Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,435
- 283,718
Kwa sasa hii Nchi haipaswi kutembelewa na yeyote anayeheshimika.
Sijui imekuwaje yaani
===
Mwanaharakati maarufu duniani wa masuala ya Elimu, Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa na mshindi mdogo zaidi wa Tuzo za Nobel, Malala Yousafzai, ametembelea Tanzania, ziara iliyoanza tarehe 9 Julai, 2025.
Mwaka 2013, Umoja wa Mataifa ulitenga tarehe 12 Julai kuwa ni siku ya Malala Duniani, kutambua jitihada mbalimbali za kuhakikisha wasichana wote duniani wanapata haki yao ya elimu.
Hii ilitokana na harakati za Malala kupigania haki ya elimu kwa wasichana, zilizopelekea kushambuliwa kwa risasi na kikundi cha Taliban akiwa anatoka shule kurudi nyumbani, akiwa na umri wa miaka 15 tu. Akinukuliwa kwenye tamko lake rasmi, Malala amesema: "Hii ni mara yangu ya kwanza kufika nchini Tanzania.
Nitasherehekea siku ya Malala kwenye jamii kwa kuonesha mshikamano na wasichana wa Tanzania, kupaza sauti zao na kujifunza kwenye mafanikio yao"
Kutokana na tarifa yake iliyochapishwa leo katika tovuti ya mfuko wake wa ufadhili (Malala Fund), imesema kuwa: akiwa Tanzania, Malala anategemewa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali, kutembelea wadau wa masuala ya elimu hasa elimu kwa mtoto a kike na kujionea kazi za sanaa na michezo zinavyohamasisha mwamko wa elimu katika jamii ya Tanzania.