'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by We acha tu, Oct 12, 2011.

 1. W

  We acha tu New Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza usiniamini haya niyaelezayo hapa, lakini ni ukweli mtupu na sasa sijui namna ambavyo ninaweza kutoka katika uhusiano huu maana sitaki kumkosesha raha mke wangu, ni kwamba mwaka 2007 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja aliyekuwa katika chuo kimoja mjini Morogoro wakati huo akiwa field Moshi kwenye moja ya taasisi ya serikali, basi nikatupa ndoano tukawa pamoja na hata aliporudi chuo kumaliza kozi yake.

  mwaka mmoja baadaye alimaliza akarudi moshi akaanafanya kazi kwenye taasisi moja binafsi tutaka pamoja tena nilimtafutia chumba nikamweka huko nikawa mimi kama baba mwenye nyumba, siku moja tukiwa kwake tulikorofishana nikaondoka kwake nyumbani bila kuaga wakati naondoka njiani alinipigia simu sikupokea kama mara tano, nikazima simu. Nilipofika nyumbani akapiga simu ya mke wangu masikini alipokea tu, yule binti akasema 'Mwambie mume wako kesho anipe sh. 40,000 nikatoe mimba yake, nampigia simu yake ajidai kazima'.

  Mungu wangu basi mke wangu kwa hekima akaniuliza "mumwe wangu haya aliyosema huyu dada ni kweli au naota? nikamuuliza amesema nini na ni nani? akasema kuna dada namba yake hii inafanana na yangu na yako (maana nilichonga namba zinazofafa zote zinatofautiana namba ya kwanza tu) anasema umpe hela kesho akatoe mimba yako.

  Nikamwambie hebu tulale tuzungumze kesho mke wangu usiku huu ni mwingi tutagombana bure kwa ajili ya simu si unajua mitandao? nikajitetea na hoja yangu ikakubalika. Asubuhi ilipofika tukaanza mjadala lakini nilipojitetea alikubali lakini kadiri tulivyokwenda alizidi kubadilika mke wangu kutokana na fikra mpya zinavyomjia kutokana na maneno yale ya binti yule hata hivyo tuliendeleea hivyo hadi alipokutana naye yule binti baada ya kumfuata kazini kwake na kupigana naye.

  Baada ya ugomvi huo mimi nikamwambia yule mwanamke nimemuacha karibu mara tatu na kweli nilimuacha kama miezi mitatu lakini baadaye nilirudi tena nikamuacha nikarudi tena nikamuacha nikarudi tena hadi leo hii tumehama sehemu ambayo mke wangu alipajua alipokuwa anaishi na sasa nimempangia chumba sehemu nyingine lakini mke wangu tangu alipogundua nipo na binti huyo haniamini tena kwani tangu nimemuoa mwaka 1997 hadi leo hakuwahi kuhisi nimetoka nje ya ndoa hadi tatizo hilo la binti huyo wa kimasai, sielewi nitatokaje na nimemwahidi kwamba nitamuo mke wa pili kwa vile mimi ni mwislamu lakini mke wangu hataki anasema nikimuoa huyo yeye anarudi kwao Tabora sasa nifanyeje?

  Naomba mnishauri wote nawapenda mke wangu ambaye tuna watoto watatu mmoja ana umri wa miaka 14, wa pili 12 na wa tatu miaka minne na nusu. je nifanyeje?
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  duh! hii kali.

  sasa muheshimiwa hapa sasa itabidi tuu ukubali kuwa kunasehemu utachukiza ili ufuraishe upande mwingine.
  kwa kuwa huyo demu sio mkewe..basi itabidi ukubali kurudi kwa mkeo na utulie nae. ila sasa nataka kukwambia kuwa ukisha amua kurudi na kukaa na mkeo basi wewe masisha yako yote utakuwa unajaribu kupata trust ya mkeo ambayo umeshaipoteza...... kiufupi umejifunga jela mara mbili!!!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  lol..................................

  unataka tukushauri...'how to eat your cake and still have it '.....???????
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hebu heshimu ndoa yako mkuu......................huh
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,759
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  ukome kuchezea feelings za huyo wa pembeni,maisha ya sasa ni magumu,kwa hao watoto uliokuwa nao,unataka nini tena?mke ndani mzuri unae.kuhangaika hangaika hakuna faida yoyote ile.wewe ni sawa sawa na mchimba kisima,utaingia mwenyewe.shauri yako
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,759
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  wanaume kama nyinyi,mnafaa kuchunwa tu,maana hamna adabu
   
 7. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mkuu kuna ulazima wa kuwa na mke pamoja na hawara??? mimi nadhani kwa hali ya sasa si vizuri kutokuwa na msimamo na matokeo yake mnatumia dini kama kigezo cha kumalizia tamaa za mwili
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ungekua unampenda mke wako ungetulia tangu mwanzo na swala la kua na mke mwingine ungemhusisha kabla ya kujiweka kwenye mitego usiyoweza kuhimili.

  Sasa you hav to deal with your mess...umeshajua kwamba kuendelea na mke wako inakubidi kuachana na huyo binti maana nyumba ndogo na mke mdogo vyote havikubaliwi na mke wako!!!Zaidi ya hapo ongeza unga uendelee kulikoroga mpaka liwe ugali alafu ushindwe kulinywa!!!
   
 9. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kajishika mwenyewe na anadai kashikwa sasa cjui anataka msaada gani maana kuna maamuzi mengi kashachukua
   
 10. sunshine1

  sunshine1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Lizzy huwa unanikonga moyo na point zako!
  Huwa unawapa bila chenga.
  Big up :poa

   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Boss

  Actually nilitaka kumshushia povu la karne huyo lofa

  Yani wewe unacheat, ukishikwa unakimbilia JF?? Si kwamba mie ni msafi hapana, but madhara na tahadhari za cheating ziko wazi, so the dude knew exactly the risks associated

  in addition, siamini kama mwanamke anaweza kupiga simu hivyo kama wewe hujamuonyesha kwamba unamdharau mkeo

  IN MANY CASES NI SISI WANAUME TUNAOWADHARAULISHA WAKE ZETU KWENYE MECHI ZA UGENINI NA KUWAPA CONFIDENCE YA KUWEZA KUWADHARAU WAKE ZETU

  USHAURI KWA MEMBER MWENYE POST 1.... JUST BE A MAN!!
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  huwezi kua na wote wawili. chagua mmoja utulie nae, tena kama utaweza iwe ni yule uliapa kua nae maisha milele
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watu wasiojua kukubali makosa yao kwa visingizo utawaweza basii....yani utadhani huyo dada ndie aliekua mwamuzi kwaajili yao wote!!
  Asante deaest....
  Wanaboa kweli watu waojua wamefanya makosa ila hawataki kuyakubali.
   
 14. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hana msimamo kwa jinsi inavyoonyesha naendeshwa sana na huyo bi mdogo kiasi cha kwamba katika maelezo yake anatetea kule nje kama hakuna njia mbadala
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hasara kweli kwa mkewe!!

  Mtoa mada unajua kabisa ili uwe na ndoa ya amani unahitajika kufanya nini...fanya hicho kitu acha kutafuta short cut maana hamna hata moja!!Amua kama unamtaka mke au nyumba ndogo kisha ujitulize hapo!!!
   
 16. Waminshari

  Waminshari Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sijawahi ku comment Leo Mara ya kwanza. Sasa boss umeshindwa kuheshimu ndoa yako kwa ajili ya tamaa? Tumia akili watoto wako ni wakubwa. Uko tayari waone baba Yao kicheche. Achana na mambo ya ajabu in the name of utaoa mke wa pili. Kwani hata hiyo dini iliyoruhusu uoe wake watatu inataka masharti ya wewe kumheshimu mkeo. #nihayotu
   
 17. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mtoa mada katika mtililiko wake kajaribu justify kuhusu nyumba ndogo kwanza kamdhalilisha mkewe kwa kupigana na hawala ... pili kile kitendo cha mke kuambiwa masuala ya mimba lilikuwa ni tusi tosha na njia pekee ya kumwacha mke.. pili jamaa hana siri kwa hawara hadi anatoa namba ya mke sasa hapo kweli kuna nini la maana
   
 18. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Huo ni uzinifu tu na uislam hauruhusu mtu mchakachuane alafu mkitosheka muoane hii haipo we simple Ni IRRESPONSIBLE
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  mbona umehesabu wanao,ile mimba ya small house imeishia wapi? nakushauri mngeitana kikao ww,mkeo, huyo binti mmasai na mmasai mwenzie anaekushikia lindo wakati ukiwa kwa mkeo. mkubaliane kugawana madaraka na mipaka. fuata ushauri wa lizzy, koroga weeh ukishakua ugali ule japo kwa shumvi manake unga ukizidi maji tena itakua balaa!
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Shekhati FaizaFoxy uko wapi?

  Mbaba (umeoa 1997), kweli umechemsha sana na kama alivyosema MTM people do cheat; lkn wewe umeonesha kumdharau sana mkeo kwa mistress wako.

  Unataka kujinasua kwa nani? Kama ni kwa hawara yako, muite nyumbani kwa mkeo, ita baadhi watu wenye heshima; muombe radhi mkeo na umpige stop huyo mwanamke mbele ya wote. Lipia damage yoyote na let it be the end!

  Sidhani utakuwa mjinga kiasi cha kutaka kujinasua from the home (wife, kids n everything) you have build for the past 15 or do years. Imagine dunia ya leo mdada wa watu amekuamini muda wote huo mpaka mlipolikoroga wazi wazi; we mwenyewe unaona humu watu wanavyotaka kukagua simu za waume zao!

  Walahi nakuapia muache huyo mkeo halafu oa hicho kichomi, tutakucouncil tu humu.
   
Loading...