Nimeporwa Nguo zangu hapa Karume na Askari wa Jiji

rajiih

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
462
688
Habari wana JF,

Poleni na majukumu ya kazi.

Twende kwenye maada husika Mimi ni machinga mdogo pale Soko la Karume kwa mara kadhaa nmekua nikikubwa na msukosuko wa kubebewa Nguo zangu na hawa Askari Jiji Sina wa kumlaumu zaidi ya serikali yangu kwani wamevunja mabanda wakapora vilivyomo kisha wakapiga stop uuzaji mbele ya hizi kingo za barabara.

Tukakubali ikabidi kwa kutafuta ridhiki tuwe tunashika mikononi napo wanakuja kutupora na kudai Faini kubwa mnoo hii sio sawa Mkuu wa mkoa na Rais wake waweke malipo ya kila mwezi kwa vijana kama posho maana tunajitahidi mno lakini matokeo yake ni kuibiwa tena na vijana wanaotumwa na serikali yetu.
 
Upo eneo la karume eneo la karume linajulikana ni eneo lililozungukwa na machinga, hawa mgambo wamekuwa wakinyanyasa sana watu kila siku wanataka uwape buku kama rushwa, nq baya zaidi hapiti moja akipita huyu anakuja mwingine usipo angalia utatoa mpaka 3000 kwa siku, wahusika wasaidieni hawa vijana.
 
Pole sana mkuu cha ajabu hayo hawezi kufanyiwa mtu anayemiliki fremu mikocheni au Masaki ila wewe mwenye elfu Tsh.60 yako ya mtaji ndio unafanyiwa umafia ili urudi Tsh.O!

Mwenye Billion 10 haguswi biasharani kwake.
 
Pole sana mkuu, hivi wale wenye vibanda ndani ya soko la karume hawalipi kodi,je nafasi kule ndani zimeisha? Kwa upande wa kariakoo kulikuwa kuna malalamiko kutoka kwa wenye maduka wanadai mauzo yamepungua kwao kwa sababu machinga wanauza bei rahisi kwakuwa hawalipi kodi hivyo inawazuia wao kuwa na mauzo mazuri,unakuta mtu ana mali ya zaidi ya mil.5 amepanga barabarani kwajili ya kukwepa kodi (ya serikali na pango)
 
  • Thanks
Reactions: Cyn
Pole sana mkuu,hivi wale wenye vibanda ndani ya soko la karume hawalipi kodi,je nafasi kule ndani zimeisha? Kwa upande wa kariakoo kulikuwa kuna malalamiko kutoka kwa wenye maduka wanadai mauzo yamepungua kwao kwa sababu machinga wanauza bei rahisi kwakuwa hawalipi kodi hivyo inawazuia wao kuwa na mauzo mazuri,unakuta mtu ana mali ya zaidi ya mil.5 amepanga barabarani kwajili ya kukwepa kodi (ya serikali na pango)
Mkuu uulizaji wako ni wa kisiasa na sijajua umri wako na Kazi yako kwa ujumla Uzi huu unamgusa MTU wa nitoke Nile nilale nife na njaa labda nikuulize swali dogo tu?!

Hivi pale Machinga complex na hapa Karume Ni masoko ya akina nani labda?! Ukifika pale Karume Kuna Bango kubwa na lenye maandishi makubwa kuwa Karume na soko kuu la wafanyabiashara wadogo wadogo halafu mambo ya unyang'anyi yanafanyika mbele ya hilo hilo Bango

Kama unauhakika na sehemu ya kazi chakula na Makazi wacha kusema siasa kwa sehemu ambayo vijana wenzako wanapotafutia ridhiki zao.
 
Hapana mkuu huenda umenielewa tofauti na nilivyouliza,pia umesema kuwa masoko hayo ni ya wafanyabiashara wadogo kwa maana ya kwamba ni ndani ya soko na sio nje ya soko,kufanya biashara nje ya soko ni hujuma kwa wafanyabiashara wadogowadogo wanaolipia kodi na fremu kwenye masoko hayo,ukifanya biashara ndani ya soko hautasumbuliwa wala kuporwa mali yako na wala hutokuwa kero kwa wapita njia barabarani
 
Huo unaofanyiwa ni uonevu, zaidi ni uporaji. Msikubali kuendelea kuonewa, unganeni mhakikishe mnafikisha malalamiko yenu kwa mkuu wa Mkoa,

Pia, hakikisheni nyie binafsi mnakjwa na umoja wenu msikubali kuona mwenzenu akiporwa mali zake huku wengine mnatazama au kukimbia, umoja wenu ndio nguvu yenu, hao migambo ni wezi.
 
Karibu huku Kijijini uje tulime na kufuga. Kamwe hutowaona hao askari wa Jiji, au wale wa kawaida wakikupora mavuno/mali yako.
 
Hapana mkuu huenda umenielewa tofauti na nilivyouliza,pia umesema kuwa masoko hayo ni ya wafanyabiashara wadogo kwa maana ya kwamba ni ndani ya soko na sio nje ya soko,kufanya biashara nje ya soko ni hujuma kwa wafanyabiashara wadogowadogo wanaolipia kodi na fremu kwenye masoko hayo,ukifanya biashara ndani ya soko hautasumbuliwa wala kuporwa mali yako na wala hutokuwa kero kwa wapita njia barabarani
Mkuu una mshahara mzuri pengine na hujawahi pitia vijibiashara ambavyo vinafanyika Maeneo ya nje pale " Kijana unajikwamua na kupata 100k kama mtaji ukaamua zako kwenda kupoint mtumba kadhaa Sawa na pesa yako wakati ukiwa katika harakati zako za kusaka wateja na nguo zako mkononi wanatokea Askari Jiji na kukupora hizo nguo tena kwa ubabe mkubwa na kudai Faini kubwa ambayo hauna mfukoni mwako wakati huo" Vuta picha ya hali gani ya machungu anayapata huyu kijana juu ya serikali na chochote kipitacho mbele yake wakati huu ikiwa wakati huo hajaiba wala kumpora mtu Wacha kusapoti upuuzi kwa kuwa uko na maisha mazuri hivi Sasa. Nikukumbushe kuna wakati halmashauri ya Soko ilikua inapitisha ushuru kwa kila Machinga pale na vijana tulikua tunalipa vyema Pasi na shaka

Uasi wa chuki na serikali kuu huwa unaanza taratibu na ipo siku nguvu ya vijana wasio na ajira itaonekana Endeleeni kula Mishahara minono katika ajira zenu
 
Huo unaofanyiwa ni uonevu, zaidi ni uporaji. Msikubali kuendelea kuonewa, unganeni mhakikishe mnafikisha malalamiko yenu kwa mkuu wa Mkoa,

Pia, hakikisheni nyie binafsi mnakjwa na umoja wenu msikubali kuona mwenzenu akiporwa mali zake huku wengine mnatazama au kukimbia, umoja wenu ndio nguvu yenu, hao migambo ni wezi.
Kila Jambo lina mwisho watanzania sio wanyonge
 
Habari wana JF,

Poleni na majukumu ya kazi.

Twende kwenye maada husika Mimi ni machinga mdogo pale Soko la Karume kwa mara kadhaa nmekua nikikubwa na msukosuko wa kubebewa Nguo zangu na hawa Askari Jiji Sina wa kumlaumu zaidi ya serikali yangu kwani wamevunja mabanda wakapora vilivyomo kisha wakapiga stop uuzaji mbele ya hizi kingo za barabara.

Tukakubali ikabidi kwa kutafuta ridhiki tuwe tunashika mikononi napo wanakuja kutupora na kudai Faini kubwa mnoo hii sio sawa Mkuu wa mkoa na Rais wake waweke malipo ya kila mwezi kwa vijana kama posho maana tunajitahidi mno lakini matokeo yake ni kuibiwa tena na vijana wanaotumwa na serikali yetu.
Tiini Sheria bila shuruti. Barbara na hifadhi zake zinalindwa kwa mujibu wa sheria
 
Mkuu una mshahara mzuri pengine na hujawahi pitia vijibiashara ambavyo vinafanyika Maeneo ya nje pale " Kijana unajikwamua na kupata 100k kama mtaji ukaamua zako kwenda kupoint mtumba kadhaa Sawa na pesa yako wakati ukiwa katika harakati zako za kusaka wateja na nguo zako mkononi wanatokea Askari Jiji na kukupora hizo nguo tena kwa ubabe mkubwa na kudai Faini kubwa ambayo hauna mfukoni mwako wakati huo" Vuta picha ya hali gani ya machungu anayapata huyu kijana juu ya serikali na chochote kipitacho mbele yake wakati huu ikiwa wakati huo hajaiba wala kumpora mtu Wacha kusapoti upuuzi kwa kuwa uko na maisha mazuri hivi Sasa. Nikukumbushe kuna wakati halmashauri ya Soko ilikua inapitisha ushuru kwa kila Machinga pale na vijana tulikua tunalipa vyema Pasi na shaka

Uasi wa chuki na serikali kuu huwa unaanza taratibu na ipo siku nguvu ya vijana wasio na ajira itaonekana Endeleeni kula Mishahara minono katika ajira zenu
Hamna haki bila wajibu.
Unawajibika kutii sheria, Fanya biashara Yako eneo sahihi , wakikufuata huko Hapo utakuwa na haki ya kulalamika
 
Mkuu una mshahara mzuri pengine na hujawahi pitia vijibiashara ambavyo vinafanyika Maeneo ya nje pale " Kijana unajikwamua na kupata 100k kama mtaji ukaamua zako kwenda kupoint mtumba kadhaa Sawa na pesa yako wakati ukiwa katika harakati zako za kusaka wateja na nguo zako mkononi wanatokea Askari Jiji na kukupora hizo nguo tena kwa ubabe mkubwa na kudai Faini kubwa ambayo hauna mfukoni mwako wakati huo" Vuta picha ya hali gani ya machungu anayapata huyu kijana juu ya serikali na chochote kipitacho mbele yake wakati huu ikiwa wakati huo hajaiba wala kumpora mtu Wacha kusapoti upuuzi kwa kuwa uko na maisha mazuri hivi Sasa. Nikukumbushe kuna wakati halmashauri ya Soko ilikua inapitisha ushuru kwa kila Machinga pale na vijana tulikua tunalipa vyema Pasi na shaka

Uasi wa chuki na serikali kuu huwa unaanza taratibu na ipo siku nguvu ya vijana wasio na ajira itaonekana Endeleeni kula Mishahara minono katika ajira zenu
Pole sana mkuu,mimi sijaajiriwa kama usemavyo wewe,usiishi kwa hisia,pia wacha makasiriko,hakuna maisha ya lelemama kijana hasa wa kiume unapaswa kupambania maisha yako kwa hali yoyote ila zingatia kufuata sheria hutojutia...nikuulize tu labda mbona wale wanaouzia biashara zao ndani ya soko hawaporwi bidhaa zao wala kubuguziwa,unafikiri itakuaje kila mtu akipanga biashara barabarani na kuacha masoko yaliotengwa rasmi? vuta picha tutakua na miji ya namna gani tusipodhibiti hali hiyo
 
Tii sheria. Ushasema kwenye kingo za barabara hivyo hapo lazima wakupore.
 
Back
Top Bottom