Nimemsikiliza Mzee Butiku dakika 45 za ITV na Radio One ameongea mengi, ila haya ndiyo yameonyesha kwanini Yeye ni Hazina ya Fikra Kubwa Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,568
108,911
1. Tanzania bado ina Viongozi Waonevu na bahati mbaya tena wengine bado tu wanarandaranda Mitaani na sijui kwanini hawagusiki na wanaogopwa na wenye Kuwawajibisha.

2. Tunataka Katiba Mpya je, yale yaliyopo Katiba iliyoko tumeyatekeleza hata kwa 75%?

3. Taifa letu sasa lina Watu Wanafiki ambao wakiwa Vichochoroni wananung'unika ila wakiwa mbele ya Viongozi wao wananyamaza.

4. Vijana wa Leo nchini Tanzania ni Waoga watupu.

5. Viongozi wanaotishia Watu wanaowakosoa ni Wasaliti wa Katiba yetu na kamwe hawatufai.

6. Vyombo vya Habari vya Tanzania siku hizi haviibui Mambo ya Kuwaamsha Wananchi kuhusu nchi yao, bali vinaibuliwa Mambo na Watawala kwa yale wayatakayo Wao.

7. Tujitahidi sana Kuwaheshimu Viongozi ( Watawala ) wetu hata kama kuna wanaotukwaza kwani ni Sisi hawa hawa ndiyo tumewaweka Madarakani walipo na kama tukitaka Kuwakosoa basi tuwakosoe kwa Staha na huu ndiyo umekuwa ( uwe ) Ustaarabu wa Watanzania.

Ninakuombea Uhai mrefu Mzee Butiku.
 
1. Tanzania bado ina Viongozi Waonevu na bahati mbaya tena wengine bado tu wanarandaranda Mitaani na sijui kwanini hawagusiki na wanaogopwa na wenye Kuwawajibisha.
Mzee Butiku naye mwoga tu. Sasa ameshindwa nn kutaja tu kuwa ni MAKONDA?

2. Tunataka Katiba Mpya je, yale yaliyopo Katiba iliyoko tumeyatekeleza hata k
Kwa hili mzee Butiku anazeeka vibaya.
 
Kwamba mzee butiku ni mzalendo sanaa au kanyimwa ugali ndio maana ana chakupoteza mbele yake.

Naye ni miongoni mwa watu waliyohusika kuendeleza katiba kandamizi ya wakoloni hiyo.
 
Huyu Butiku angekuwa na busara angesikika na kuonya wakati JIWE anakiuka katiba kwa maanuzi yake yaliyowakandamiza wananchi.

Enzi yake Jiwe alijitahidi sana kuonekana kuwa anafuata nyayo za Mwalimu kumbe alikuwa chui tu aliyevaa ngozi ya kondoo na Watu kama Butiku wakamuamini Kuwa alikuwa anafuata nyayo za Mwalimu hasa pale alipolazimisha kuhamia DODOMA hata bila matayarisho!! Kutumika Jina la mjomba wake kukamfunga mdomo!

Je, Butiku alikuwa wapi wakati Jiwe anawatisha wananchi na kuwanyima uhuru wao kwa kutumia vyombo vya dola kuwathibiti?

Kwani ni vijana tu wanaotakiwa kunung'unika na wazee sio sehemu ya jamii inayotakiwa kuonesha ujasiri pale haki inapopokwa?

Butiku anajitokeza sasa ili nae aonekane Kuwa yupo lakini hana faida kwa sasa kwa maendeleo ya Taifa hili. Ana jukumu la kuisaidia familia ya mwalimu ambayo inahitaji sana msaada wake kwa hivi sasa kwani Ukoo una VITUKUU!
 
Akina Butiku ni wazee wasiona faida Tanzania.
 
Umefanya vizuri kuyaweka kwenye mtiririko wa orodha.

2. "Tunataka Katiba Mpya" itakayowezesha kila mtu kuwajibishwa kwa mujibu wa katiba hiyo. Hii ya sasa kuna watu wapo juu yake, hawawezi kuwajibishwa kutokana na katiba hii.

3. Tanzania sasa ina watu wanafiki kila sehemu, na hii ni kutokana na siasa za kuleana zilizopo ndani ya CCM. Watu wanaogopa kuwa wakweli, kwa sababu maslahi yao yote wamewekeza kwenye chama. Ondoa chama hicho, watu wataanza kuwa huru na kuwa wakweli.
4. Vijana? Watakuwaje majasiri huku wakijua maslahi yao yapo ndani ya chama. Watapozwa pozwa na kusahau kwamba nchi watakayoirithi ni mzoga.

5. Viongozi wanaotishia watu, wanajuwa vyombo vinavyotakiwa kulinda haki za wananchi hao vimo mifukoni mwao. Bila kuwa na uhakika huo, kammwe hawawezi kumtishia yeyote.

6. Vyombo vya habari? Oooh, nchi hii ina vyombo vya habari tena? Kila mtu anatafuta upendeleo wa kuteuliwa au kufanikishwa katika shughuli zake na hao hao wanaosababisha matatizo yote ya nchi hii, CCM.

7. Ni wapi waliowekwa madarakani. Wote wamejiweka madarakani kwa nguvu.

Mzee Butiku na Mzee Warioba wamebaki kuwa sauti za nyikani tu, hawasikilizwi na hao watawala wala hawawanyimi usingizi. Wamekuwa ni watu wa kupuuzwa tu!
 
Katika watu ambao ni hatari kwa maendeleo, ustawi na mustakabali wa taifa hili ni hawa wazee wa Cold-War.
Jaribio lao la Ujamaa lilifeli vibaya na nchi ikaangukia pua, lakini nashangaa kwanini bado tunawasikiliza tu.
Ni wapi Afrika ambapo hapakuwa na "Ujamaa" ambako walinemeka sana! Unapokuwa kama santuri mbovu, wakati mwingine mikwaruzo hiyo pia hulainika na mara moja moja kunyoosha wimbo kwa usahihi. Hii ya kwako imegota moja kwa moja, vipi?
 
Back
Top Bottom