Nimeota ndoto Wakili Mwabukusi amekuwa mpole sana

Michael Uledi

Senior Member
Mar 29, 2023
132
322
George Michael Uledi.
August 7,2023.

Boblia takatifu inasema "..Mungu huongea na watu katika ndoto na maono wakati wa usingizi mzito unapowavamia.."(Yob 33:15).Kama hivyo ndivyo,basi Mungu wangu jana aliongea na mimi kupitia ndoto au maono.

Askofu Gwajima katika somo lake la ndoto aliwahi kusema "ndoto ni taswira,picha au matukio ambayo unaumbwa katika ulimwengu wa roho na baafae kuja kujidhihirisha kwenye ulimwengu wa kawaida wa dunia.".Kwahiyo ndoto za Mungu ni ishara ya yale yajayo kesho katika maisha yako.Duu kweli Mungu fundi.

Jana usiku wa saa tisa nimeota nipo na wakili Boni Mwabukusi akiwa amekaa juu ya meza ya mbao na juu ya meza hiyo kulikuwa na vitu kama vitambulosho(Press Cards au au kitu kama Passport)hivi vyenye nembo ya Tanzania na sio Tanganyika Juu yake.Vitambulisho hivyo vilikuwa na rangi ya Njano.

Idadi ya vitambulisho hivyo vilikuwa saba lakini pia sio zaidi ya Nane.Vyote vilikuwa vinaratibiwa na Wakili Boni Mwabukusi huku akiwa anavigawa kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wanakwenda mmoja mmoja mezani kwake.

Zamu yangu ya kwenda kuchukua kitambulisho hicho ilipofika nilikaribia mbele ya meza ya Wakili Mwabukusi.Wakili aliponiona mbele yake akasema kwa Kinyakyusa"..Uledi mdogo wangu umenibomoa sana...huku anachekaa......."

Na mimi nikamjibu"..kaka ulikuwa na kauli nzitp sama katika sakata la Bandari,...kwamba wewe hautishwi na wewe ni mtanganyika...."Nilimjibu.Baadae Wakili akanikumbatia huku akisema alikuwa anatetea maslahi ya Taifa,tukacheka kwa pamoja baadae akanipatia kitambulisho ambacho juu yake kiliandikwa Tanzania na chenye nembo ya Bibi na Bwana.Nikaondoka.

Swali langu ambalo nataka tutafakari kwa pamoja kiroho ni nini maana ya ndoto hii hasa wakati huu Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ikitarajiwa kutoa hukumu yake leo August 7,2023 kuhusu Shauri la Kikatiba la Uwekezaji ndani ya Bandari ya Dar.

I.Nini maana ya Vitambulisho vile vyenye nembo ya Taifa huku vikiwa na Jina la Tanzania Juu yake?Kwanini vitambulisho vile viwe chini ya Wakili Mwabukusi na yeye ndio awe mgawaji Mkuu?

II.Nini maana ya Uchache wa vitambulosho vile.yaani viwe chini ya Saba na sio zaidi ya Nane?Kwanini visongekuwa vingi kwa maana ya mia mbili au mia tatu?Why uchache ule wenye makadirio ya vitambulisho saba au nane?

III.Nini maana ya rangi ya damu ya nje ikiwa imechanganyika na njano kwenye vitambulisho vile?

Nataka tutafakari pamoja kuhusu ndoto hii.Mwimbaji Kristina Shusho aliwahi kuimba kwamba "..nipe.macho nione,..sawa.sawa".Mungu atupe maana ya ndoto hii kwa nguvu zake.

+255692473785.
 
Hiyo ni ndoto tu kama ndoto zingine za kawaida.

UFunuo wa Mungu hauna kificho kama anatakabkukupa uelewa fulani huutoa straight soma ua fuatilia wote waliopata maono ya kweli ya kimungu huupeleka ujumbe wao bila kificho. Mfano angalia manabii wote walipewa ujumbe na ndio waliousimamia.

Hapo ni ndoto kama ndoto zingine unazoota unakojoa kwenye kichaka kumbe unakojoa kitandani
 
Umeota ndoto mwenyewe, ukahusisha Biblia na Mungu kwenye ndoto yako, ukamtaja Mwabukusi na Gwajima. Namba ya simu ya nini sasa wakati tiyari umetusimulia
 
Umeota ndoto mwenyewe, ukahusisha Biblia na Mungu kwenye ndoto yako, ukamtaja Mwabukusi na Gwajima. Namba ya simu ya nini sasa wakati tiyari umetusimulia
Ameitoa ili ikiwa nyumbu mmekasirika haswa....yaani kikwelikweli basi mupige hiyo kumtukana kama kawaida yenu kutoa matusi.
 
Back
Top Bottom