Nimepoteza bima ya afya na ninaumwa sana

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,708
1,553
Habari ndugu,

Kifupi nina tatizo hivyo naomba msaada wa ushauri, nimepoteza bima ya afya na nina tatizo hivyo inatakiwa nifanyiwe operation haraka iwezekanavyo! Hivyo naomba ushauri wa kujua njia ninazoweza kuzifuata ili niweze kurew tena bima upesi ili niweze kupata huduma.

Nitashukuru kwa watakaonishauri juu ya hili.
 
Pole ndugu, nami nasubiria jibu kuna mtu kapoteza card pia
 
Nenda ofisi za NHIF wakupe temporary permit then utaratibu wakutengenezewa ID mpya utafuatwa,ukumbuke kubeba passport size 1
 
Nenda ofis za bima NHIF jiran nawe watakupa barua ya kwenda hospitali unayotaka kwenda tibiwa,ila kupata kadi mpya utalipia sh.elfu20 kwa ajili ya kadi ilopotea ukiambatanisha na loss reportkutoka polisi, all in all first of all utapewa kwanza barua ya kwenda kutibiwa hayo mengine yatafuatia utapohitaj kadi nyingine
 
Kama Kuna hospitali ushawahi kutibiwa na bima na zile document unazo nenda hapo kisha watakupa namba ya kadi yako
then hospital yoyote ukienda na namba ya kadi yako still unakubalika maana ikiingizwa katika system itasoma ditails zako zote pasipo na shaka.
Lakini pia kama hapo pameshindikana nenda ofisi zozote za bima zilizo karibu nawewe(Za Wahusika Ulikokata Bima) Unapewa barua ambayo itakuwa na namba ya kadi yako na uthibitisho wako so unaweza tibiwa kwa barua hiyo mahala popote huku ukiwa taari umepewa utaratibu wa namna ambavyo utapata kadi mpya
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Pole sana..

Fika ofisi za Bima yako ya afya waeelezee tatizo lako... watakusaidia...


Cc: mahondaw
Kama ni urgent operation akatibiwe kwanza ila nadhani cost itamuhusu make kama ni kupata bima mpya mpaka ajaze form na huchukua muda fulani labda kama watatake ishu yake serious wamfanyie haraka
 
Jambo la kwanza unatoa taarifa kwa Bima yako. Pili pata loss report ya Polisi. Baada ya hapo nenda kwenye ofisi ya Bima yako upewe barua ya muda wakiwa wanaendelea na mchakato wa kadi nyingine mpya.

Pole sana
 
Nenda Polisi kapate loss report alafu nenda ofisi ya bima utapewa akaunti ya kilipia benki Tsh 20,000/= ukipeleka risiti watakupa kibali temporary kwa wiki moja km kadi haijatoka utaongezewa siku mpaka itakapo toka!
 
pole nenda ofisi ya bima afya ya afya yakaribu na wewe utapewa barua ya muda huku unangaikia kitambulisho kopya hakikisha umeenda na paspot size 1
 
Back
Top Bottom