Nimemvulia Kofia rapa Dizasta vina

Nimemvulia Kofia rapa Dizasta vina

mwakavuta

Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
99
Reaction score
307
Kwangu mimi huyu ni rapa bora wa muda wote ninamuweka kundi moja na marapa bora kabisa waliowahi kutokea Tanzania. Sijaona kazi yake yoyote ambayo hajaitendea haki.

Huyu jamaa hajawahi kukosea stail yake ya kuachia ngoma kwa series, kuanzia Hatia, nobody is safe, lost angel, siku mbaya, kanisa, ndoa, kikao amedhihirisha uwezo mkubwa sana alio nao kifalsafa. sasa hivi amekuja na ngoma mpya kwa mtindo wa masimulizi inaitwa Verteller ni wimbo unaofaa kusikilizwa na kila mwenye akili.

Tatizo la Dizasta nililoliona si mtu wa kuachia videos za nyimbo zake hii inamkosesha coverage ya television nyingi.

Naona sasa kuna haja ya wakereketwa wa hip-hop ngumu kuanzisha kituo cha redio kitakachowapa heshima wasanii wetu wa hip-hop ngumu watambulike zaidi.

Binafs sina deni na Dizasta hii ni icon ya hip-hop ya tanzania kwa miaka mingi sana ijayo.
 
Hii ungeweka kwenye jukwaa la entertainment but all in all yuko vizuri jamaa sema tu wasanii wengi waliopitia kwa Duke (M-Lab) wanaimba kwa mtindo wa kufanana sana
 
Umeaona uje ujipigie promo? Safi sana..
 
Umelist vzr hizo ngoma ila kuna hii KANISA..... Hii nyimbo ni fikirishi sana na ipo very straight. Hatia zipo nyingi 1,2,3.. kali sana jamaa anajua kupanga Vina anjiita #JESUS'TA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom