Nimemsaidia Mwanamke asijitoe Uhai sababu ya Magumu ya Ndoa anayopitia

Dr. Mariposa

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
2,762
8,321
Jana nilikua Beach nafanya mazoezi ya viungo, wakati naendelea na kujinyoosha nyoosha likaja gari kali aina ya Prado jeusi, kwa speed yake ikanifanya niache nilichokua nafanya niangalie kifuatacho. likaenda kufunga break karibu kabisa na bahari, halafu hakukua na watu wengine karibu eneo hilo, ni eneo lenye ukimya sana.

Zikapita kama dakika 5 hivi, ndipo mlango ukafunguliwa akashuka Mwanamke mmoja matata sana, kimo cha wastani na umbo la wastani lenye mahipsi yamechomoza kiasi, amevaa suruali ya jeans iliyombana vizuri na kiblauzi kifupi yaan akinyanyua mkono kiuno kipo wazi, nywele amebana wanaita kidoti.

Basi akashuka ni kama vile alikua anaongea nikadhani yupo na Mtu mwingine kwenye gari lakini akarudi akashusha vioo na kuzima gari ndipo nikajua yupo peke yake.

Mimi nikaendelea kufanya mazoezi huku namuangalia kwa chini chini, nilihisi tu ujio wake sio wa kheir, nikamuona anakuja uelekeo niliopo, nikajiandaa, aliponifikia akanisalimia akasogea kwa mbele kidogo akakaa kwenye mchanga, akaanza kulia.

Niliishiwa pozi lote ikabidi nimfate alipoketi na kumuuliza kulikoni mbona analia, mazungumzo yetu;

"Hii Dunia haijawa sawa kwa upande wangu, natamani niondoke Duniani lakini nawaza Watoto bado wadogo ni mateso gani nitawaachia, ."

Hapo nikakaa chini kwanza, nikamwambia kwanza atoe hasira, uchungu, maumivu na kila kilichopo ndani ya kifua chake, akataka kujua kivipi nikamwambia, "nasogea pembeni yako, naomba ulie unavyoweza, lia kwa sauti hadi unapohisi machozi yamekauka na uchungu umeisha".

Hkua mbishi nikasogea pembeni akakaa kama sekunde kadhaa akaanza kulia, alilia kwa dakika kama 10 hivi, baadae akanigeukia nikamfata alipo, nikampa hongera na kumuomba afanye kitu kingine.

"Kama hutojali, pandisha suruali yako tusogee kwenye maji", hakubisha maskini dada wa watu, hapo maji ndio yanaanza kurudi, kwa hiyo mawimbi ya kutosha, tulipofika kwenye maji tukasimama, nikapiga kelele kaliii, nikamwambia na yeye afanye hivyo.

Mwanzo aliona aibu au kama mizinguo flani hivi lakini akajitahidi akapiga na yeye kelele moja, mimi nikarudia tena na yeye akarudia nikamuona ana enjoy kufanya vile basi alipiga kelele nyingi hadi akaanza kucheka, kwa mbali Mtu angetuona tumechanganyikiwa,.

Si ndio tukakumbuka gari alipaki karibu na bahari na maji yanarudi basi tukalikimbilia huku tunacheka, akalitoa na kupaki sehemu nzuri.

Nikamwambia kama hatojali anisubiri niende home nikaoge na kubadili nguo kisha nirudi. Akataka kujua ninapoishi, sio mbali na hapo beach ni mwendo wa miguu dkk 7 tu, akasema kama mimi sitojali twende wote ninapoishi, nikasema fresh, nikajitosa kwenye gari haooo hadi home.

Ilikua so weird kumkaribisha a stranger nyumbani kwangu ila nikapiga Moyo konde niliyataka mwenyewe, nikampa juice ya baridi akawa anashuka nayo, mie nikaoga chap na kuvaa, nikarudi kujumuika nae, yakaanza maswali kibaooooo kama tupo kwenye interview.

Nilifanikiwa kumjibu yote, nikamuuliza na yeye alikua anawaza nini alipofika pale baharini akawa mkweli alitaka ajitose baharini afie humo ndio maana alichagua sehemu isiyo na watu ili asipate kuokolewa, anasema aliponiona ni kama wazo lake liliyeyuka ghafla labda sababu hakudhani angekuta Mtu.

Akashukuru kua anajisikia mwenye amani ya Moyo japo anatamani asirudi nyumbani kwake lakini hana jinsi pale ndio kwake.

Mateso ya Ndoa Mume wake ni Mlevi sana, Mzinzi, wana Watoto wawili wapo Boarding School, Mumewe amekua anarudi usiku mwingi anamtukana bila sababu, anamdhalilisha.

Kiufupi hajawahi kua na furaha tangu ameolewa mwaka wa 15 sasa, wakikaa kwenye vikao vya suluhu, Mwanaume ana ahidi kujirekebisha lakini wakirudi hali ni ile ile, anajihisi amekosa msaada na Dunia ni kama imemtenga haioni maumivu yake.

Aliongea vitu vingi sana na mimi nilikua msikilizaji wake uzuri hakulia tena, hadi anaaga alikua mwenye Tabasamu mwanana, weekend hii tumepanga tukapate chakula cha Jioni sehemu.

Nimekua proud nimeweza kumsaidia Mtu asijitoe Uhai wake, yafuatayo tumuachie Mungu mwenyewe .
 
Jana nilikua Beach nafanya mazoezi ya viungo, wakati naendelea na kujinyoosha nyoosha likaja gari kali aina ya Prado jeusi, kwa speed yake ikanifanya niache nilichokua nafanya niangalie kifuatacho, likaenda kufunga break karibu kabisa na bahari, halafu hakukua na watu wengine karibu eneo hilo, ni eneo lenye ukimya sana,


Nimekua proud nimeweza kumsaidia Mtu asijitoe Uhai wake, yafuatayo tumuachie Mungu mwenyewe

Huna mda utamla na gari atakupa kaka ila jitahid kuwa mwema
 
Huyo mwanamke hakuachi teali kashajua wewe ndo una uwezo wa kumpa amani ya moyo
Swala la kumla au kutomla hilo ni kipengele kingine ambacho nategemea uzi siku za karibuni kuwa mshakulana hilo halipingiki na hachomoki mtu sababu wanawake wameubwa na mioyo ya kurudisha fadhila kwanjia yoyote ile.

Mwanamke unamnunulia gari la milioni 30 anakwenda kuliwa na mwamba aliemsaidia kubadilisha tairi wakati amepata pancha, ni kawaida kwao.

Hiyo ni karata mkuu umeshaichanga, we icheze kwa akili mingi.
 
Back
Top Bottom