Nimenunua kiwanja lakini kina shida

Kijana ushe2

Senior Member
Apr 6, 2017
176
122
Habari za asubuhi wanajf wenzangu
Awali ya yote namshukuru MWENYEZI MUNGU kwa kunijalia kuwa SALAMA wa AFYA. Nimenunua eneo la makazi kwa muuzaji ambae hapo awali walielewana na mtu kimdomo bila maandishi na akapewa hela laki 1 (NILIKUWA SIFAHAMU KUHUSU HYUO MUNUNUZI )
Baadae wakawa wanatafuta wa KUNUNUA nikaenda tutaelewana Bei nikaenda kwa NWENYEKITI WA KITONGOJI tukaandikishana na mashahidi wakawepo ambao walishuhudia tukiuziana jumla tulikuwa 8 kwa kutumia mkataba mihuri na passport tukabandika

Sasa baadae yule mama akaenda kumlipa laki 1 yule jamaaaa akaenda kushitaki KWA MTENDAJI WA KIJIJI )WAMEUZA ENEO AMBALO WALIKUWA WAMEELEWANA TANGU MWANZO LAKINI HAWAKUANDIKISHANA POPOTE PALE MTENDAJI AKANITAFUTA AKANIAMBIA HAPO UMEZIWA ENEO AMBALO WALIKUWA WAMESHAELEWANA WAAMBIE AKINA MAMA WAKURUDISHIE HELA NAMI NIKAMWAMBIA HAPANA LILE ENEO NI MALI YANGU NYARAKA ZOTE NINAZO
AKANIAMBIA haliwezekani

MWENZAKO alitoa pesa mwanzo baadhi halafu wewe umeenda kuelewana Mara ya pili na akawalazimisha wale mamama wasubirie tarehe 15/2/ wakalipwe hela yao ya kukamilishia nami

NAOMBA USHAURI MIMI NILIWALIPA HELA YOTE NIFANYEJE SASA HAPO ILI ARDHI YANGU IWE SALAMA??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndio hawa watendaji wetu wengi vijana waliojazwa mtaani, kisa ana elimu ya 4m4.......
Huku kuna mmoja hatoki nje, kuogopa wananchi.

Yeye anajua kbsa mambo hayo yanaenda kimaandishi, Anamsikiliza anaeleta mdomo ambao kila yule anao?,

Na akija mwingne akisema walishaelewana na mama kabla ya huyo jamaa? na mwingne na mwingne?

Na Si alitoa laki Moja na ndio hio karudishiwa sbb kiwanja kimeenda?

Ile sio BIASHARA ya nguo dukani kwamba eti nitoe nusu nusu ili uzuie isiuzwe,
Hii Ni mali na anayeuza ana SHIDA(tofautisha biashara na shida)

Wewe ndio tumeelewana utoe pesa nikuuzie,
umetoa nusu, pengine umepitisha mda wa kumalizia,
Mm shida yangu ipo pale pale, amekuja anayeweza kutatua shida yangu, tumemalizana, Nimekurudishia pesa yako,
Sasa kosa li wapi?

Labda km mama ameuza kabla ya siku ya mwisho waliyopatana(km walipatana) mnunuzi kumalizia hela yote...
Lkn tukumbuke still huyu mtu pengne ana shida na tukisema tutoke nje ya ubinadamu pia 'huna ushahidi..'

Na yote kwa yote hapo wakupelekeshana ni wao wenyewe.....
Maana hukuhusika wala kujulishwa hayo...
kwa sasa kiwanja hicho hata aliekuuzia hana sauti nacho...

Kurudisha hicho kiwanja ni either...

Uamue tuu kua yaishe km hakuna ulazima wa kupigishana kelele na kuepuka mali yenye malalamishi......

Uepuke usumbufu unaoweza jitokeza kutoka kwa Muuzaji, Mnunuzi wa kwanza na serikali hasa huyo mtendaji(japo sioni kosa kisheria).

Na yote hayo ukiamua una uwezo wa kudai Pesa ya usumbufu...

Huyo jamaa akikutana na wakaksi hata hio laki haipati na hana namna ya kukubana....

Hata akitaka kesi, yeye shida yake si HICHO kiwanja? na tayari uhalali wa kumuuzia unao?
Km vipi mwambie na wewe unakiuza na upo tayari kumuuzia aachane na huyo muuzaji wa mwanzo...
akija kutaka kununua mpe bei yako......
hawezi/hataki aache....

Ila mwisho wa yote km hakuna ulazima wa ligi...
temana nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waambie kwa upole unatangulia mahakamani, na unawashtaki wote, kuanzia wahusika serikali ya mtaa na muuzaji kwa UTAPELI...

Viongozi serikali ya mtaa waambie nakala inaenda kwa mkurugenzi na DC eneo husika...

Wapuuzi hao..


Everyday is Saturday..........:cool:
 
Pesa hawana wameni9nyesha kingine nimekataaa kipo mbali na Barabara nimewaambia wakauziane wao hukohuko Lin sio kwenye eneo langu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulitoa pesa kwa maandishi.na mihuri ya serikali imegongwa.na sahihi pia zimepigwa.usikubali upuuzi wowote .fukuza kabisa hao.hata huyo aliyekuuzia asikuzoee.biashara imekwisha.hayo mengine hayakuhusu.hata huyo mtendaji waweza mshitaki.hayupo juu ya sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulitoa pesa kwa maandishi.na mihuri ya serikali imegongwa.na sahihi pia zimepigwa.usikubali upuuzi wowote .fukuza kabisa hao.hata huyo aliyekuuzia asikuzoee.biashara imekwisha.hayo mengine hayakuhusu.hata huyo mtendaji waweza mshitaki.hayupo juu ya sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Okay wewe nimekuelewa nami nitapiga copy niende navyo mpaka kwa DC na mkurugenzi kwa ujinga wanaotaka kufanya NIMELIPA HELA KWA KIWANJA SIO KURUDISHIWA PESA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho kiwanja ni Mali yako halali kabisa,acha uwoga huyo mtendaji mwambie akikufuatilia utaenda mahakamani,hatuwezi kufuga viongozi Wa hovyo kama hao.
Jisikie huru tena ikibidi anza ujenzi kabisa au panda hata mihogo
 
Kama wako radhi kukurudishia fedha zako, pokea fedha zako na tafuta kwingine, ni kweli unayo haki lakini binadamu tumegeuka wanyama, jambo dogo kama hilo ambalo una haki, binadamu wanaweza kukufanyia mambo mabaya sana, wakakupa hasara isiyomithirika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom