Nimenyimwa Mtoto

Neng'uli

Senior Member
Aug 1, 2011
126
33
"Nilikuwa na Mpenzi, tukabahatika kupata mtoto wa kiume,anakaribia umri wa miaka mitatu mwezi ujao, Kwa muda mrefu nimekuwa nikimwomba mzazi mwenzangu anipe mtoto akakae na wazazi wangu na hatimaye kuanzishiwa shule huko, kwa sababu naamini wazazi wangu watamlea mtoto kwa mazingira (ambayo nimekulia) ambayo mimi naamini ni mazuri kuliko pale kwa wazazi wa mwanamke, Nataka akakae huko hadi hapo nitakapo jipanga tena upya kimaisha, Tumefanya vikao vingi sana na hadi sasa sijafanikiwa kumpata mtoto wangu, naomba ushauri nifanyeje?"

Ni Maneno ya rafiki, ambaye anaomba ushauri, Naamini humu JF kuna wadau wengi wenye upeo wakutosha Binanfsi nimekosa Jibu la kumpa
 
mimba ikaingia,mpaka miezi 9.
Mtoto kazaliwa alikua wapi?
Embu muulize rafiki yako vizuri kwanza utupe full mkanda.
 
Nataka akakae huko hadi hapo nitakapo jipanga tena upya kimaisha, hiyo red ndo imefanya unyimwe yaelekea umefilisika...JIPANGE UPYA KWANZA
 
Mkuu.. Haya masuala ya paternity yana matatizo.. Ila busara inatuongoza kuamini kwamba kama mzazi wa kike hana matatizo ya kiafya na kifedha ni vizuri yeye ndo akae na mtoto na kumlea huku mzazi wa kiume akihakikisha anatimiza majukumu yake kwa mtoto wake huyo.. Mfume dume umetupumbaza sana wanaume kiasi cha kujiona sie ndo tuna haki kuliko mama ambae mtoto amekaa tumboni mwake kwa miezi tisa na kujifungua kwa uchungu.. Tushindwa kuona connection kati ya uchungu wa mtoto kukaa kwa mama kwa miezi tisa na pia ule uchungu wa kujifungua na mapenzi yasio na chembe cha shaka toka kwa mama kwenda kwa mtoto..
 
"Nilikuwa na Mpenzi, tukabahatika kupata mtoto wa kiume,anakaribia umri wa miaka mitatu mwezi ujao, Kwa muda mrefu nimekuwa nikimwomba mzazi mwenzangu anipe mtoto akakae na wazazi wangu na hatimaye kuanzishiwa shule huko, kwa sababu naamini wazazi wangu watamlea mtoto kwa mazingira (ambayo nimekulia) ambayo mimi naamini ni mazuri kuliko pale kwa wazazi wa mwanamke, Nataka akakae huko hadi hapo nitakapo jipanga tena upya kimaisha, Tumefanya vikao vingi sana na hadi sasa sijafanikiwa kumpata mtoto wangu, naomba ushauri nifanyeje?"

Ni Maneno ya rafiki, ambaye anaomba ushauri, Naamini humu JF kuna wadau wengi wenye upeo wakutosha Binanfsi nimekosa Jibu la kumpa
ungekuwa umelelewa malezi mazuri usingempa bint wa watu mimba na kumkimbia...
 
Mkuu.. Haya masuala ya paternity yana matatizo.. Ila busara inatuongoza kuamini kwamba kama mzazi wa kike hana matatizo ya kiafya na kifedha ni vizuri yeye ndo akae na mtoto na kumlea huku mzazi wa kiume akihakikisha anatimiza majukumu yake kwa mtoto wake huyo.. Mfume dume umetupumbaza sana wanaume kiasi cha kujiona sie ndo tuna haki kuliko mama ambae mtoto amekaa tumboni mwake kwa miezi tisa na kujifungua kwa uchungu.. Tushindwa kuona connection kati ya uchungu wa mtoto kukaa kwa mama kwa miezi tisa na pia ule uchungu wa kujifungua na mapenzi yasio na chembe cha shaka toka kwa mama kwenda kwa mtoto..

Niliogopa kuwa muwazi sana angalau kulinda urafiki
 
sababu anayoitoa ya kumtaka mtoto haiingii akilini.....
kama vile ambavyo yeye anaona kwa wazazi wake ni bora kuliko kwa mwanamke ndivyo mwanamke anavyoona pia kuhusu kwao. Kila mtu anaamini alikokulia kuna malezi bora kuliko kwa mwingine.
atafute sababu nyingine ya kuomba mtoto.
 
Mwambie huyo jamaa kuwa mama wa mtoto yuko sahihi. Baba hafai kuachiwa mtoto wa umri wa miaka mitat kwani hana mkakati wowote wa kumlea zaidi ya kuwapelekea mzigo wazazi wake yaani babu na bibi wa mtoto. Mwisho wa siku huyo mtoto atakosa malezi ya baba na mama.
 
Umtenda kosa la jinai la kumpa mimba binti mtoto chini ya umri unaohitajika kulingana na statement zako. Nitakusaidia kwa kukuitia Kova ili akufikishe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Feleshi akufungulia mashtaka yafuatayo: (1) kumpa mimba msichana chini ya umri miaka 18 (2)kushindwa kumtunza mtoto wako.
 
Mama mtoto yuko wapi...kwakweli hata mimi sioni sababu ya kupewa wazazi wako ikiwa mamamtoto yupo hai, vipi yeye aaminishe wazazi wako kuliko wake?
 
Hii ndio tabu ya baadhi yetu wanaume, haswa wale wasiojielewa...inakuaje unafanywa JOGOO WA KUAZIMWA?...
Kwa akili yako, hivi kweli unaweza kumchukua mtoto wa miezi mitatu halafu umtenganishe na mama yake???
Hata hivyo kuna mambo kadhaa nahisi ndiyo yalomfanya huyo mwanadada aendelee kumng'ang'ania huyo mwanenu...
Mosi, Anajua kwa yeye kuendelea kuwa na mtoto, ndio dhamana pekee kwa yeye kuendelea kupata matunzo toka kwako...
Pili, nadhani kisheria ukishamzalisha mwanamke...inampasa mwanaume aendelee kutoa matunzo kwa mtoto hadi anapofikisha miaka kadhaa(nimesahau umri husika)...

Ushauri:
Acha kukwepa majukumu ya kumtunza mama wa mtoto kwa kisingizio cha kumchukua mwanenu, maana ulipoamua kumzalisha uliona anafaa kuwa mama wa mwanao otherwise you would have opted to adopt a child!!!
 
Hii ndio tabu ya baadhi yetu wanaume, haswa wale wasiojielewa...inakuaje unafanywa JOGOO WA KUAZIMWA?...
Kwa akili yako, hivi kweli unaweza kumchukua mtoto wa miezi mitatu halafu umtenganishe na mama yake???
Kuna mambo kadhaa nahisi ndilo yamfanya huyo mwanadada aendelee kumng'ang'ania huyo mwanenu...
Mosi, Anajua kwa yeye kuendelea kuwa na mtoto, ndio dhamana pekee kwa yeye kuendelea kupata matunzo toka kwako...
Pili, nadhani kisheria ukishamzalisha mwanamke...inampasa mwanaume aendelee kutoa matunzo kwa mtoto hadi anapofikisha miaka kadhaa(nimesahau umri husika)...

Ushauri:
Acha kukwepa majukumu ya kumtunza mama wa mtoto kwa kisingizio cha kumchukua mwanenu, maana ulipoamua kumzalisha uliona anafaa kuwa mama wa mwanao otherwise you would have opted to adopt a child!!!

Hiii Inabidi ni print ifike kama ilivyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom