Nimempa mimba, ananichukia hataki hata kuniona

Nimempa mimba, ananichukia hataki hata kuniona

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2013
Posts
3,097
Reaction score
1,356
Jamani, mnijuzeni mwenzenu mpenzi wangu tulikuwa tumeamua kuishi pamoja kabla ya kuhalalisha kwa watumishi wa Mungu.

Wakati huo tunasubiria tukawa tunamega taratibu tunda la mti wa katikati, ghafla mwenzangu mara kavimbiwa, kichefuchefu mara woohh....(katapika) alipoenda kupima akakuta amenasa.

Sasa shida ananichukia vibaya mno na sasa hivi yuko na kisirani na kiburi, ananiangalia kwa jicho la dharau sana!

Na mimi nimeona isiwe shida nimehama zangu nikarudi makazi yangu ya mwanzo, analalamika nirudi na mimi nimegoma.

Anataka nikajitambulishe kwao na mimi nikifikiria anavyonichukia nimemwambia kamwe siendi na pia ana kitabia cha kunishurutisha mara kwa mara kwa kunitumatuma ovyo..." Sielewi kapatwa na nini?

Ushauri jamani.
 
Pole sana kiongoz, hiyo ni Hali ya kawaida Sana lkn jitahid kuwa nae karibu tu maana hiyo mimba ndo imemfanya awe hivyo, mana yake amekebebea ujauzito hivyo bc atazaa mwanaume
 
Pole sana kiongoz, hiyo ni Hali ya kawaida Sana lkn jitahid kuwa nae karibu tu maana hiyo mimba ndo imemfanya awe hivyo, mana yake amekebebea ujauzito hivyo bc atazaa mwanaume

Asante Mkuu! Kwahiyo uhakika litakuwa dume..?
 
Mimba hizo, hupelekea kuchukia wanawake au wanaume, bt inategemeana na ujauzito wenyewe
 
Hizo ni complications za mamba tu wala usiingie mining baadaye ya miezi mitatu ya ujauzito wake hali hiyo itaisha utaona atakavyo kupenda zaidi.Usikimbie mkuu hiki ni kipindi cha kumega tunda kwa uhakika
 
Eti "Sielewi kapatwa na nini?

wewe umempa mimba halafu unatuuliza kapatwa na nini.
 
Sasa kwanini mnapeana mimba bado watoto hivi? Kueni kwanza mtajua outcomes za matendo yenu

Watoto hawana uwezo wa kupeana mimba wewe ebu heshima mbele brother...!
 
kapatwa na mimba.. sasa wewe mvumilie yeye hapo haelewi kinachoendelea we endelea na ratiba za kujitambulisha kwao tu
 
Kijana mpende uyo aiseee anakultea dume soon kuwa nae karibu mleteee vizawadi zawadi vindim,ukwaju,maembe yenyepilipili na vyuku kwa wingi ,mubembeleze kiss nying utaona mwenyewe
 
Kijana mpende uyo aiseee anakultea dume soon kuwa nae karibu mleteee vizawadi zawadi vindim,ukwaju,maembe yenyepilipili na vyuku kwa wingi ,mubembeleze kiss nying utaona mwenyewe

Hahaha eti..! Ananiletea dume...! Asante kwa ushauri ngoja nijitume nione kama nitatuzwaa...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom