Nimenusurika, kidogo yanikute

chief72

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
625
302
Jamani juzi jioni mishale ya saa kumi na moja nilikuwa na rafiki angu wa kike,alipenda kupiga picha mbili tatu kwa hiyo akaomba tutafute maeneo mazuri na yakuvutia, kwa kihelehele changu nikaenda hom nkabeba kamera yangu tukaenda umbali kama wa kilometa tano hivi...eneo tulilofika lilikuwa tulivu na lina mawe makubwa sana yamebebana kwa ustadi wa hali ya juu...tukaenda bana, tukapiga picha vizuri tu ingawa kuna watu walipita haraka haraka na huku wakionyesha kama mshangao flan, si hatukujali...tulimaliza fresh zoezi lile kwa picha zaidi ya thelathini...... jana sasa, kuwa adisia watu tulipo enda hawaja amini hadi tulipo waonyesha picha, kumbe lile eneo ni hatari kwa majini, watu huwa hawaendi kabisa, hata kupita karibu na pale mwisho huwa saa tisa jioni...ni hatari inavosemekana...sasa sijui why hatukuzulika dunia hiii
 
Ni eneo gani hilo? Litaje tuchangie vizuri , wengine haka katanzania twakajua kama Almentary canal
 
ni makambako jamani, panaitwa Maguvani, mtoni, karibu na shule ya maguvani....pana mawe yamejipanga vizur sana
 
he!...najuta kwa nini nimesoma hii saa hizi......naogopajeeee....
 
Back
Top Bottom