Nimesikitishwa na kauli ya Clouds FM

Nakumbuka huyu jamaa hapa kwenye picha aliwahi 'kuporomosha' matusi hadharani kwenye kampeni za uchaguzi mdogo kule Arusha.
Baadaye kidogo clouds fm wakamwita kwenye mahojiano kwenye kipindi cha 'jahazi' na wakamsafisha sana, na 'wakahalalisha' matusi yake.
Leo hii sishangai kusikia clouds fm wakisema hayo waliyoyasema.

 
Mara nyingi sana hawa jamaa wanajisahau sana wanapotangaza habari zao,naisi hawajitambui kabisa juu ya nafasi yao.
 
Hili walilisema jana kwenye kipindi chao, Babra Hassani ndiye aliyelianzisha hili swala kwamba ni bora wawapotezee ukawa kwa kutosoma habari zao kwasababu ukawa wamesusia bunge wakati katiba ni ya watu wote, PJ na Mbwiga nao wakaunga mkono.
 
Tz kuna radio station nyingi na wanatangaza vizuri sana bila kubagua , sasa hao clouds kupitia power breakfast wakisitisha kutangaza habari za UKAWA wengine watatangaza tu......MIMI KAMA MWANANCHI WA TZ NAPENDA HARAKATI ZA UKAWA
 
Katika list ya radio bora Africa iko ndani ya top 10 imeshika no 7 na radio pekee Tanzania ktk top 10 ya the best Radio station in Africa.
 

Yaan nikisikia mtu anasema anasikiliza clouds fm au tbc radio simtofautishi na mtu anayesoma gazeti la uhuru au mzalendo maana wote ni kama wametokea uzao mmoja
 

Pole bado unasikiliza clouds tu ndugu yangu pole sana kama unataka kipindi bora cha asubuhi sikiliza Morning Magic ni bonge ya kipindi aisee..!
 
Sijui ni lini nilibahatika hata kwa dakika moja kufungua, wachilia mbali kisikiliza Clouds Fm...
 
Ni jambo la kustaajabisha kuona kuna watu bado wanasikiliza Clouds au Uhuru na TBC Fm...
 
Hao Clouds nina muda sana siwasikilizi walishapoteza haiba kwa watanzania wengi tu sababu ya watangazaji wao makanjanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…