Wana jamii forums wenzangu kama siku tatu zilizopita katika jiji la Dar es Salaam kuna ajali mbaya sana ilitokea maeneo ya Buguruni/Tabata kama sikosei. Ajali hii imesababisha vifo na vilema kwa wapendwa wetu. Siyo jambo zuri hata kidogo ni mwendawazimu tu ndo anaweza kufurahia tukio lile.
Kilichonisukuma kuandika thread hii ni video moja ya tukio lile ambayo inamwonyesha ndg yetu mmoja na mke wake wakilia kwa uchungu sana, baba akiwa amembeba mwanaye ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 au 13 akiwa amepasuka kichwa na ubongo umemwagika kabisa, kama mzazi nimeumizwa sana na video ile kwa kweli mtu aliyepiga video ile na kusambaza kwenye magroup ya facebook na kwingine hakuitendea haki familia ile na hata mtoto yule ambaye ndoto zake zimezimwa na ajali ile. kwani ametoka nyumbani asubuhi akielekea shule akiwa na ndoto zakuja kuwa mtu fulani siku fulani. Maskini hakurudi kumwona Dady na Mum.
Hebu fikiria mtoto anaamka asubuhi anakuaga baba/mama naenda shule nawe kama mzazi unampatia mipango ya siku nzima baada ya shule afanye nini kwa siku ile. Ghafla kabla hata hujaondoka nyumbani kuelekea kazini ama kwenye biashara zako, unapata taarifa mwanao kapata ajali, unaondoka kwa haraka sana ukiwa hata hujavaa shati unakutana na situation kama ile, kweli mwanao mpendwa kapata ajali, tena mbaya na imegharimu uhai wake, kichwa kimepusuka chote. Unachanganyikiwa kabisa usijue nini cha kufanya kwa wakati huo. Unaishia kumbeba mwanao ukilia kwa uchungu.Mtu mmoja kwa sababu tu anasimu yake mkononi yeye kwa raha kabisa anarekodi tukio lile na kulirusha kwenye mitandao ya kijamii.
Watanzania wenzangu hebu tuwe na utu na huruma kwa wenzetu. Mtu yule mimi simfahamu lakini kupitia jamii forums naomba nitoe pole kwa familia ile. Binafsi nimeumia sana, yule ndg amepata wakati mugumu sana kwa tukio lile, emembeba mtoto ambaye kwa kuchanganyikiwa alikuwa anadhani bado yuko hai, na akiwa anahitaji msaada ampeleke mwanae hospitali kila aliyekuwa anamwona anamkimbia.
Sina maneno mazuri ya kuelezea hili tukio, lakini nitoe tu pole kwa familia hii.
POLENI SANA WAFIWA WOTE