We acha tu
New Member
- Aug 1, 2011
- 3
- 1
Unaweza usiniamini haya niyaelezayo hapa, lakini ni ukweli mtupu na sasa sijui namna ambavyo ninaweza kutoka katika uhusiano huu maana sitaki kumkosesha raha mke wangu, ni kwamba mwaka 2007 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja aliyekuwa katika chuo kimoja mjini Morogoro wakati huo akiwa field Moshi kwenye moja ya taasisi ya serikali, basi nikatupa ndoano tukawa pamoja na hata aliporudi chuo kumaliza kozi yake.
mwaka mmoja baadaye alimaliza akarudi moshi akaanafanya kazi kwenye taasisi moja binafsi tutaka pamoja tena nilimtafutia chumba nikamweka huko nikawa mimi kama baba mwenye nyumba, siku moja tukiwa kwake tulikorofishana nikaondoka kwake nyumbani bila kuaga wakati naondoka njiani alinipigia simu sikupokea kama mara tano, nikazima simu. Nilipofika nyumbani akapiga simu ya mke wangu masikini alipokea tu, yule binti akasema 'Mwambie mume wako kesho anipe sh. 40,000 nikatoe mimba yake, nampigia simu yake ajidai kazima'.
Mungu wangu basi mke wangu kwa hekima akaniuliza "mumwe wangu haya aliyosema huyu dada ni kweli au naota? nikamuuliza amesema nini na ni nani? akasema kuna dada namba yake hii inafanana na yangu na yako (maana nilichonga namba zinazofafa zote zinatofautiana namba ya kwanza tu) anasema umpe hela kesho akatoe mimba yako.
Nikamwambie hebu tulale tuzungumze kesho mke wangu usiku huu ni mwingi tutagombana bure kwa ajili ya simu si unajua mitandao? nikajitetea na hoja yangu ikakubalika. Asubuhi ilipofika tukaanza mjadala lakini nilipojitetea alikubali lakini kadiri tulivyokwenda alizidi kubadilika mke wangu kutokana na fikra mpya zinavyomjia kutokana na maneno yale ya binti yule hata hivyo tuliendeleea hivyo hadi alipokutana naye yule binti baada ya kumfuata kazini kwake na kupigana naye.
Baada ya ugomvi huo mimi nikamwambia yule mwanamke nimemuacha karibu mara tatu na kweli nilimuacha kama miezi mitatu lakini baadaye nilirudi tena nikamuacha nikarudi tena nikamuacha nikarudi tena hadi leo hii tumehama sehemu ambayo mke wangu alipajua alipokuwa anaishi na sasa nimempangia chumba sehemu nyingine lakini mke wangu tangu alipogundua nipo na binti huyo haniamini tena kwani tangu nimemuoa mwaka 1997 hadi leo hakuwahi kuhisi nimetoka nje ya ndoa hadi tatizo hilo la binti huyo wa kimasai, sielewi nitatokaje na nimemwahidi kwamba nitamuo mke wa pili kwa vile mimi ni mwislamu lakini mke wangu hataki anasema nikimuoa huyo yeye anarudi kwao Tabora sasa nifanyeje?
Naomba mnishauri wote nawapenda mke wangu ambaye tuna watoto watatu mmoja ana umri wa miaka 14, wa pili 12 na wa tatu miaka minne na nusu. je nifanyeje?