Nimemsikiliza Mzee Butiku dakika 45 za ITV na Radio One ameongea mengi, ila haya ndiyo yameonyesha kwanini Yeye ni Hazina ya Fikra Kubwa Tanzania

Kuwaweka Warioba na Butiku kundi moja sio sahihi hata mara moja Ingawa wanatoka sehemu moja!! Warioba is principled na sio mnafiki unlike Butiku ambae anaangalia maslahi yake yanapatikana wapi!! Enzi ya Jiwe kwavile taasisi yao ilikuwa inafadhiliwa kwa kiasi na Jiwe hakuwa na ubavu wa kujitokeza na kukosoa na sasa ili ajulikane kuwa yupo ndio anaanza kupiga mayowe.

Jaji Warioba has always been consistent.
Sina ufahamu mzuri na huo unafiki wa Butiku, na ndio kwanza nausikia toka kwako.

Kutosikika tu wakati wa Magufuli haiwezi kuwa ndicho kikawa kigezo cha kuwa mnafiki. Kunaweza kuwa na sababu nyingine za kumfanya asiseme kitu wakati huo. Sikumsikia hata siku moja akisifu lolote linalofanywa na Magufuli ili kuonyesha unafiki wake na unufaika wake.

Kama unao mfano halisi, naomba uuweke hapa kama ushahidi.
 
Namheshimu Mzee Butiku lakini natofautiana na mtizamo na maoni yake kuhusu wanaodai Katiba mpya.

..Mzee Butiku hatakiwi kushangaa kwanini Watz wanataka Katiba mpya wakati hii tuliyonayo haitekelezwi kwa 75% kama anavyodai.

..Mzee wetu alikuwepo kwenye TUME YA MABADILIKO YA KATIBA. Alishiriki kukusanya maoni ya wananchi. Alishiriki kuandaa Rasimu ya mapendekezo ya Katiba mpya.
 
Sikumsikia hata siku moja akisifu lolote linalofanywa na Magufuli ili kuonyesha unafiki wake na unufaika wake.

Mimi nilimsikia Butiku akimsifu Magufuli kuhusu uhamiaji wa makao makuu kwenda Dodoma ili hali seriklai ilikuwa haina bajeti ya kufanikisha kuhamia huko; hata kukasababisha katibu mkuu wa hazina wa wakati huo marehemu Likwelile apingane na Magufuli na kupelekea kufutwa kazi kwake na yeye kumuweka nduguye!! Kukaa kimya wakati watawala wanavunja katiba ni sawa na kukukubaliana na matendo yao!!
Magufuli alikuwa mfadhili mkuu wa familia ya Nyerere pengine nalo hilo lilimfanya awe bubu!!
 
Katika watu ambao ni hatari kwa maendeleo, ustawi na mustakabali wa taifa hili ni hawa wazee wa Cold-War.

Jaribio lao la Ujamaa lilifeli vibaya na nchi ikaangukia pua, lakini nashangaa kwanini bado tunawasikiliza tu.

Wanatupotezea muda tu, wameshindwa kutuachia taasisi imara wanakuwa motivation speakers.
 
Unaona iulivyo mpuuzi?
Kwa hiyo huwezi kutoa mfano hata mmoja, lakini unataka Tanzania isilinganishwe na nchi yoyote? Hiyo Tanzania ipo sayari ya pekee ambako matatizo yanayowapata wengine yenyewe haiyapati?
Hizo "NB" hazina maana yoyote kama huwezi kujibu swala la msingi.
Teh, teh, teh naona unataka kuniingiza kwenye siasa za viroja, kejeli, matusi na taarabu lakini huko siwezi kuingia. Hivyo wewe endelea kurusha vijembe lakini mimi nitakujibu tu hoja iliyoko mezani. Haya twende taratibu basi:

Mosi, Ujamaa nchini Tanzania ulifeli vibaya mno, hilo la kukimbilia kusema hata nchi ambazo zilikuwa za kibepari hazikuwa na maendeleo kuliko Tanzania nadhani ni kichaka cha kujificha tu, aidha kukwepa ukweli au kutoangalia mambo kwa mapana. Mifumo yote ya uzalishaji (Modes of Production) kuanzia utumwa, ukabaila, ubepari na ujamaa huwa na sifa zinazofanana, lakini leo hii ukisema uchukue mfumo wa ubepari na kuuanzisha kwenye kila nchi duniani kama mfumo rasmi wa uzalishaji nakuhakikishia lazima utapata matokeo tofauti.

Katika haya matokeo utakuta nchi ambazo zimefanikiwa sana na kutajirika, lakini kuna nchi ambazo zitakuwa zimefeli sana na kuwa masikini. Hili litatokea hata pale ambapo utatumia ujamaa kama ndiyo mfumo wa uzalishaji duniani kote. Sasa nini kinapelekea matokeo tofauti, tunakuja kwenye hoja yangu sasa: Kila nchi ina mazingira yake ambayo yanafanya iwe tofauti na nchi nyingine. Hivyo kupima maendeleo ya nchi moja kwa kuangalia mafanikio ya kiuchumi ya nchi nyingine, siyo jambo sahihi sana.

Nikupe mfano hai, hebu tuangalie The Structural Adjustment Programme (SAP), wengi wanadhani huu mchezo ulianza na nchi za Afrika. Lakini ulianza barani Ulaya kipindi cha The Marshall Plan, sema tu ulikuwa unafanywa na Marekani na siyo World Bank (WB) na IMF. Ulaya ilifanikiwa kiuchumi na kuna nchi zilitajirika sana tu, lakini nyingine zikafeli na kuishia kulaumu. SAP zikapelekwa Latin America ambapo nchi zilifanikiwa sana kiuchumi, lakini SAP zilezile hazikufanikiwa barani Afrika. Unadhani kwanini hazikufanikiwa ????

Mwaka 1998 Mwalimu Nyerere aliwakemea wazungu hadharani ndani ya mkutano akisema kila nchi ina mahitaji yake, hivyo kutumia sera ya jumla jumla kumesababisha matatizo. Akasema walimkosoa sana lakini wao wamefanya nini. SAP hazikufanikiwa Tanzania, lakini Argentina zilifanikiwa. Unadhani bado ni sawa tu kuendelea kulinganisha nchi ????

Pili, Sasa basi haya kabla ya kukimbilia huko kwenye GDP na kuanza kufananisha Tanzania na nchi nyingine, basi tuanze kwa kupima hali ya maisha ya watu kwenye nchi husika kwa kutumia nyenzo za kisayansi kama Human Development Index (HDI) ambayo hupima Life Expectancy, Per Capita Income Indicators na Education, vitu ambavyo ni msingi ndani ya taifa moja peke yake.

Haya sijayasema mimi MALCOM LUMUMBA, mchumi mkubwa duniani Prof Mahbubi Ul Huq ndiyo aliyekitengeneza hiki kipimo na kusema kitumike kupima maendeleo ya nchi husika kabla ya kutaka kufananisha taifa moja na jingine. Lengo la kufanya hivi ni kwasababu ukuaji wa ukuaji wa uchumi (Economic Growth) vinaweza visihusiane kabisa na raia wa kawaida kuwa na maisha mazuri ( Personal Well-being) au kupunguza utofauti wa vipato (Level of Inequality). Ntafurahi sana endapo Mkuu Kalamu1 utanirekebisha katika hili na kunipa kitu kipya kichwani,......

Hebu tuje sasa kwenye hoja yako ambayo wewe mwerevu uliyediriki kabisa kuniita mimi mpuuzi. Unauliza nchi gani ya Afrika ambayo haikuwa ya kijamaa lakini ilipata maendeleo kuliko Tanzania, ukataka kabisa na mifano. Mimi nijibu kama ifuatavyo: Mosi, kipimo sahihi cha kuangalia maendeleo ya nchi ni kuipima nchi husika kwa kuangalia maisha ambayo watu wake wanaishi kwanza, siyo kulinganisha GDP na nchi zingine. Hapa hatuwezi kulinganisha Tanzania na nchi nyingine kwasababu maendeleo hayo in Monetary Terms Alone, but also Non-Monetary Terms.......

Mwanauchumi nguli duniani wa kizazi chetu, ambaye ana tuzo ya Nobel ya Uchumi Prof Joseph Stiglitz anasema hivi, ukilinganisha Uchumi baina ya nchi peke yake hauwezi kufika kwenye jawabu sahihi. Hivyo yeye akapendekeza nyenzo kama The Capability Approach, ambayo hujikita katika kuangalia uwezo binafsi wa watu katika kufanikiwa kupata mafaniko binafsi endapo wataamua kufanya hivyo wakipewa uhuru.

Unaweza kusema watu wako huru kuzalisha au kutumia rasilimali zao na haki hizo ziko kikatiba, lakini kiuhalia hayo ni maneno matupu na watu wachache sana ndiyo huwa na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. Haya anayasema Prof Amartya Sen, siyo mimi. Sasa tujiulize swali la msingi kabisa tukitumia The Capability Approach: Hivi ni watanzania wangapi (Binafsi) wana uwezo wa kuzitumia rasilimali zilizopo Tanzania katika kujikwamua kiuchumi ??? (Tupime hili tukilinganisha kipindi cha Ujamaa na kipindi chetu hiki cha leo)

NB: Wajamaa waliwatengenezea watanzania uwezo binafsi wa kutumia rasilimali zao ????

Prof Joseph Stiglitz anasema hivi, tusipime uchumi kwa kuangalia "Gross" bali "Nets" ambapo ametaka tujikite kutazama hali ya wananchi wenyewe. Hivyo nikitazama watanzania, uwezo na rasilimali walizonazo hawakutakiwa kuwa hapa walipo leo hii. Hivyo kusema kwasababu nchi nyingine zilifeli basi Tanzania ni sawa kufeli ni hoja inayonishangaza sana. Lakini niko wazi kufundishwa zaidi, maana sifahamu kila kitu......

Mwisho kabisa, naongezea kitu kinaitwa Adjusted GDP's Approach. Hapa wachumi wanasema kwamba nchi husika kupimwa yenyewe ni jambo sahihi zaidi kwasababu maendeleo ya nchi hayatakiwi kuangaliwa katika nyanja ya uchumi peke yake (Monetary Terms Only). Hivyo lazima tuanze kuipima nchi husika kwenye muhimu kama utoaji wa afya bora, elimu bora, utunzaji wa mazingira n.k.

Hapa namaliza na maswali ya msingi kabisa: Watanzania wangapi walipata afya bora na elimu kipindi cha Ujamaa ??? Je, vipi kuhusu haki za msingi za kiraia (Basic Human Rights) pamoja na taasisi za kiraia ambazo zilitakiwa kutengenezwa ili kulinda haki za raia ??? (Kumbuka Karl Marx, anasema Human Rights are nothing rather than manifestations of The Capitalist Superstructure )

Mzee Nyerere naye akaamini kabisa akafutilia huko The Bill of Rights, wakisema It's a luxury we cannot afford.

Hivyo basi, mimi nasema tena: UJAMAA ulifeli na ukitaka kutumia ushauri na akili zilezile zilizotusababishia haya matatizo tuliyonayo leo basi endelea. Lakini pia ukiamini kabisa kwasababu mataifa mengine ambayo hayakuwa ya kijamaa yalifeli basi na sisi hatukuwa na namna, nakutakia kila la kheri mkuu.

Hapa barani Afrika kuna watu wanaamini kabisa kwamba ukoloni ndiyo umetuweka hapa tulipo, AND NOTHING IS EVER THEIR FAULT. Lakini wanasahau kwamba kuna nchi zilitawaliwa na wakoloni ila zikapiga hatua kubwa sana kiuchumi kuliko wengine.

Karibu tujadili....................
 
Inawezekana ujamaa ulifeli kama unavyodai. Hili ni suala linalohitaji mjadala mpana. Ulifeli kwa vigezo gani. Mfano mmoja idadi ya viwanda vilivyojengwa kipindi hicho huoni ilikuwa hatua nzuri kuelekea katika kujenga msingi wa Tanzania ya viwanda.

Pamoja na upungufu wa sera hiyo suala moja tunakubaliana. Tulifanikiwa kujenga taifa moja ambalo tofauti za kikabila, kijimbo, na kidini zilipungua na kukosa nguvu ya kutawala maisha ya watanzania. Matokeo yake amani na utulivu vimetamalaki kiasi kwamba anayetaka kufanya siasa kwa kutumia vigezo hivyo hatoboi pamoja na changamoto za katiba iliyopo.
Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha kwamba Ujamaa ndiyo mfumo uliojenga umoja wa kitaifa na kutuondolea ukabila na udini. Pia leo hakuna anayeweza kututhibitishia kwamba bila kuwepo Ujamaa basi Tanzania isingekuwa moja. Mfumo wa kikomunisti ulikuwepo nchini Yugoslavia, lakini nini kilitokea baada Josep Tito kufariki: Walichinjana kama kuku.....

Marekani nchi yenye majimbo, tena ya kibepari imedumu kwa zaidi ya miaka 300. Ina madhaifu mengi sana kama nchi, lakini raia wake hujivuna sana kuwa wamarekani. Awe ni Muitalia, Mchina, Mjerumani, Maurishi au Mweusi, wote hujivunia kuwa wamarekani. Unadhani sisi tunaweza kusema tuna umoja na uzalendo kama Wamarekani ??? Unaweza nithibitishia kwamba Ujamaa ndiyo huleta Umoja ???

Ambalo linatakiwa kukushangaza ni hili: Nchi ambazo tulikuwa tunazinyooshea vidole kwa kuwa na ukabila kama Nigeria, leo hii ndiyo nchi ambazo raia wake wanaongoza kwa kuwa na umoja na mshikamano kwenye mambo ya msingi na yenye tija kwa taifa lao. Kizazi kile cha zamani kimepita, kimekuja kizazi kipya kilichoelimika ambacho hakifuendekezi sana ukabila.

Wenzetu wamepitia kwenye mambo mengi kama Vita vya Biafra, ukikteta wa Bwana Abacha na mwishowe wameona madhara ya kucheza na uhuru. Nigeria isingekuwa hapa kiuchumi kama watu wake wasingeamua kishirikiana na kuvumiliana. Kadiri siku zinavyoenda na wanazidi kupaa kiuchumi, kitakuja kizazi kilichoelimika ambacho kitataka kufika mbali zaidi hivyo kitaachana kabisa na ukabila na udini.

Leo hii Tanzania nchi ambayo mnasema ni ya kijamaa ndiyo imekuwa nchi ambayo ukabila na udini vinazungumzwa waziwazi. Mbaya zaidi kuanzia Ikulu, heri tungezungumza sisi lakini bahati mbaya Raisi wa nchi anakuwa mkabila, mdini na mbaguzi halafu unasema bado sisi ni wamoja kweli. Hivi unaamini kabisa kinachosumbua muungano leo hii, ni mfumo wa Muungano ??? Ubaguzi na Udini, hakuna kingine, mtafumba macho lakini ukweli ndiyo huu. Leo hata muwekewe serikali tatu, watanganyika na wazanzibar hamuwezi kushibana......

Udini, Ukabila, Ukanda na ubaguzi wa aina yoyote ile ni dalili ya Ujinga ndani ya taifa. Kadiri taifa linavyoelimika ndivyo watu wake huachana kabisa na udini, ukabila, ukanda na ubaguzi wa aina yoyote ile. Tanzania ya leo ina wajinga wengi mno, tena wengine wana PhD kabisa ndiyo maana utasiki vitu vya ajabu kabisa, kama Wakristo hivi, waislamu hivi, mara SUKUMA GANH hivi. UJINGA MTUPU
 
Hata Lisu ni muog tu ndiyo maana alijificha kwenye ubalozi na kisha kukimbiza ubawa wake Ubelgiji.
Kwake nikawaida kujificha,
Hata alipopigwa risasi alijitahidi kujificha.
Mungu huwa anamficha.Kwa akili yake yakibinadamu hangeweza.
 
Hawa ndio chanzo kikubwa cha mkwamo tulio nao leo kama nchi.
Halafu bado wao ndiyo wanaendelea kutuamulia kila kitu mpaka leo. Jaribio lao la mwisho la kutaka kuirudisha nchi kwenye mstari kwa kumuweka Raisi Magufuli ili kuinyoosha nchi iliyoharibiwa na Jakaya Kikwete, lilienda vibaya mno na kutengeneza nyufa kubwa sana ndani ya taifa hili. Hawa watu wako kwenye vyombo nyeti vya dola na wanaendelea kutoa maamuzi, huku wakijulikana kama WENYE NCHI au WAZEE.

Nikiwaona wao na watoto wao waliowekwa kwenye mfumo huwa napatwa sana na kisirani kwasababu Tanzania inaelekea kubaya mno na tusipokuwa makini damu itakuja mwagika huko mbele. Historia itakuja kuwahukumu sana kwasababu mikono yao imejaa damu ya watanzania wasio na hatia. Aidha tuwatoe wao na watoto wao kinguvu au tuache watutumbukize shimoni,.......
 
Mimi nilimsikia Butiku akimsifu Magufuli kuhusu uhamiaji wa makao makuu kwenda Dodoma ili hali seriklai ilikuwa haina bajeti ya kufanikisha kuhamia huko; hata kukasababisha katibu mkuu wa hazina wa wakati huo marehemu Likwelile apingane na Magufuli na kupelekea kufutwa kazi kwake na yeye kumuweka nduguye!! Kukaa kimya wakati watawala wanavunja katiba ni sawa na kukukubaliana na matendo yao!!
Magufuli alikuwa mfadhili mkuu wa familia ya Nyerere pengine nalo hilo lilimfanya awe bubu!!
Kuna mambo ambayo ni vigumu kuyapinga, kama hilo la kuhamia Dodoma, pamoja na kwamba sikupenda mambo ya Magufuli, hilo nililipenda. Sasa kama huko kutakufanya wewe unione mimi kuwa najipendekeza kwa Magufuli, hakika utakuwa umekosea kabisa.

Hivi familia ya Nyerere walifanyiwa kitu gani cha ziada ya walichokuwa wanafanyiwa na awamu nyingine? Aliwajengea nyumba, barabara? Kafanya nini ambacho kilikuwa cha kuonyesha upendeleo kwa familia hiyo.

Bado sijaona sababu yako kumpachika mzee Butiku koti la unafiki. Nadhani unazo sababu nyingine ambazo hupendi kuzitaja hapa.
 
Karibu tujadili....................
Mkuu, sina muda wa hizi nadharia kwa sasa. Utaniwia radhi.

Sikuweza kusoma andiko lako lote, sehemu fupi niliyosoma nimeona yapo ninayoweza kukubaliana nawe, na bila shaka yapo mengi ambayo tunaweza kutokubaliana.

Lakini la muhimu ni hili: haitoshi kabisa kusema tu kwamba uchumi wa Tanzania ulianguka kwa sababu ya 'ujamaa', na kusahau kabisa hali ya uchumi duniani ilivyoziathiri nchi zote, hata zile ambazo uchumi wake ulikuwa juu kwa wakati huo.

Ndiyo, kuna mambo yalichangiwa na ubovu wa utendaji wetu, na kusababisha hali iwe duni zaidi, lakini hilo haliondoi ukweli wa hali kuwa ngumu duniani kote, na zaidi ya hapo, tukalazimika kupigana vita katika hali mbaya hiyo!

Inatosha kwa leo.
 
Halafu bado wao ndiyo wanaendelea kutuamulia kila kitu mpaka leo. Jaribio lao la mwisho la kutaka kuirudisha nchi kwenye mstari kwa kumuweka Raisi Magufuli ili kuinyoosha nchi iliyoharibiwa na Jakaya Kikwete, lilienda vibaya mno na kutengeneza nyufa kubwa sana ndani ya taifa hili. Hawa watu wako kwenye vyombo nyeti vya dola na wanaendelea kutoa maamuzi, huku wakijulikana kama WENYE NCHI au WAZEE.

Nikiwaona wao na watoto wao waliowekwa kwenye mfumo huwa napatwa sana na kisirani kwasababu Tanzania inaelekea kubaya mno na tusipokuwa makini damu itakuja mwagika huko mbele. Historia itakuja kuwahukumu sana kwasababu mikono yao imejaa damu ya watanzania wasio na hatia. Aidha tuwatoe wao na watoto wao kinguvu au tuache watutumbukize shimoni,.......
Sasa nashindwa kujuwa ni wapi wewe na mimi tunapotofautiana sana baada ya kukusoma hapa. Pengine ni kwenye neno hilo la 'UJAMAA' tu ndilo lenye shida, lakini hata huko, katika mistari ya mwanzo uliyoniandikia katika andiko lile refu, niliona hakuna tatizo lolote mbali ya kutaja tu neno 'ujamaa'.

Ninaiskitikia sana nchi hii kwa sasa. Sijui itakuwaje!
 
Katika watu ambao ni hatari kwa maendeleo, ustawi na mustakabali wa taifa hili ni hawa wazee wa Cold-War.

Jaribio lao la Ujamaa lilifeli vibaya na nchi ikaangukia pua, lakini nashangaa kwanini bado tunawasikiliza tu.
Mbona watanzania wote wanajua kuwa Tanzania miaka 60 bado ni maskini kwa sababu ya ufisadi na ubadhirifu Mali ya umma?
Maendeleo yanaletwa na Matumizi Bora ya rasilimali za nchi, Kodi ya Nchi, uzalendo, utawala Bora na haki za binadamu ambazo zinawezekana ki rahisi Sana ktk Taifa ambalo watu wameamua kuishi kijamaa!

Ujamaa ni nguzo halisi ya maendeleo!

CCM inajinasibu kuwa chama ni Cha kijamaa, na serikali ni ya kijamaa lakini uhalisia ni kwamba Tanzania hatujawahi kuwa wajamaa

Taifa la kijamaa halina uhujumu uchumi, kubambikiana kesi, kunyanyasa Raia, hakuna rushwa wala wizi wa kura, kukanyaga Katiba, hakuna muungano wa serikali mbili Bali serikali moja, hakuna vyama vingi vya siasa, hakuna kikosi Cha wasio julikana, hakuna mifumuko ya Bei holela n.k

Munaotukana ujamaa, hamuujui ujamaa! Tanzania hatujawahi kuishi ujamaa,

Wanadamu Wana mioyo ya ubinafsi, hawatakuja kuishi ktk ujamaa!

Ujamaa utabaki kwenye serikali ya mbinguni tu
 
1. Tanzania bado ina Viongozi Waonevu na bahati mbaya tena wengine bado tu wanarandaranda Mitaani na sijui kwanini hawagusiki na wanaogopwa na wenye Kuwawajibisha.

2. Tunataka Katiba Mpya je, yale yaliyopo Katiba iliyoko tumeyatekeleza hata kwa 75%?

3. Taifa letu sasa lina Watu Wanafiki ambao wakiwa Vichochoroni wananung'unika ila wakiwa mbele ya Viongozi wao wananyamaza.

4. Vijana wa Leo nchini Tanzania ni Waoga watupu.

5. Viongozi wanaotishia Watu wanaowakosoa ni Wasaliti wa Katiba yetu na kamwe hawatufai.

6. Vyombo vya Habari vya Tanzania siku hizi haviibui Mambo ya Kuwaamsha Wananchi kuhusu nchi yao, bali vinaibuliwa Mambo na Watawala kwa yale wayatakayo Wao.

7. Tujitahidi sana Kuwaheshimu Viongozi ( Watawala ) wetu hata kama kuna wanaotukwaza kwani ni Sisi hawa hawa ndiyo tumewaweka Madarakani walipo na kama tukitaka Kuwakosoa basi tuwakosoe kwa Staha na huu ndiyo umekuwa ( uwe ) Ustaarabu wa Watanzania.

Ninakuombea Uhai mrefu Mzee Butiku.
Hiyo no 7 sio sahihi. Viongozi tulionao sasa hatujawaweka sisi kwa kura zetu bali wamekuwa na vyombo vya dola chini ya kichaa yule
 
Hivi kwa nini ukumsikiliza Silaa na kuweka uchambuzi wake hapa?Au kwa kuwa point zake zilimkanda Mbowe na CHADEMA kwa ujumla?.
 
Hivi kwa nini ukumsikiliza Silaa na kuweka uchambuzi wake hapa?Au kwa kuwa point zake zilimkanda Mbowe na CHADEMA kwa ujumla?.
Umezuiwa kuanzisha Uzi unaomhusu Slaa? Yeye kapenda maelezo ya Butiku na ana sababu ambazo Wenye busara ndani ya JF wanajua Kwa nini!! Wewe kama unaona aliyoongea Slaa yana uzito anzisha Uzi wako watu wachangie.
 
Back
Top Bottom