Nimepima nina tatizo la nguvu za kiume

Nimepima nina tatizo la nguvu za kiume

Lemidmckon

Member
Joined
May 14, 2019
Posts
19
Reaction score
21
Habarini za muda huu ndugu zangu Wana jf,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27, nina tatizo la nguvu za kiume kwa muda mrefu sasa (takriban 9-10 years) yaani uume umelegea sana sana na hauwezi kusimama kiasi kwamba siwezi kufanya chochote hata hisia za mapenzi/msisimuko haupo kabisa kipindi cha nyuma nimetumia sana dawa mbalimbali tena kwa gharama kubwa mno bila mafanikio.

Hivi karibuni nimeenda kupima hospital nikaambiwa nina matatizo ya mfumo wa mzunguko wa damu na matatizo kwenye moyo kuna shida kwenye zoezi zima la kusukuma damu, parasympathetic nervous system, pelvic muscle problem (associated with pelvis pains), na kuhusu mambo mengine niko sawa.

Mfano Kisukari, pressure (normal), Ini, Figo, Hormones, Prostate gland, uzito (61kg,175cm uref), cholesterol sina, na mambo mengne kama sigara, viagra, drugs, masturbation, pombe n.k wala sihusiki navyo kabisa.

Naombeni ushauri na tiba ndugu zangu!

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri usilichukulie hili tatizo kama kikwazo kwenye maisha yako, lichukulie kama changamoto ya kawaida tu then nguvu kubwa ielekeze kwenye mambo productive.

Kama huwezi kumimbisha basi tafuta mwanamke mwenye sifa kama zako, then tafuteni mtoto/ watoto muwaasili kisha maisha yaendelee.

Usitumie nguvu kubwa sana kwenye kutafuta tiba ya hili tatizo maana kama umezaliwa nayo huwa ni nadra sana kupona, sanasana matapeli wakigundua una tatizo watakulia pesa zako weee lkn mwisho wa siku tatizo litabaki palepale.

BTW pole sana mkuu, hiyo ni sehemu ya maisha yetu sisi wanadamu.

Unforgetable
 
1. Mazoezi ya maana. Yatakayokutoa jasho haswaaa.
2. Kunywa maji ya kutosha. Ulazimishe mwili uzoee kupata maji mengi. Usisubirie hadi upate kiu.
3. Kula vyakula vya asili kwa sana. Achana na vinywaji vya viwandani.
4. Mboga mboga( mboga za majani)
Kula za kutosha, siyo kijiko kimoja.
5. Matunda kwa sana brother.
Achana na biscuits na mikate.

Ukibadili life style tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kama haisimami haisimami tu hata ule mihogo ".Alisikika mzee mmoja
Pole sana ndugu.
Hilo ni tatizo la kibaiolojia, linatibika ila kwa gharama za mamilioni
 
Kama hili tatizo umezaliwa nalo niliona kwenye group Moja iviii wakisema kwamba mama yako anaweza akalitibu Sasa cjui anaweza kutibu ukiwa mtoto tuu ukiwa mtu mzima ndo basiii ata nshasahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom