Nimempenda Mtu Nisiyemfahamu-Sijawahi Kumuona

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Ndugu zangu,habari zenu.

Ni matumaini yangu kuwa sote tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila siku.

Ndugu yenu nimepata namasaibu yanayonitatiza na sijapata ufumbuzi. Ni hivi,nimejigundua kwamba nimefall in love na mtu ambaye sijawahi kumuona,sijui yeye ni nani,ana umri gani,kabila lake,ameoa ama la,ana mchumba ama la kifupi ni kuwa simfahamu kabisa.Huyu mtu nimchambuzi wa mambo mbalimbali ya siasa,uchumi n.k. Na kwa bahati mbaya sana tunaishi mbali mi niko Tz mwenzangu yuko nje ya nchi wala sijui yuko nchi gani.

Jamani am serious in love with this person,nifanye mwenzenu naugua kwa mahaba,siko tayari kulikosa penzi lake..Naombeni mbinu zenu nifanyeje ili awe wangu wa maisha.

Tafadhali naombeni ushauri wa kweli,tuache utani,am serious.
 

aisee hayo ni masahibu makubwa sana; la maana we mmwagie sera tu akikuelewa basi ndiyo hivyo tena amekuwa wako. La maana usikate tamaa.
 
Mwambie haya maneno yote kwenye pm na yeye atakupa msimamo wake baada hapo mtaendelea kufahamiana zaidi. Goodluck ni jambo la kawaida hilo usjione wa ajabu lol.
 
chatroom jeiefu imeleta mambo!...haya goodluck mama
 
Fixed point we to ushauri wako kulingana na srdi husika.Habari za kujua jinsia ya mpendwa au mpenda haina maana kwa sasa..We saidia bila kujali jinsia kwani mapenzi hayana jinsia na kutongoza au kutongozwa hakuangalii jinsia pia..Mwaga point basi..
 
Fixed point we to ushauri wako kulingana na srdi husika.Habari za kujua jinsia ya mpendwa au mpenda haina maana kwa sasa..We saidia bila kujali jinsia kwani mapenzi hayana jinsia na kutongoza au kutongozwa hakuangalii jinsia pia..Mwaga point basi..

Mimi nilikuwa kwanza namshitua Mzee asije akakazana kutafuta binti kumbe wewe unatafuta njema, ha haaaaaaaaaaa.
Ushauri wangu ni kwamba, kama unaweza kuwasiliana naye fanya hivyo. hata kama humfahamu. ila usianze kwa kumwambia kuwa unampenda, anza na salamu na maongezi ya kawaida kabisa. kadiri mtakavyokuwa mkiwasiliana utamfahamu zaidi na baadae ukishajua mwelekeo wake ndo unaweza kumwambia.
all the best
 
mmh.. basi miye ndio nimepatwa na utata; labda itabidi aje kutufafanulia..

mambo ya kua-sume jinsia za watu haya Mzee yanaweza kukupeleka kusiko. haya sasa mwenyewe ungekuwa busy kutafuta binti kumbe mwenzio anatafuta mkaka. kaaaazi kweli kweli
 
he he hee,nahisi hii sredi ni yako mkuu huyu mama kakuzimia ka avatar kako na mapolitiki.

Babu kijana.Give me a break!can someone fall in love kupitia Avatar ya Mwanakijiji I dont think so.Kibabu chenye fimbo kina mvuto gani?lol..Toa ushauri basi..
 
he he hee,nahisi hii sredi ni yako mkuu huyu mama kakuzimia ka avatar kako na mapolitiki.

nimecheka hapa sina mbavu na uzee huu nikimfia mtu kifuani si atapelekwa mtu Maweni bure.. lakini nimesoma sijaona kama anasema huyu mtu yupo JF!
 
GS....hayo maneno uliyoongea hapo juu kabisa yanaaonesha ni jinsi gani umemzimia huyo jamaa.....Cha msingi anza tu kummmwagia sera kwa PM,usiogope/usione aibu.........................Mtokee tu
 
Mmmm sasa hapo sijakuelewa kilichokufanya umzimie ni makala zake? sauti yake au ni nini? lakini nadhani bado hujafa maana ungekuwa unampenda sana kweli ungekuwa na full details zake. maana kwa upande wangu naona maelezo bado au yamejichanganya na imaginary pperson wako tu.
 
Ana mshiko lakini au umempenda tu?

Ukimsoma vizuri GS hapo juu kaongea maneno haya hapa chini;

"Ndugu yenu nimepata namasaibu yanayonitatiza na sijapata ufumbuzi. Ni hivi,nimejigundua kwamba nimefall in love na mtu ambaye sijawahi kumuona,sijui yeye ni nani,ana umri gani,kabila lake,ameoa ama la,ana mchumba ama la kifupi ni kuwa simfahamu kabisa.Huyu mtu nimchambuzi wa mambo mbalimbali ya siasa,uchumi n.k. Na kwa bahati mbaya sana tunaishi mbali mi niko Tz mwenzangu yuko nje ya nchi wala sijui yuko nchi gani.''
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…