Nimeota ndoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeota ndoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mvaa Tai, Sep 23, 2010.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  NIMEOTA NDOTO WATANZANIA WOOTE KILA SIKU WANAFANYA MAMBO YAFUATAYO.

  1. WANALIPA KODI BILA KUKWEPA, WATUMISHI WA TRA WAMEACHA TABIA ZA KUSHIRIKIANA NA WALIPA KODI WASIO WAAMINIFU KATIKA KULIPA KODI. WATANZANIA WAMEFIKIA MAHALA UKIMUUZIA BIDHAA BILA KUMPATIA RISITI INAYOONYESHA MAKATO YA KODI, HURUDISHA BIDHAA ZAKO ZOTE.

  2.WATU WANAFANYA KAZI KWA BIDII IWE SHAMBANI AU OFISINI

  3.WATANZANIA WAMEACHA KUNUNUA BIDHAA KUTOKA NJE AMBAZO ZINATENGENEZWA HAPA NCHINI KAMA VILE FENICHA NA MAZIWA YA PAKITI. WANAJUA UMUHIMU WA KUNUNUA SABUNI YA UNGA YA FOMA GOLD YA TANZANIA(kwa mfano) BADALA YA OMO YA KUTOKA KENYA AU SOUTH AFRICA.

  4. MADUKA YOOTE YA SHOPRITE TANZANIA YAMEFUNGWA KWASABABU HAYAPATI WATEJA KWASABABU YANAUZA SEHEMU KUBWA YA BIDHAA ZAO KUTOKA NJE YA NCHI NA WATANZANIA KWA KULIJUA HILO KWAMBA NI SEHEMU YA SABABU YA WAO KUWA NCHI MASIKINI HAWAENDI TENA SHOPRITE, HATA KWENYE MADUKA YA KAWAIDA WATANZANIA WANAISOMA VIZURI BIDHAA KUJIRIDHISHA KWAMBA NI BIDHAA YA KITANZANIA.

  5. WATANZANIA WOTE WENYE SIFA ZA KUPIGA KURA WANAJITOKEZA WOOTE KUPIGA KURA ILI KUWAWAJIBISHA VIONGOZI MAFISADI NA WABINAFSI.

  GHAFLA NDOTO YANGU IKAKATISHWA NA MOJA YA WATEJA ALIYENIGONGEA MLANGO KWA NGUVU BAADA YA KUSIKIA NIKIKOROMA NA YEYE AKIWA AMESUBIRI SANA MLANGONI KUMBE NILIKUWA NIPO OFISINI NA NI MTUMISHI WA SERIKALI.

  KWA WATAALAM WA NDOTO NANI ANAWEZA KUNITAFSRIA HII NDOTO?
   
 2. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  hata mie nilishaota ndoto kama yako nikenda kwa sheikh yahya na tafsiri yake ilikuwa hivi "ndoto hiyo huletwa na jini "mabadiliko ya uongozi" na jini huyu huenda ulimpata kwa kuudhuria midahalo na kampeni za vyama vya upinzani vyenye nia ya kuingoa ccm madarakani ili vilete mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kutetea rasilimali zetu wazawa....

  pia akasema jitahidi "kuvaa jiwe la ccm na ufisadi" ili kujikinga na jini huyu maana anaweza kukufanya ujikute ukimpigia kura dr. slaa wa chadema ifikapo 31 octoba 2010 na kama upo dsm maeneo ya ubungo unaweza kujikuta unamchagua john mnyika au mitaa ya kawe ukampa kura yako dada mdee...ila kama utakuwa segerea lazma jini huyu atakufanya umjague ndg mpendazoe ili tuu azma yake ya kuleta maendeleo itimie...

  toka siku hiyo niloota ndoto kama yako jini huyo kanizidi nguvu kiasi kwamba hata kabla ya trh 31 oct 2010 nimejikuta nikitaka kuwaambukiza kwa nguvu zooote watanzania ugonjwa niloupata wa"kuandika sms 1 kila siku na kuisambaza kwa watanzania woote juu ya "kumpokea jini "mabadiliko ya uongozi" na kila jini akinipanda napenda sana kuwapigia simu wazee wangu huko vijijini na kuwaambia kuwa jini wangu kanituma mie kiti wake niwaambie "pokeeni pesa na khanga na tshirt za ccm ila kura zenu mpeni mzee slaa na chadema ili "mupate elimu bure na afya bure na maisha yaongezeke ladha maana hakutakuwa na kodi za mifugo wala mazao yenu hamtopangiwa wapi pa kuuza...hongera kwa kuingiwa na jini "mabadiliko ya uongozi " tzania
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mungu wangu ndoo maana hata nikiwa napita barabarani nimeanza kuzichukia rangi za njano na kijani, sijui nitafanyaje maana nilikuwa mshabiki wa yanga na rangi zao nahisi kama zina hatia katika kuwafanya watanzania wawe maskini.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sisi tunaota ndotoni, wenzetu wa dunia ya kwanza na ya pili hayo ndiyo maisha ya kila siku!
  Anatakiwa aje raisi ambaye ni mchanganyiko wa udikteta, uwajibikaji na busara!
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ushindwe tena ulegee!!!!!!!!! Sisi tunapenda sana amani tuliyonayo hapa kwetu tanzania. Hivi unapenda yatukute ya rwanda na burundi? plz usivichague vyama vya upinzani vitaleta vita, hukumbuki kile kipindi mahita akiwa mkuu wa jeshi la polisi tanzania alikamata kontena bandarini likiwa limesheheni siraha za moto na visu vikiwa vina bendera za cuf? Serikali ya ccm ni makini sana iliamua kupuuza hilo jambo ndo maana huwezi kupata hatua zilizochukuliwa na mahakama kuhusiana na tukio hilo. Naipenda sana ccm
   
Loading...