia mzigo.
Kutokana na hali niliyoikuta niliwaomba wadeni wangu wanipe muda wa miezi miwili niwalipe. Nikaanza kusagisha watu wajumla jumla na wengine waliokuwa wanahitaji kutumia nembo yetu niliwauzia mifuko.
Nashukuru Mungu nilifanikiwa kulipa deni lote mwezi nne mwanzoni (deni 2,000,000 mts). Mwezi wa nne mahindi yakaanza kupatikana kwa wingi. Nikafanikiwa kununua kama tonne 20 ( kipindi chote sikutoka kuja kumuona mke ambaye sasa hivi ni mjamzito. Mwezi wa tano mwanzoni nikarudi nyumbani).
Nikakaa kwa muda wiki moja na nusu nilipotaka kurudi sasa. Mzee wangu sasa ndo akanigeuka. Akanambia hela ya mahari ndio mtaji wangu alionipa pia akaanza kumnyima mama yangu mzazi hata hela ya kutumia.
Wadogo zangu ambao wako chuo nao ada inasumbua hawapati hata hela za chakula. Mmoja yuko UDOM kuna mwingine yuko India anasoma Medicine.
Nilikuwa na kiwanja imebidi niuze nimtumie nauli huyu wa India arudi.
Akili yangu imestuck. Sina kazi kwa sasa, wadogo zangu wote shule ndo inaenda kufa. Nimejaribu kuomba kazi ila mpaka sasa sijafanikiwa hata kuitwa. Akiba yangu yote imeisha kwa kumhudumia mama mzazi, mke na wadogo zangu wote maana mimi ndo wananitegemea.
Natamani nimfungulie mashtaka lakini upande mwingine unambia niache tu labda ni upepo tu ndo umepita.
Naombeni msaada wa kimawazo naangamia mwenzenu