ungekuwa umelelewa malezi mazuri usingempa bint wa watu mimba na kumkimbia..."Nilikuwa na Mpenzi, tukabahatika kupata mtoto wa kiume,anakaribia umri wa miaka mitatu mwezi ujao, Kwa muda mrefu nimekuwa nikimwomba mzazi mwenzangu anipe mtoto akakae na wazazi wangu na hatimaye kuanzishiwa shule huko, kwa sababu naamini wazazi wangu watamlea mtoto kwa mazingira (ambayo nimekulia) ambayo mimi naamini ni mazuri kuliko pale kwa wazazi wa mwanamke, Nataka akakae huko hadi hapo nitakapo jipanga tena upya kimaisha, Tumefanya vikao vingi sana na hadi sasa sijafanikiwa kumpata mtoto wangu, naomba ushauri nifanyeje?"
Ni Maneno ya rafiki, ambaye anaomba ushauri, Naamini humu JF kuna wadau wengi wenye upeo wakutosha Binanfsi nimekosa Jibu la kumpa
Mkuu.. Haya masuala ya paternity yana matatizo.. Ila busara inatuongoza kuamini kwamba kama mzazi wa kike hana matatizo ya kiafya na kifedha ni vizuri yeye ndo akae na mtoto na kumlea huku mzazi wa kiume akihakikisha anatimiza majukumu yake kwa mtoto wake huyo.. Mfume dume umetupumbaza sana wanaume kiasi cha kujiona sie ndo tuna haki kuliko mama ambae mtoto amekaa tumboni mwake kwa miezi tisa na kujifungua kwa uchungu.. Tushindwa kuona connection kati ya uchungu wa mtoto kukaa kwa mama kwa miezi tisa na pia ule uchungu wa kujifungua na mapenzi yasio na chembe cha shaka toka kwa mama kwenda kwa mtoto..
Hii ndio tabu ya baadhi yetu wanaume, haswa wale wasiojielewa...inakuaje unafanywa JOGOO WA KUAZIMWA?...
Kwa akili yako, hivi kweli unaweza kumchukua mtoto wa miezi mitatu halafu umtenganishe na mama yake???
Kuna mambo kadhaa nahisi ndilo yamfanya huyo mwanadada aendelee kumng'ang'ania huyo mwanenu...
Mosi, Anajua kwa yeye kuendelea kuwa na mtoto, ndio dhamana pekee kwa yeye kuendelea kupata matunzo toka kwako...
Pili, nadhani kisheria ukishamzalisha mwanamke...inampasa mwanaume aendelee kutoa matunzo kwa mtoto hadi anapofikisha miaka kadhaa(nimesahau umri husika)...
Ushauri:
Acha kukwepa majukumu ya kumtunza mama wa mtoto kwa kisingizio cha kumchukua mwanenu, maana ulipoamua kumzalisha uliona anafaa kuwa mama wa mwanao otherwise you would have opted to adopt a child!!!
ungekuwa umelelewa malezi mazuri usingempa bint wa watu mimba na kumkimbia...
mwache mtoto alelewe na mama yake kama hana tatizo linaloweza kumdhuru mtoto.........