Habari Wana Jamvi,nahitaj Msaada Wenu Naona Kiza Nimepotea Kwenye Msitu Wenye Giza Na Mbwa Mwitu Wakali. Mimi Ni Kijana Below 25 Years,nimefanikiwa Kukwepa Anasa Zote Lakin Nimejikuta Nadumbukia Kwenye Uraibu Wa Kununua Madada Poa.
Kama Kijana Mwenye Heshima Mtaani Nisiyeacha Ibada(swala Tano) Nimeshindwa Kuwakwepa Madada Poa Tena Wa Bei Kdogo Elfu 50,70 Kwa Mwezi Naweza Nunua Hata 2 Au Nikijizua Sana Mmoja Na Huwa Sinunui Wa Bei Rahc.Naumia Sana Kwanza Na Hii Tabia Pili Kupoteza Pesa Tatu Napoteza Heshima Yangu Binafsi Ingal Huwa Nanunua Mbali Na Eneo Wanaonijua Naona Kama Nina Nidhamu Ya Uwoga Naonesha Heshima Kwa Watu Ikifika Usiku Nakuwa Fisi.
Pesa Yangu Haifany Maendeleo Zaid Ya Hyo Anasa. Sivuti Bangi,sigara Wala Pombe. Naomba Kusaidiwa Kuachana Na Hii Tabia Nateseka Sina Amani Ya Moyo.Nipo Kwenye Stage Ambayo Nisiponunua Malaya Ndani Ya Mwezi Naanza Kama Kuumwa Basi Ntakopa Pesa Ili Nikanunue.
Ni Kipindi Cha Mwaka Mmoja Na Nusu Tangu Nianze Kununua Nishalala Na Wanawake 13 Au 14,kuna Kpind Niliacha
Kwanza pole kwa hiyo changamoto ya kushindwa kuiacha hiyo tabia. Pili inaonekana kwako hiyo ni tabia mbaya na ndiyo maana inakuumiza kila wakati na kutamani kuiacha.
Kwa kawaida ukiona kuna jambo unalifanya halafu baada ya kulifanya unajutia basi jua hilo jambo ni baya kwako siyo kwa watu wengine, kwako wewe.
Unaweza kuachana na hiyo tabia kama utafanya yafuatayo kwa kumaanisha kutoka akilini mwako na moyoni. Zingatia, maanisha akilini na moyoni. Kama kimojawapp kati akili hakipo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea na huo ulevi.
Fanya maamuzi magumu. Maamuzi ya kuacha hiyo tabia kwa dhati ndiyo njia pekee ya wewe kuachana na hiyo tabia. Amua kuanzia leo hii tarehe 02/11/2023 kuwa hutanunua tena ngono na badala yake amua kuoa au kuwa na mpenzi mwenye msimamo, anayehiheshimu, na ambaye utasumbuka kumtongoza na kumpata.
Kuwa na nidhamu. Ukishafanya maamuzi, jipe amri ya kuhakikisha kuwa hutanunua malaya kwa miezi 6 ijayo na hakikisha unasimamia maamuzi yako. Akili yako itakuwa inakukumbusha ununue malaya pindi mwili wako ukijaa na hisia lakini jitahidi kudhibiti. Dhibiti akili yako, mwili wako na hisia zako, siyo kuruhusu kudhibitiwa na vitu hivyo.
Ukifanikisha kufanya hivi kwa miezi 6, basi utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kuacha ulevi wako.
Zingatia pia, tabia zote mbaya ni matokeo ya kutokuwa na malengo na misimamo.
Weka lengo la kifedha ambalo litakufanya kila mwezi uwe na sehemu ya kupeleka pesa. Lengo hilo liwe ni lengo chanya siyo lengo hasi.
Wote mnaonunua malaya acheni bwana hiyo tabia mbaya, na acheni udomo zege. Tafuteni wanawake ambao mtahangaika kuwapata. Jifunzeni kutongoza basi.
Mimi natoka. Utekelezaji mwema