Nimepigana na rafiki yangu kisa msg, watu wamejaa

Makimuda255

Senior Member
Jul 31, 2020
165
286
Bandugu wa JamiiForums

Nimeleta hili jambo limenitokea usiku huu hapa alichokifanya huyu rafiki yangu

Mimi ni rafiki toka zamani tulipokutana chuo mwaka wa kwanza hadi sasa tupo mwaka wa pili chuo flan hivi hapa Arusha

Mara ya kwanza alikua anakaa na mwenzake ambaye wameanzia toka huko diploma lakini wakashindwana

Hiyo siku akanitumia msg kwamba anaomba siku anarudi huku arusha maana vyuo vinafunguliwa aje ashukie kwangu maana hana pa kushukia hivyo atakaa kama week tu akitafuta chumba.

Nikamkubalia bila tatizo akawa anakaa kwangu, bila shida nikawa namsitiri kwa kila hali simuulizi hela yoyote ya kula au gharama ya kununua chochote.

Siku zikaenda akawa hana dalili ya kuhama
Nikamueleza hali halisi kwamba ajitahidi atafute room maana muda umeenda sana na boom ashapata bas akaendelea kukaa na hatimaye akapata kwake japo alikua hataki kuondoka.

Akawa hakai sana huko kwake muda mwingi anakuja kwangu anakaa unakuta kakwama tunasaidiana hapa na pale

Sasa mimi nilichukia jambo moja....ana kasumba ya kupenda kupinga kila kitu atabisha kila kitu...hicho ndo tulikua tunapishana nacho kila siku na hata yule mshikaji alokaa nae mwanzo wakashindwana.

Akapata matatizo mama yake akaugua hakua na hela akaniomba nimkopeshe 90k nikampa mimi nina kanuni moja nikikusaidia sitaki utangaze au sinaga tabia ya kutangaza mambo yangu na yeye

Sikuwai mwambia mtu chochote hata tukipishana kauli,na pia alikaa kwangu bila mtu yoyote chuo kujua... maana sinaga tabia za kutangaza mambo

Sasa akawa ana tabia za ajabu ..mara utakua na jambo la kuumwa haji kukuona, ukiwa matatzoni hakusaidiii....ni mtu mbinafsi tu...

Mimi nilimchukulia km ndugu kbs.. lakini akawa habadiliki atafanya makosa ataomba msamaha na samahani nyngi itapita kesho atarudia

Halaf jamaa ukikosea ni mtu wa kukukosoa tu, na kukusema tu na kukukejeli...nikagundua huyu sio rafiki mwema....

Nikaamua kumchana live kupitia watsaap nikamueleza ukweli mwanzo mwisho kwamba anayofanya sio fair na abadilike...

Mchizi akaona msg akaomba msamaha na kwamba nisvunje ushikaji na kwamba amebadilika

Zimepita km week hiv leo tupo wote hapa maana nilikua naumwa tu nipo mnyonge natetemeka homa toka asbh naumwa ghafla akaanza tena issue ni msosi nikamuambia leo tunakula nn akasema hajui kwa kua sikua na hela akasema anaenda kula mgahawani kisa napika dagaa

Nikamwambia sawa ila sio poa kudharau chakula hapo akaanza kukumbushia ishu za zile msg akawa ananiuliza km niliizifuta yaani msg nilizomtumia kumchana ukweli ile siku.

Nikwamwambia mm hizo msg hazina shida kwanini anamind wakat alishasoma kwanini anaforce nifute?Duuh nikiwa nimelala naumwa ghafla mtu akanirukia akanikaba koo kwamba nifute hizo msg akanibana pumzi sasa kwa kua nilikua naumwa nilimsukuma nikanyanyuka tukaanza kupigana anangangania simu yangu

Tulipokua tunashikana tupigane akawahi kisu sasa hapo nikaona ashashika kisu nikaita msaada kwa majirani wakaja wapangaji wenzangu.

Akataka kukimbia wakamuwah ndo nikawaeleza uhalisia akabaki akiduwaa na kutetemeka nilikua na hasira kinyama na nipo naumwa hata kula siwez nina week nimekua hadi weak.

Nimemuacha aende lakini sijui km nitakuja msamehe huyu mtu nilimshamsaidia sana matokeo yake ni haya.

Urafiki huu duuuh nambie ingekua ni ww ungefanyaje kwa huyu mtu?maana nina hasira sana nataman nikipone nikamlipizie kisasi wakuu nishaurini nimfanye nn huyu rafiki.
 
Utotohood....ukija kuwa mkubwa kama kidume afu unamiliki geto la kupangia hakuna atakae kusumbua zaidi baba/mama mwenye nyumba tu
 
Bodi ya Mikopo inawaangalia tu mnavyo kula hilo Boom lake! na baada ya kushiba, mnaishia kupigana! Mkimaliza chuo, makato ya 15% na rentation fees ya 6% kwa mwaka vinawasubiri.
 
Aisee..hukuwa na haja ya kugombana nae,huyo ulitakiwa umuombe ishu,angehama akiogopa unaweza mvizia usiku.
 
Back
Top Bottom