Nimestuka sana leo nilivyoambiwa nimelipiwa bili ,mpaka sasa natahamaki

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,864
Leo nilibahatika kutembelea moja ya mgahawa mjini kupata chochote kitu baada ya mihangaiko ya hapa na pale.kwenye mgahawa ule niliagiza chakula ambacho nilikuwa nakihitaji "menu ilikuwa ya nguvu".

Nilifanikiwa kumaliza msosi wangu. Vizuri nikaenda zangu kuosha mikono na kuelekea counter kwenda kulipia bili nionfoke zangu cha kushangaza wakati natoa pesa yule manager kaniambia umeshalipiwa kanirudishia pesa zangu nikastuka sababu nilikuja mwenyewe kwenye mgahawa ule na pia ndani ya mgahawa ule sikumuona mtu ninaye mfahamu.Ikabidi nimkazie jamaa nimelipiwa na nani wakati nipo pekee yangu akawa anakataa kupokea hela akisema huwa hawapokei bill mara mbili hivyo niende zangu nimeshalipiwa.Kumuuliza vizuri akasema jamaa mmoja hivi kavaa kapelo na miwani ndiye kanilipia ikabidi niondoke zangu nikiwa na hali ya mshangao

Kutoka nje nafungua simu niingie whatsap nakuta bundle hakuna palikuwepo na kiduka nje ya mgahawa ule nikaenda kuagizia vocha ya voda cha kushangaza yule muuza duka akakataa kupokea hela yangu akidai kuna mtu kanilipia aise nilikuwa mbogo lakini alisema bro kuna mtu kashalipa tayar nikamtupia vocha yake na kusepa zangu

Wadau leo nimekuwa nikijiuliza maswali mengi ni nani huyu anayelipia watu ? Ana nia gani ? Na kwann


Ile hoteli siendi tena na tayari wameshampoteza mteja

Mpaka sasa sielewi kwa mantiki ipi from nowhere uambiwe imelipiwa bili
 
Kweli kiongozi sio njozi
aisee..jaribu kutafiti muende hata wawili kwenye ile hotel tena...kila mtu akae siti yake wewe kaa sehem ileile uliyozoea na yule mwenzako mwambie akusaidie kuchunguza huyo mtu ni nani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom