Nimeokota kitambulisho cha NIDA

Kuna jamaa aliwahi okota simu ya mtu ikamponza, akataka irudisha kwa nia nzuri lakini ikamponza. Kitambulisho nachoweza kuokota na nikatoa taarifa ni cha ndugu yangu. Vingine napotezea hapo hapo, sitaki usumbufu na vyombo vya dola.
 
Peleka polisi man. Niliokota wallet ina IDs kibao za mtu mmoja, nikaona ya ofisini kwake DIT. Hapo nimeokota Chang'ombe kule.

Kwakua nilikua na trip ya posta iyo siku, nikajifanya mwema nikaenda nacho DIT walinzi nikawavuka bila kuwaambia ila nilivoenda mapokezi nikawaambia. Nikawekwa sehemu akaja HR nikawa naongea nae.

Aisee kumbe jamaa alivamiwa jana yake alivokua anarudi kutoka kazini. Kaibiwa ibiwa ye yupo hospital.

Sema HR alikua muelewa, ila nikaacha taarifa zangu. Owner alikuja akanitafuta akiwa na polisi aone kama atanitambua ni moja ya watu niliomuattack, alivoniona tu akasema hapana uyu mrefu sana walikua wafupi. Nikasema dah. Wema huu.
 
Apo ungekua wafupi kama wao sijui nani angekua anaandika hapa saivi
 

Mtu mrefu sasa hivi ungekuwa unacheza kikapu Segedansi...
 
Kitendo cha kukipeleka kitambulisho chake kinatosha kabisa kuonyesha hujui chochote wala hujahusika hakuna muhalifu atakae mdhuru mtu na akapeleke kitambulisho chake polisi au kwenye ofisi yake
 

Unaweza ukakuta unafanya wema wa mshumaa, unawapa wenzako mwanga, huku unateketea.
 
Mbna [emoji23][emoji23][emoji23] unanitisha mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…