Nimeondolewa kwenye Tarrif 0 [Tanesco]

Nimeondolewa kwenye Tarrif 0 [Tanesco]

Sababu za kuondolewa ni kununua umeme wa elfu 10 ili itakapokatwa kodi ya makazi ibaki elf 9 ndo iwe malipo ya umeme. Sijui hata nifanyeje jamani maskini mimi
Haiitwi tarrif zero Ni Tarrif 4
Hapo ushapigwa penalty nenda ofisin ukajaze form upyaa
 
Utatakiwa kukaa ndani ya miezi mitatu ukitumia umeme usiozidi units 75 kwa kila mwezi, baada ya hapo utaenda kwenye ofisi za tanesco tawi lililokaribu yako, utaomba kukurudisha tena kwenye tarrif zero.
AHSANTE

Usinunue zaidi ya umeme wa sh, 3000/-
usizidishe unit 75 per month
Kwa hiyo usipozidisha unit 75 huku unaweka wa 20k hawakupi?
 
Sababu za kuondolewa ni kununua umeme wa elfu 10 ili itakapokatwa kodi ya makazi ibaki elf 9 ndo iwe malipo ya umeme. Sijui hata nifanyeje jamani maskini mimi
Mifumo y kizamani sanaa yana... Yani yakipuuzi... Inatakiwa wangepima kiwango cha units unazotumia sio unit unazo nunua
 
Sababu za kuondolewa ni kununua umeme wa elfu 10 ili itakapokatwa kodi ya makazi ibaki elf 9 ndo iwe malipo ya umeme. Sijui hata nifanyeje jamani maskini mimi
Tafuta pesa. Ukipenda bure utaolewa kila siku na kila mtu hapa mjini
 
hmm, hapana hakuna mita inayosetiwa, wana monitor matumizi yako PALE unaponunua umeme
ndiyo maana wanaweza kukuchomoa kwenye T0 ( au kukurudisha ) hukohuko uliko

kuna nyumba naijua wako kwenye T0 , tena ni ya wapangaji, wanachofanya ni kwamba, 69 zikiisha njiani, wanalala giza siku zilizobaki mpaka mwezi utimie ( siku 30 wanaongeza na siku 1 ) ndiyo WANANUNUA tena, unaona kiuhalisia hawa matumizi yao siyo 69 kwa mwezi
Mfano nikitumia chini ya unit 69?
 
TANESCO nahitaji msaada mimi natumia maximum unit 45 kwa mwezi nitumie utaratibu gani kupata hiyo tarrif 0?
 
Subiri bwawa letu pendwa lijae maji umeme utashuka bei wala hautafikiria hayo mambo ya 0 tariff
 
Unatumia unit chini ya 75 kwa mwezi? Unakaa Ghetto? Huna familia? Huna matumizi ya umeme ni bora ununue solar tu uwashe taa mbili ,upige subufa na kuchaji simu.
 
Back
Top Bottom