Nimepanga mwanangu asome mwisho Kidato cha 4, asiendelee cha 5 na 6

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,724
19,866
Habarini wazazi na wakereketwa wa mfumo wa elimu ya hapa nchini.

Nimetafakari sana nimegundua elimu ya Tanzania ina format ya zamani so kudeal na ulimwengu wa leo ni vigumu mno na ndiyo maana tuna wahitimu ngazi ya degree ila kichwani wana general knowledge kiasi kwamba hata ukimpa milion 50 mhitimu wa chuo aliekuwa analalamika swala la mtaji baada ya miezi mitatu unamkuta ana ngeu usoni ambazo zimezaliwa na umiliki wa hiyo milion 50.

Juzi nimeshangazwa pale Kariakoo nimekutana na vijana wawili wenye asili ya Uarabu wa Kipemba ambao nilisoma nao primary miaka takribani 23 iliyopita ambapo mimi nilifaulu na wao walifail hivyo mimi niliendelea na masomo ya O Level na kupasua anga mpaka kufikia chuo kikuu. Tulifurahi sana kuonana na tukaanza kupiga mastori mixer kuuliza washikaji fulani tuliosoma nao siku hizi wapo wapi.

Sasa kwenye story zetu wale mabrothers hawajagusia kuwa waliendelea na shule ila nachokumbuka kwao dingi na maza wao walikuwa ni wauza duka coz kwao palikuwa karibu na Shule tulikuwa tunapaita kwa mpemba. Kumbe wale jamaa walivyofail wakapachikwa pale dukani na kila mmoja alipewa ki-segment chake cha kusimamia mauzo na faida mpaka kufikia hatua lile duka likazaa maduka mawili ya jumla(mahitaji ya nyumbani) So kwangu mimi ile ilikuwa ndo O Level yao.

Nifupishe kusema ni hivi wale jamaa kwa sasa wamenunua uapnde wa juu wa ghorofa pale KKOO na ndo makazi yao pia wana maduka ya injini na spare part used mpya pale pembeni mwa ghorofa la Machinga Complex kiukweli wapo vizuri wanajua kila kifaa na changamoto zake na wanatoa hadi ushauri wa magari na wala hawajasomea Ugerejia (nilienda kununua kifaa fulani cha gari langu) .Kichwani mwangu nikaandika kuwa hiyo specialisation yao ndo advance school yao.

Kwenye hapo nilibainisha tofauti zifuatazo:

1. Walianza kuyaishi maisha halisia na kujitegemea mapema ambapo mimi nilikuwa bado nipo shule coz wana watoto wakubwa kuliko mimi.

2. Wana experience ya mtaa na maisha kuliko mimi ambae nilikuwa john kisomo; I mean wakati mimi naisoma dunia ya dhahania wao wanaiishi dunia halisia.

3. Vifaa huwa wanafuata na kuagiza makontena kutoka Dubai hivyo hata kingereza tunafanana nao hata kama wanaongea kingereza kisicho syntax wala phonology

4. Wanakopesheka na bank hela kubwa kuliko mimi ninaekopea mshahara yaani kimionekano tu mimi naonekana dalali wao ndo waajiriwa.

5. Mimi pamoja kupoteza muda mwingi shuleni nalipwa laki 7 yenye makato lukuki ila wao wanaweza piga faida mara kumi ya mshahara wangu kwa mwezi.Hii imenifanya nishike pen na karatasi ku estimate gharama alizopoteza mzazi wangu kunipeleka hizi shule ushuzi za kibongo bongo. Ambapo zimenipa taaluma tofauti na ninayofanyia kazi. Mbaya zaidi gharama zinaonesha ni nyingi kuliko nachoapata.

(BILA WIZI SERIKALINI HUTOBOI HATA JPM AJUE HILI)

6. Nina mengi sana ya kuitukana elimu yetu ki ukweli ni hasara kubwa mno wanayoingia wazazi wetu na mimi game limechange naitwa mzazi na nisipoangalia naingia kwenye gurudumu la kusomesha mtoto kwa hasara kama walizoingia wazazi wangu.

HIVYO BASI MIMI KAMA MZAZI NIMEAMUA YAFUTAYO:

1. Nimegundua kwanza elimu yetu haipo kumpa mwanafunzi silaha za kupambana na uhalisia wa maisha ya kileo tena yaliyojaa teknolojia badala yake humpangusa utahira/uprimitive wa kuzaliwa na kumfanya ajitambue kuwa yupo mjini na aweze kubeti, kuwa dalali na kuchapa mdomo awe mwanasiasa ama kuajiriwa nje ya hapo anakuwa hana tofauti maiti iliyowekwa betri ikapata uzima na kutembea barabarani.

Hivyo navyoongea sasa nimemuhamisha mwanangu kutoka shule zinazoitwa English medium na kumpeleka shule za serikali zenye mtaala huo ili akaone kuna namna fulani ya ugumu wa maisha na hatimae ile hela niliyokuwa nawapelekea English medium nimeenda kununua mashamba ya miti ya mbao (ndo fixed acc yao). Pia kwa kuwahamisha nimejikuta napata nguvu ya kujenga nyumba za kupangisha na lodge kama kitegauchumi cha familia. Nimejikuta nawaza hata kununua shamba la miparachichi na nimeshanunua na heka 40 za shamba la mikorosho Mtwara japokuwa siasa za huyu bwana zimeenda kutibua hii biashara.

Vyote hivyo sio kama najitapa humu JF bali nataka niwaamshe wazazi wanaopambana kumlipia mil 4.6 mtoto kwa mwaka ili akamalize shule then akae nyumbani kwa ukosefu wa ajira apate frustration na msongo wa mawazo na azekee home na frustration ikizidi inaweza mpeleka kijana kwenye matumizi ya dawa za kulevya akihisi ni tumaini pekee lililobaki kwake.

2. Watoto wangu watasoma government na sitaki wasome secondary above form four na hivyo nimepanga niwawekee akiba yao kwa mtindo wa mashamba ya miti, lodge, nyumba za kupangisha ili wakifika form four wakasomee taaluma za upekee sio hizi yebo yebo mfano wa taaluma yebo yebo ni hizi kama Accountant, Procurement, Logistic, PPM, BAF n.k. Nipo radhi mwanangu nimpeleke aanze ku-specialize kwenye vifaa tiba, urubani, mionzi, mutengeneza hata majukwaa ya kina diamond kuanzia form four ili aspecialize jambo lake alilosomea ili awe master hata kama nikimtafutia mtaji wa mil 50 ataupeleka kwenye fani na ujuzi wake hata kama nitauza nyumba.

N:B Haya ni mawazo yangu tu. Kama tunafanana mawazo gonga hata like au comment chochote kuboresha mawazo haya kwa sababu navyoona serikali ya JMT haina mpango kuboresha na kubadilisha huu mfumo mfu wa elimu ya Tanzania tunashindwa hata na wakenya kidogo wameanza kurespond na elimu ya mkoloni aliyotuachia.
 
Tunafeli kwa mengi, Wahindi na Waarabu watoto wao tunasoma nao St Kayumba lakini wakirudi nyumbani, baba haendi bar kula nyama choma jioni anakaa sebuleni na wanae. Akija Uncle Hamood kusalimia kahawa na chai vinawekwa kwenye vikombe na wanakunywa wote.

Baba na Uncle Hamood hawaongelei mchepuko wenye chura zaidi, wanaongelea risk factors za biashara.
 
Unazungumzia Apprenticeship. Hiyo ndio ilikuwa mfumo wa elimu duniani kwa milenia, kabla ya kuja mfumo wa sasa. Michael Faraday ni mfano mmoja wa mafanikio ya mfumo huo.

Pengine mkuu OP utanufaika ukisoma kitabu cha Robert Greene "Mastery".
 
Mshahara laki 7 ambao una makato kibao, lkn ulikuwa na uwezo wa kupeleka watoto wako international,pili kwa laki saba hiyo hiyo unataka kujenga lodge, kwa laki saba hiyo hiyo ya makato unamiliki gari na kwa laki saba hiyo hiyo ndio inaleta chakula mezani.

Hapa katikati kuna miujiza utakuwa unaifanya.

😀😀😀😀
 
Wewe ndye mbabaishaji. Waliotengeneza magar ya kwanza hata hawakwenda shule. Walioenda shule ndyo waliokuja kusoma mfumo wa magar unavyofanya kazi.
Hao vijana wa kiarabu walioishia kidato cha nne kama hawajasoma wamejuaji kila kifaa cha gari kinavyofanya kazi na changamoto zake?
 
Tunafeli kwa mengi, Wahindi na Waarabu watoto wao tunasoma nao St Kayumba lakini wakirudi nyumbani, baba haendi bar kula nyama choma jioni anakaa sebuleniena wanae. Akija uncle Hamood kusalimia kahawa na chai vinawekwa kwenye vikombe na wanakunywa wote. Baba na uncle Hamood hawaongelei mchepuko wenye chura zaidi wanaongelea risk factors za biashara.
Kabisa yaani sisi tunajiua wenyewe alafu wazuri kulalamika kama hao wapemba walikuwa wakirudi shule unawakuta dukani kwao na ukiwacheck wana nidhamu kichizi.
 
Back
Top Bottom