Nimeshida 5000$

Infopaedia

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,231
1,487
Wakuu leo jioni nimerudi nyumbani toka kwenye mihangaiko yangu na kukuta msg hii kwenye simu yangu.

''Congratulation you have win 5000$ call free this number 002399882137 immediately''

Sijapiga hiyo number sababu akili yangu hainipi kabisa. Kwanza sijawahi kushiriki shindano lolote hivi karibuni, pili hiyo number ya simu ni mashaka. Spelling za neno immediately wameandika ''immediatly'', ujumbe hauna nukta wala mkato. Hayo yote yananifanya chale zinicheze. Aliyewahi kupokea aina hii ya msg na anajuwa kinachoendelea naomba anipe habari zaidi.
 
ukipiga tu vihela vyako vyoote vya kwenye M-PESA au TIGO-PESA au AIRTEL-MONEY ndio sahau vinayeyuka immediately.
 
Huu mchezo mbona wa kizamani unaotumiwa na wajinga wa kinegeria kuganga njaa. Futa hiyo msg mwanangu uendelee na mambo mengine ya maana. Wako wengi Sinza kwa sasa wakihadaa watu kuwa wana deals za maana wakati ni vibaka wanaopaswa kuchomwa moto. Bahati mbaya mabinti zetu vihiyo wanawapapatikia na kuwawezesha kupata vibali vya kuishi chini ya kisingizio cha ndoa uchwara. Fungueni macho mnaliwa mchana.
 
Shauri yako!
mi niliagiziwa check ya $3,500 kuwa nimeshinda $300,000, nikaambiwa nikiipata hiyo 3500 niwapigie b4 i cash it. know what happened? Nilivyopiga niliambiwa niagize security fees za $2,000 kwa njia ya Western Union ili niagiziwe pesa iliyosalia!! Wajinga ndo waliwao!It was a Fake check!!!!
 
wanaita scam messages, pia wanatuma hata emails na kuomba particulars kibao kwa madai email yako imeshinda.....ni uongo
 
Mkuu umesema kweli ...... hawa jamaa watawaumiza sana dada zetu kwa sababu wamefanya hivyo karibu kila nchi walipotia team. Mashori mpo hapo ?? accent za Naija si mnazinyaka kwenye filamu zao? Ogaaaa
 
Huku Malawi kampuni za simu (TNM na Airtel) zimewatahadharisha wateja wao kuhusu meseji hizo za kitapeli. Nadhani na kampuni zetu zingefanya hivyo kuwaokoa baadhi ya ambao wanaweza kuingizwa mjini.
 
Wakuu leo jioni nimerudi nyumbani toka kwenye mihangaiko yangu na kukuta msg hii kwenye simu yangu.

''Congratulation you have win 5000$ call free this number 002399882137 immediately''

Sijapiga hiyo number sababu akili yangu hainipi kabisa. Kwanza sijawahi kushiriki shindano lolote hivi karibuni, pili hiyo number ya simu ni mashaka. Spelling za neno immediately wameandika ''immediatly'', ujumbe hauna nukta wala mkato. Hayo yote yananifanya chale zinicheze. Aliyewahi kupokea aina hii ya msg na anajuwa kinachoendelea naomba anipe habari zaidi.
Hawa ni matapeli tena wasioenda shule (you have win) yaani
 
Asanteni sana wakuu kwa kunipa ushauri kuntu na kutoa muda wenu kuandika. Kwakweli sikujihangaisha tena na ile msg. Tunapokutana na vitu kama hivi tuvilete hapa jamvini ili wengine nao waelewe kinachoendelea. Hiyo itasaidia kuwaokoa wingine wanaoweka tamaa mbele kufikiri nyuma. Asanteni wote.
 
wakuu leo jioni nimerudi nyumbani toka kwenye mihangaiko yangu na kukuta msg hii kwenye simu yangu.

''congratulation you have win 5000$ call free this number 002399882137 immediately''

sijapiga hiyo number sababu akili yangu hainipi kabisa. Kwanza sijawahi kushiriki shindano lolote hivi karibuni, pili hiyo number ya simu ni mashaka. Spelling za neno immediately wameandika ''immediatly'', ujumbe hauna nukta wala mkato. Hayo yote yananifanya chale zinicheze. Aliyewahi kupokea aina hii ya msg na anajuwa kinachoendelea naomba anipe habari zaidi.
pumb zao mimi wamenitumia saa11: 27: 39 wakaniambia nipige namba 002399882116
 
Hao ni wahuni jamani lets ignor them. wengine wanakuja na gear ya deal za madawa feki kazi ni kutafuta deal za fedha za wajinga. lets be carefull on this.
 
Kuna jamaa yangu alitumiwa e-mail ikimuomba akubari kufanya deal ateuliwe kama mrithi wa jamaa aliyekufa uko ulaya na kuacha pesa nyingi benk. Jamaa kakubari akaombwa na kutuma kopi ya paspoti, akaunti namba na bank statement japo ajaombwa pesa,mi nimemwambia umeshaibiwa lkn yeye amejipa moyo ni dili la kweli sababu akutoa pesa. Bado najiuliza hawa jamaa wananufaika vipi na usanii huu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom