Nimepanga mwanangu asome mwisho Kidato cha 4, asiendelee cha 5 na 6

Habarini wazazi na wakereketwa wa mfumo wa elimu ya hapa nchini.

Nimetafakari sana nimegundua elimu ya Tanzania ina format ya zamani so kudeal na ulimwengu wa leo ni vigumu mno na ndiyo maana tuna wahitimu ngazi ya degree ila kichwani wana general knowledge kiasi kwamba hata ukimpa milion 50 mhitimu wa chuo aliekuwa analalamika swala la mtaji baada ya miezi mitatu unamkuta ana ngeu usoni ambazo zimezaliwa na umiliki wa hiyo milion 50.

Juzi nimeshangazwa pale Kariakoo nimekutana na vijana wawili wenye asili ya Uarabu wa Kipemba ambao nilisoma nao primary miaka takribani 23 iliyopita ambapo mimi nilifaulu na wao walifail hivyo mimi niliendelea na masomo ya O Level na kupasua anga mpaka kufikia chuo kikuu. Tulifurahi sana kuonana na tukaanza kupiga mastori mixer kuuliza washikaji fulani tuliosoma nao siku hizi wapo wapi.

Sasa kwenye story zetu wale mabrothers hawajagusia kuwa waliendelea na shule ila nachokumbuka kwao dingi na maza wao walikuwa ni wauza duka coz kwao palikuwa karibu na Shule tulikuwa tunapaita kwa mpemba. Kumbe wale jamaa walivyofail wakapachikwa pale dukani na kila mmoja alipewa ki-segment chake cha kusimamia mauzo na faida mpaka kufikia hatua lile duka likazaa maduka mawili ya jumla(mahitaji ya nyumbani) So kwangu mimi ile ilikuwa ndo O Level yao.

Nifupishe kusema ni hivi wale jamaa kwa sasa wamenunua uapnde wa juu wa ghorofa pale KKOO na ndo makazi yao pia wana maduka ya injini na spare part used mpya pale pembeni mwa ghorofa la Machinga Complex kiukweli wapo vizuri wanajua kila kifaa na changamoto zake na wanatoa hadi ushauri wa magari na wala hawajasomea Ugerejia (nilienda kununua kifaa fulani cha gari langu) .Kichwani mwangu nikaandika kuwa hiyo specialisation yao ndo advance school yao.

Kwenye hapo nilibainisha tofauti zifuatazo:

1. Walianza kuyaishi maisha halisia na kujitegemea mapema ambapo mimi nilikuwa bado nipo shule coz wana watoto wakubwa kuliko mimi.

2. Wana experience ya mtaa na maisha kuliko mimi ambae nilikuwa john kisomo; I mean wakati mimi naisoma dunia ya dhahania wao wanaiishi dunia halisia.

3. Vifaa huwa wanafuata na kuagiza makontena kutoka Dubai hivyo hata kingereza tunafanana nao hata kama wanaongea kingereza kisicho syntax wala phonology

4. Wanakopesheka na bank hela kubwa kuliko mimi ninaekopea mshahara yaani kimionekano tu mimi naonekana dalali wao ndo waajiriwa.

5. Mimi pamoja kupoteza muda mwingi shuleni nalipwa laki 7 yenye makato lukuki ila wao wanaweza piga faida mara kumi ya mshahara wangu kwa mwezi.Hii imenifanya nishike pen na karatasi ku estimate gharama alizopoteza mzazi wangu kunipeleka hizi shule ushuzi za kibongo bongo. Ambapo zimenipa taaluma tofauti na ninayofanyia kazi. Mbaya zaidi gharama zinaonesha ni nyingi kuliko nachoapata.

(BILA WIZI SERIKALINI HUTOBOI HATA JPM AJUE HILI)

6. Nina mengi sana ya kuitukana elimu yetu ki ukweli ni hasara kubwa mno wanayoingia wazazi wetu na mimi game limechange naitwa mzazi na nisipoangalia naingia kwenye gurudumu la kusomesha mtoto kwa hasara kama walizoingia wazazi wangu.

HIVYO BASI MIMI KAMA MZAZI NIMEAMUA YAFUTAYO:

1. Nimegundua kwanza elimu yetu haipo kumpa mwanafunzi silaha za kupambana na uhalisia wa maisha ya kileo tena yaliyojaa teknolojia badala yake humpangusa utahira/uprimitive wa kuzaliwa na kumfanya ajitambue kuwa yupo mjini na aweze kubeti, kuwa dalali na kuchapa mdomo awe mwanasiasa ama kuajiriwa nje ya hapo anakuwa hana tofauti maiti iliyowekwa betri ikapata uzima na kutembea barabarani.

Hivyo navyoongea sasa nimemuhamisha mwanangu kutoka shule zinazoitwa English medium na kumpeleka shule za serikali zenye mtaala huo ili akaone kuna namna fulani ya ugumu wa maisha na hatimae ile hela niliyokuwa nawapelekea English medium nimeenda kununua mashamba ya miti ya mbao (ndo fixed acc yao). Pia kwa kuwahamisha nimejikuta napata nguvu ya kujenga nyumba za kupangisha na lodge kama kitegauchumi cha familia. Nimejikuta nawaza hata kununua shamba la miparachichi na nimeshanunua na heka 40 za shamba la mikorosho Mtwara japokuwa siasa za huyu bwana zimeenda kutibua hii biashara.

Vyote hivyo sio kama najitapa humu JF bali nataka niwaamshe wazazi wanaopambana kumlipia mil 4.6 mtoto kwa mwaka ili akamalize shule then akae nyumbani kwa ukosefu wa ajira apate frustration na msongo wa mawazo na azekee home na frustration ikizidi inaweza mpeleka kijana kwenye matumizi ya dawa za kulevya akihisi ni tumaini pekee lililobaki kwake.

2. Watoto wangu watasoma government na sitaki wasome secondary above form four na hivyo nimepanga niwawekee akiba yao kwa mtindo wa mashamba ya miti, lodge, nyumba za kupangisha ili wakifika form four wakasomee taaluma za upekee sio hizi yebo yebo mfano wa taaluma yebo yebo ni hizi kama Accountant, Procurement, Logistic, PPM, BAF n.k. Nipo radhi mwanangu nimpeleke aanze ku-specialize kwenye vifaa tiba, urubani, mionzi, mutengeneza hata majukwaa ya kina diamond kuanzia form four ili aspecialize jambo lake alilosomea ili awe master hata kama nikimtafutia mtaji wa mil 50 ataupeleka kwenye fani na ujuzi wake hata kama nitauza nyumba.

N:B Haya ni mawazo yangu tu. Kama tunafanana mawazo gonga hata like au comment chochote kuboresha mawazo haya kwa sababu navyoona serikali ya JMT haina mpango kuboresha na kubadilisha huu mfumo mfu wa elimu ya Tanzania tunashindwa hata na wakenya kidogo wameanza kurespond na elimu ya mkoloni aliyotuachia.
Safi sana sana sana sana. Hata akienda veta Kama huna mtaji wa kumrithisha poa tu. Umakenika. Ufundi wa majengo nk nk utampa maisha zaidi kuliko a’level na upuuzi gani sijuwi.
Apprenticeship inalipa ila bongo ndio bomu kishenzi..
 
Hebu tuache Kila Jamii inautashi wake wa kukabiliana na mazingira, Waafrika starehe na mapenzi ipo kwenye DNA yetu
Hakuna cha DNA wala nn bali ni kujiendekeza tu. Mbna kuna mabillionea kibao wa kiafrika ina maana wao hawana DNA?
 
Mtoto wangu akimaliza darasa la saba namtupa kwenye migodi yangu namfunza vifaa na utaalamu wa uchimbaji madini tunachimba hivi unafanya hivi soko twende China, uingereza,nk unapata hivi pesa unawekeza hapa,Nchi imejaa madini KILA namna wilaya zote.

Na sio kumpeleka kwenye mfumo wa elimu takataka usiomsaidia zaidi ya kumfanya awe masikini.
Exposure atapata nikisafiri nae nchi mbalimbali duniani .

Hivi serikali inajisikia unawasomesha watu hadi masters hadi chuo kikuu kisha anakuja kuwa machinga au bodaboda.
Kwann usiwekeze zaidi kwenye vyuo vya ujuzi zaidi kama walivyofanya wakoloni.
Kuwa na vyuo vikuu vingi katika nchi ni kuongeza idadi ya masikini nchini.
Hawawez kuskiliza huu ushauri kwa sabab watoto wao huwa wana ajira kabla hata hawajahitim masomo.
 
Mtoto wangu akimaliza darasa la saba namtupa kwenye migodi yangu namfunza vifaa na utaalamu wa uchimbaji madini tunachimba hivi unafanya hivi soko twende China, uingereza,nk unapata hivi pesa unawekeza hapa,Nchi imejaa madini KILA namna wilaya zote.

Na sio kumpeleka kwenye mfumo wa elimu takataka usiomsaidia zaidi ya kumfanya awe masikini.
Exposure atapata nikisafiri nae nchi mbalimbali duniani .

Hivi serikali inajisikia unawasomesha watu hadi masters hadi chuo kikuu kisha anakuja kuwa machinga au bodaboda.
Kwann usiwekeze zaidi kwenye vyuo vya ujuzi zaidi kama walivyofanya wakoloni.
Kuwa na vyuo vikuu vingi katika nchi ni kuongeza idadi ya masikini nchini.
Jtahd mwanao afike fom 4 ili akili yake ifunguke/exposure
 
Kukaa darasani kunakuoa Exposure ya kujifunza...90% ya wenye mindset ya kujifunza Mambo mapya ni wasomi si kwasababu walisomeshwa huko darsani bali kukaa huko unapipaita darasani ndipo kumewapa hiyo Culture.

'99% of Start-up Founders wana at least bachelor degree'

'99% of applicants was fund mbalimbali i.e TEF wanna bachelor degree'

It is culture
Hahahaaa kuna mengi sana huyajui kuhusu hii elimu mzee.
 
Asee ili uuelewe huu uzi ni lazima pia uwe umesoma kama hujasoma huwez kuelewa jamaa anamaanisha nn ila mm nmeuelewa sana hao wanaouliza kama watoto wakiishia 4m4 hao ma md na ma engineer watatoka wapi huyu sizani kama kasoma na kama amesoma itakua enzi za nyerere, alokwambia mtu ambae hajasoma form 5 na 6 hawez kuwa md ni nani? Huo uwezekano upo tena anakua very competent, binafsi mpaka leo hii cjawahi kujua elimu ya advance ina umuhimu gani japo upo lkn niangalia na negativity naona upande wa negativity ni mkubwa kuliko positivity na ni sehemu ambayo imeuwa ndoto za watu wengi, tusiishi kwa kukalili zama zinabadirika mtoto aliemaliza 4m4 yake akaenda moja kwa moja chuoni akasoma koz yake ya diploma ya pharmacy huwez kumuweka pamoja na mtoto alomaliza akasoma advance alaf akaangukia kweny degree ya sheria asee labda atamzid kweny uref wa cv pekeake.
 
Hata CV hawezi kumzidi. Cheti cha diploma ni muhimu kuliko cha advance
 
Wewe msomi nipe faida mojawapo wanayoifurahia hawa watu watatu hapa na vyeti vyao walivyovipambania miaka na miaka,binafsi alochoongea jamaa kina ukweli na lilikuwa wazo langu kichwani ila nilikuwa pia najaribu kutafufa wenye mawazo kama yangu kumbe tupo wengi.
Ubarikiwe sana boss sio lazima TUWAZE WOTE KWA PAMOJA TENA MAWAZO YA MAZOEA YA KILA SIKU
 
Uzi umefika mbali sana labda niulize kama watu hawatasoma mpaka bachelor je nani wataanzisha miradi mikubwa kama ya nuclear energy, space technology, aviation nk ambazo zinataka watu walio iva hasa kwenye sayansi.
Watu hapa wanaangalia zaidi elimu na kazi, wanaamini mtu akishindwa kupata kazi basi hio elimu haina maana.
Chanzo cha yote haya ni kitu kinaitwa
1 .Umahiri
2. utambuzi
Ndugu zangu umahiri ndio kila kitu na utambuzi ndio msingi wa umahiri.
Tujifunze kwa wenzetu jinsi walivyoweza kujenga hizo stadi mbili.
Tatizo sio kidato chs sita wala chuo kikuu na hata Veta sio suluhusho.
Kama veta anafundishwa na mhitimu wa chuo kikuuu unachokipinga je mhitimu wa atakuwa na tofauti gani na mwalimu wake!( like father like son).
Sikatai yapo masomo tunatakiwa tuyatilie mkazo kido sana mfano historia, jografia ya ullaya, stadi za kazi zisizoeleweka nk.
Kitu kikubwa zitambueni njia za kujenga unahiri kwa watoto wakiwa bado wadogo, jambo lingine waongozeni watoto wawe focused ili waweze kuwa mahiri kwa nambo machache mfano mchepuo wa sayansi na lugha, biashara na lugha, technolojia na lugha, maarifa ya nyumbani na lugha, kilimo na lugha nk.
Tabia ya nyinyi wazazi kuwaachia walimu wawafundishe watoto wenu masomo yote ndio inayopelekea watoto wenu kutokua mahiri.
Unafurahi mtoto wako kuwa wa kwanza badala ya kufurahi mtoto wako kuonesha muelekeo wa mchepuo fulani.
Tusisubiri watoto wamalize 4m4 bali tuanze nao wakiwa bado wadogo na jitahidi kutambua walimu wachache wenye kujielewa ushirikiane nao kuwasimamia watoto kujenga mwelekeo wa mwanao.
Bahati mbaya sana shule nyingi zimejiundia kamfumo ka kuwaweka watoto shuleni asubuhi mpaka jioni kila siku, hivyo shule zimekuwa jela za hiari na mzazi ni ngumu kutafuta mbadala kwa mtoto wake mpaka j/mosi na j/pili.
 
Asee ili uuelewe huu uzi ni lazima pia uwe umesoma kama hujasoma huwez kuelewa jamaa anamaanisha nn ila mm nmeuelewa sana hao wanaouliza kama watoto wakiishia 4m4 hao ma md na ma engineer watatoka wapi huyu sizani kama kasoma na kama amesoma itakua enzi za nyerere, alokwambia mtu ambae hajasoma form 5 na 6 hawez kuwa md ni nani? Huo uwezekano upo tena anakua very competent, binafsi mpaka leo hii cjawahi kujua elimu ya advance ina umuhimu gani japo upo lkn niangalia na negativity naona upande wa negativity ni mkubwa kuliko positivity na ni sehemu ambayo imeuwa ndoto za watu wengi, tusiishi kwa kukalili zama zinabadirika mtoto aliemaliza 4m4 yake akaenda moja kwa moja chuoni akasoma koz yake ya diploma ya pharmacy huwez kumuweka pamoja na mtoto alomaliza akasoma advance alaf akaangukia kweny degree ya sheria asee labda atamzid kweny uref wa cv pekeake.
Asante kwa uelewa wako mzuri mimi nipo na wewe kuwa kama kusomea aanze mapema kuspecialize ili awe mbobezi kwenye fani husika kuliko kupelekana form five na six akasomee general KNOWLEDGE
 
Uzi umefika mbali sana labda niulize kama watu hawatasoma mpaka bachelor je nani wataanzisha miradi mikubwa kama ya nuclear energy, space technology, aviation nk ambazo zinataka watu walio iva hasa kwenye sayansi.
Watu hapa wanaangalia zaidi elimu na kazi, wanaamini mtu akishindwa kupata kazi basi hio elimu haina maana.
Chanzo cha yote haya ni kitu kinaitwa
1 .Umahiri
2. utambuzi
Ndugu zangu umahiri ndio kila kitu na utambuzi ndio msingi wa umahiri.
Tujifunze kwa wenzetu jinsi walivyoweza kujenga hizo stadi mbili.
Tatizo sio kidato chs sita wala chuo kikuu na hata Veta sio suluhusho.
Kama veta anafundishwa na mhitimu wa chuo kikuuu unachokipinga je mhitimu wa atakuwa na tofauti gani na mwalimu wake!( like father like son).
Sikatai yapo masomo tunatakiwa tuyatilie mkazo kido sana mfano historia, jografia ya ullaya, stadi za kazi zisizoeleweka nk.
Kitu kikubwa zitambueni njia za kujenga unahiri kwa watoto wakiwa bado wadogo, jambo lingine waongozeni watoto wawe focused ili waweze kuwa mahiri kwa nambo machache mfano mchepuo wa sayansi na lugha, biashara na lugha, technolojia na lugha, maarifa ya nyumbani na lugha, kilimo na lugha nk.
Tabia ya nyinyi wazazi kuwaachia walimu wawafundishe watoto wenu masomo yote ndio inayopelekea watoto wenu kutokua mahiri.
Unafurahi mtoto wako kuwa wa kwanza badala ya kufurahi mtoto wako kuonesha muelekeo wa mchepuo fulani.
Tusisubiri watoto wamalize 4m4 bali tuanze nao wakiwa bado wadogo na jitahidi kutambua walimu wachache wenye kujielewa ushirikiane nao kuwasimamia watoto kujenga mwelekeo wa mwanao.
Bahati mbaya sana shule nyingi zimejiundia kamfumo ka kuwaweka watoto shuleni asubuhi mpaka jioni kila siku, hivyo shule zimekuwa jela za hiari na mzazi ni ngumu kutafuta mbadala kwa mtoto wake mpaka j/mosi na j/pili.
Ukiusoma vizuri huu uzi haumanishi watu kutofika chuo kikuu nachomanisha tunaliana muda darasani kwa kulishwa general KNOWLEDGE ambayo inakosesha wahitimu wetu kitu ulichoita UMAHIRI we unafikili ili uwe injinia,IT ni lazima usome six hadi chuo jibu ni hapana.Muone BILL GATE aliachana na shule akaamua kuanza kuwa mahiri wa kugonga codes na hatimae akawa software developer na leo hii kaja na kampuni lake la MICROSOFT uzi wangu umelenga kuilalamikia elimu yetu kuwa haimtengenezi mhitimu kuwa competence kwenye hii dunia ya utafutaji na hivyo mawazo yake yanakuwa tegemezi wa KUAJIRIWA ILI AIBE NDO AJENGE.
 
Moja ya malengo ya elimu ni kuelimika ili kuisaidia jamii iliyokuzunguka kutatua matatizo yao,
Kama lengo la elimu litachukuliwa ni kupata tu mshahara mkubwa basi huwezi kuona umuhimu wa elimu,mtu aliyesoma hawezi kufanana na asiyesoma hata kama asiyesoma atakua tajiri kumshinda aliyesoama,asiye soma lazima amtegemee aliyesoma,kwenye biashara yake atatumia teknolojia ya mawasiliana,vifaa vya ofisini,transportation...na hayo yote ni matokeo ya elimu.
So kaka we una hoja ipi hapo ukilinganisha na uzi unavyosema
 
Suala si graphics design,IT,Engineering nk. Suala ni competence, awareness,mindset nk
Ndio hayo tuanayojadili kuwa kusoma kwa kufuata tu madarasa badala kusoma ili uelime na ujitambue.kuna watu hawajapitia hio It they make money,wewe na digrii,diploma,certificate unakwama wapi?
Sayansi haijawahi kukosa ajira duniani kote.Mambo ya kusomea vitu vya ubunifu ukibwani ni shida bado kuna watu wanabisha.Mtu umalize form six ndo ukajifunze programming miaka 3 hapo lazima uwe mweupe. Do it early! do it early! ndio mfumo was sayansi, vinginevyo tutalaumu sana.
Etheiopia wameanzisha after school curriculum, hivyo vijana mda wa jioni wanajifunza how to program a robots je hao watoto utakuja kulinganisha na wakwetu mtu anamaliza chuo ROBOT anamsikia kwenye vitabu tu.Tusipoangalia hadi vinchi kama Rwanda vitatipita.
Rwanda mpaka sasa sio wenzetu fuatilia matusi wanayofanya kwenye ulimwengu wa Technology
 
Tunafeli kwa mengi, Wahindi na Waarabu watoto wao tunasoma nao St Kayumba lakini wakirudi nyumbani, baba haendi bar kula nyama choma jioni anakaa sebuleni na wanae. Akija Uncle Hamood kusalimia kahawa na chai vinawekwa kwenye vikombe na wanakunywa wote.

Baba na Uncle Hamood hawaongelei mchepuko wenye chura zaidi, wanaongelea risk factors za biashara.
Halafu wakifanikiwa mnawaita wanyonyaji huku nyie mitaji yenu imeishia kwenye pombe ya kipumu,dengelua na kuwacheza unyango wasichana wadogo.
 
Kila mtu akiwaza kama wewe, ni nani atakuwa engineer wa kutengeneza barabara? Ni nani atakuwa Medical Doctor wa kutibu wengine.

Kwa kuwa hao ni watoto wako na sisi hatuwezi kukupangia maisha, hata ukitaka waishie darasa la sita ni wewe tu na maisha yako.
Kwa maengineer ni wale wanotengeneza barabara tu?
 
Habarini wazazi na wakereketwa wa mfumo wa elimu ya hapa nchini.

Nimetafakari sana nimegundua elimu ya Tanzania ina format ya zamani so kudeal na ulimwengu wa leo ni vigumu mno na ndiyo maana tuna wahitimu ngazi ya degree ila kichwani wana general knowledge kiasi kwamba hata ukimpa milion 50 mhitimu wa chuo aliekuwa analalamika swala la mtaji baada ya miezi mitatu unamkuta ana ngeu usoni ambazo zimezaliwa na umiliki wa hiyo milion 50.

Juzi nimeshangazwa pale Kariakoo nimekutana na vijana wawili wenye asili ya Uarabu wa Kipemba ambao nilisoma nao primary miaka takribani 23 iliyopita ambapo mimi nilifaulu na wao walifail hivyo mimi niliendelea na masomo ya O Level na kupasua anga mpaka kufikia chuo kikuu. Tulifurahi sana kuonana na tukaanza kupiga mastori mixer kuuliza washikaji fulani tuliosoma nao siku hizi wapo wapi.

Sasa kwenye story zetu wale mabrothers hawajagusia kuwa waliendelea na shule ila nachokumbuka kwao dingi na maza wao walikuwa ni wauza duka coz kwao palikuwa karibu na Shule tulikuwa tunapaita kwa mpemba. Kumbe wale jamaa walivyofail wakapachikwa pale dukani na kila mmoja alipewa ki-segment chake cha kusimamia mauzo na faida mpaka kufikia hatua lile duka likazaa maduka mawili ya jumla(mahitaji ya nyumbani) So kwangu mimi ile ilikuwa ndo O Level yao.

Nifupishe kusema ni hivi wale jamaa kwa sasa wamenunua uapnde wa juu wa ghorofa pale KKOO na ndo makazi yao pia wana maduka ya injini na spare part used mpya pale pembeni mwa ghorofa la Machinga Complex kiukweli wapo vizuri wanajua kila kifaa na changamoto zake na wanatoa hadi ushauri wa magari na wala hawajasomea Ugerejia (nilienda kununua kifaa fulani cha gari langu) .Kichwani mwangu nikaandika kuwa hiyo specialisation yao ndo advance school yao.

Kwenye hapo nilibainisha tofauti zifuatazo:

1. Walianza kuyaishi maisha halisia na kujitegemea mapema ambapo mimi nilikuwa bado nipo shule coz wana watoto wakubwa kuliko mimi.

2. Wana experience ya mtaa na maisha kuliko mimi ambae nilikuwa john kisomo; I mean wakati mimi naisoma dunia ya dhahania wao wanaiishi dunia halisia.

3. Vifaa huwa wanafuata na kuagiza makontena kutoka Dubai hivyo hata kingereza tunafanana nao hata kama wanaongea kingereza kisicho syntax wala phonology

4. Wanakopesheka na bank hela kubwa kuliko mimi ninaekopea mshahara yaani kimionekano tu mimi naonekana dalali wao ndo waajiriwa.

5. Mimi pamoja kupoteza muda mwingi shuleni nalipwa laki 7 yenye makato lukuki ila wao wanaweza piga faida mara kumi ya mshahara wangu kwa mwezi.Hii imenifanya nishike pen na karatasi ku estimate gharama alizopoteza mzazi wangu kunipeleka hizi shule ushuzi za kibongo bongo. Ambapo zimenipa taaluma tofauti na ninayofanyia kazi. Mbaya zaidi gharama zinaonesha ni nyingi kuliko nachoapata.

(BILA WIZI SERIKALINI HUTOBOI HATA JPM AJUE HILI)

6. Nina mengi sana ya kuitukana elimu yetu ki ukweli ni hasara kubwa mno wanayoingia wazazi wetu na mimi game limechange naitwa mzazi na nisipoangalia naingia kwenye gurudumu la kusomesha mtoto kwa hasara kama walizoingia wazazi wangu.

HIVYO BASI MIMI KAMA MZAZI NIMEAMUA YAFUTAYO:

1. Nimegundua kwanza elimu yetu haipo kumpa mwanafunzi silaha za kupambana na uhalisia wa maisha ya kileo tena yaliyojaa teknolojia badala yake humpangusa utahira/uprimitive wa kuzaliwa na kumfanya ajitambue kuwa yupo mjini na aweze kubeti, kuwa dalali na kuchapa mdomo awe mwanasiasa ama kuajiriwa nje ya hapo anakuwa hana tofauti maiti iliyowekwa betri ikapata uzima na kutembea barabarani.

Hivyo navyoongea sasa nimemuhamisha mwanangu kutoka shule zinazoitwa English medium na kumpeleka shule za serikali zenye mtaala huo ili akaone kuna namna fulani ya ugumu wa maisha na hatimae ile hela niliyokuwa nawapelekea English medium nimeenda kununua mashamba ya miti ya mbao (ndo fixed acc yao). Pia kwa kuwahamisha nimejikuta napata nguvu ya kujenga nyumba za kupangisha na lodge kama kitegauchumi cha familia. Nimejikuta nawaza hata kununua shamba la miparachichi na nimeshanunua na heka 40 za shamba la mikorosho Mtwara japokuwa siasa za huyu bwana zimeenda kutibua hii biashara.

Vyote hivyo sio kama najitapa humu JF bali nataka niwaamshe wazazi wanaopambana kumlipia mil 4.6 mtoto kwa mwaka ili akamalize shule then akae nyumbani kwa ukosefu wa ajira apate frustration na msongo wa mawazo na azekee home na frustration ikizidi inaweza mpeleka kijana kwenye matumizi ya dawa za kulevya akihisi ni tumaini pekee lililobaki kwake.

2. Watoto wangu watasoma government na sitaki wasome secondary above form four na hivyo nimepanga niwawekee akiba yao kwa mtindo wa mashamba ya miti, lodge, nyumba za kupangisha ili wakifika form four wakasomee taaluma za upekee sio hizi yebo yebo mfano wa taaluma yebo yebo ni hizi kama Accountant, Procurement, Logistic, PPM, BAF n.k. Nipo radhi mwanangu nimpeleke aanze ku-specialize kwenye vifaa tiba, urubani, mionzi, mutengeneza hata majukwaa ya kina diamond kuanzia form four ili aspecialize jambo lake alilosomea ili awe master hata kama nikimtafutia mtaji wa mil 50 ataupeleka kwenye fani na ujuzi wake hata kama nitauza nyumba.

N:B Haya ni mawazo yangu tu. Kama tunafanana mawazo gonga hata like au comment chochote kuboresha mawazo haya kwa sababu navyoona serikali ya JMT haina mpango kuboresha na kubadilisha huu mfumo mfu wa elimu ya Tanzania tunashindwa hata na wakenya kidogo wameanza kurespond na elimu ya mkoloni aliyotuachia.
1. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi! Ukiona mgonjwa fulani kapona kwa sababu katumia dawa A kama hujapimwa na kukutwa na aina ya ugonjwa kama wake usichukulie kuwa kutumia dawa A kama yeye hata wewe utapona. Kuna watu wengi wamedanganyika kwa hili, kwani hata kama dalili za ugonjwa zinafanana, inawezekana ugongwa ukawa tofauti au hata kama ikitokea ugonjwa ni uleule, dozi ya kila mmoja inaweza ikawa tofauti kwa sababu mbalimbali za kiafya zinazotokana na umri, aina ya ugonjwa, kuenea kwa ugonjwa mwilini nk.
2. Elimu ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania.
3. Utaratibu wa elimu Tanzania ni kusoma kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu: a) Elimu ya msingi (ambayo sasa hivi ni bure): darasa la kwanza hadi Kidato cha Nne b) Elimu ya Juu I (high school): Kidato cha 5-6, c) Elimu ya Juu II: Chuo Kikuu.
4. Mtoto aliyefaulu na mwenye uwezo wa kuendelea kusoma, yuko entitled kusoma hadi chuo kikuu/kumaliza masomo yake.
5. Mzazi kuamua mtoto wake mwenye uwezo wa kuendelea kusoma, asiendelee kusoma ni kumkosea haki. Ni sawa na yeye kama wazazi wake wangeamua akomee darasa la kwanza, la nne, la saba au kidato cha pili wakati kwa utaratibu wa masomo uliopo mtoto angeweza kusoma hadi mwisho (kuhitimu elimu ya chuo kikuu, nk).
6. Ingawa kufaulu katika maisha kunaweza kusitegemee aina ya elimu aliyonayo mtoto, kusoma na kufikia kiwango cha juu cha elimu si ushahidi wa mtoto kutofanikiwa katika maisha. Kutofanikiwa katika maisha kunachangiwa na sababu mbalimbali.
7. Kwa hiyo, kudhani kwamba elimu ni kikwazo cha kutofanikiwa katika maisha ni ignorance ya hali ya juu (ni kutojitambua kwa mzazi na kuamua mambo kwa kutegemea mafanikio ya watu wengine ambayo unakuta undani wae hatuujui). Huwezi kuamua jambo kubwa bila kujua undani wake - hizi ni fikira potofu!
8. Kuna mzazi namfahamu mtoto wake alifaulu vizuri sana Kidato cha 6 na mtoto alitaka asome kidato cha sita hadi chuo kikuu, lakini mzazi alitaka mtoto aende chuo kutoka kidato cha nne na ndivyo alivyofanya, lakini naamini mtoto atakuwa affected kisaikolojia siku za baadaye kwa sababu hapakuwa na sababu ya msingi ya kumzuia mtoto asiendelee kidato cha 5 na 6 na hata chuo kikuu.
9. Ni uonevu mkubwa kumnyima mtoto fursa ya kujiendeleza kimasoma kwa kudhani kuwa atachelewa kufanikiwa katika maisha kwa sababu kumkatisha mtoto masomo (short-cut) siyo ushahidi pia kuwa mtoto atafanikiwa katika maisha. Kufanikiwa nako kunatokana na sababu mbalimbali.
10. Mpe mtoto fursa ya kusoma kama mtoto mwenyewe ana uwezo wa kuendelea kusoma na kama mzazi ana uwezo wa kumwendeleza mtoto.
 
Back
Top Bottom