Nimemnyima jirani yangu kibao cha nazi

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,199
Yamenikuta leo jumapili!

Leo siku ya wapendanao nasoma gazeti langu la JF sitting room.nimeona msichana wa kazi anajongea akionyesha anajambo anataka kunialifu.nikampa nafasi aongee kaniambia 'JIrani anaazima kibao cha Nazi' nimeshtuka,sijawahi sikia hilo toka nimeanza kuishi Dar,naamini ni kutokana na mazingira na malezi niliyolelewa.

Huyu jirani ni mpangaji wangu ambaye anaishi nje ya uzio wa nyumba ninayoishi.nimemwambia Dada wa kazi kuna vitu vya kuazima kama jembe/shoka n.k lakini sio kila kitu unaazimisha asipewe kwakuwa ni kifaa cha msingi anapaswa kuwa nacho.

Yawezekana ataniona kauzu, lakini napenda ajifunze the hard way kuwa sio kila kitu unaazima kwa jirani. Hata kama umezoea uswahilini,ukifika kwa washua jipange vitu vya kuwashirikisha kabla hujapoteza heshima yako na sifa ya kukaa na hao majirani.

Tupate funzo wakuu, Bongo tegemea kusikia yale ambayo hujawahi sikia au kufikiria.
 
Yamenikuta leo jumapili leo siku ya wapendanao nasoma gazeti langu la jf sitting room.nimeona msichana wa kazi anajongea akionyesha anajambo anataka kunialifu.nikampa nafasi aongee
kaniambia 'JIrani anaazima kibao cha Nazi' nimeshtuka,sijawahi sikia hilo toka nimeanza kuishi Dar,naamini ni kutokana na mazingira na malezi niliyolelewa.
Huyu jirani ni mpangaji wangu ambaye anaishi nje ya uzio wa nyumba ninayoishi.nimemwambia Dada wa kazi kuna vitu vya kuazima kama jembe/shoka n.k lakini sio kila kitu unaazimisha asipewe kwakuwa ni kifaa cha msingi anapaswa kuwa nacho.
Yawezekana ataniona kauzu,lakini napenda ajifunze the hard way kuwa sio kila kitu unaazima kwa jirani.hata kama umezoea uswahilini,ukifika kwa washua jipange vitu vya kuwashirikisha kabla hujapoteza heshima yako na sifa ya kukaa na hao majirani.
Tupate funzo wakuu,Bongo tegemea.kusikia yale ambayo hujawahi sikia au kufikiria.
Mkuu unajua ni kama umefanya mtu asile.kama hupendi ungetoa hicho kibao na maelekezo kuwa hupendi kuazimwa
Vipi ikitokea umepata kiharusi cha ghafla halafu ukahitaji msaada wa jirani
 
Ungempa tu! Labda una wasiwasi mwingine! Unasema "ni kitu cha msingi anatakiwa kuwa nacho" sasa kama hana mazoea ya kutumia inakuwaje?
 
Yamenikuta leo jumapili leo siku ya wapendanao nasoma gazeti langu la jf sitting room.nimeona msichana wa kazi anajongea akionyesha anajambo anataka kunialifu.nikampa nafasi aongee
kaniambia 'JIrani anaazima kibao cha Nazi' nimeshtuka,sijawahi sikia hilo toka nimeanza kuishi Dar,naamini ni kutokana na mazingira na malezi niliyolelewa.
Huyu jirani ni mpangaji wangu ambaye anaishi nje ya uzio wa nyumba ninayoishi.nimemwambia Dada wa kazi kuna vitu vya kuazima kama jembe/shoka n.k lakini sio kila kitu unaazimisha asipewe kwakuwa ni kifaa cha msingi anapaswa kuwa nacho.
Yawezekana ataniona kauzu,lakini napenda ajifunze the hard way kuwa sio kila kitu unaazima kwa jirani.hata kama umezoea uswahilini,ukifika kwa washua jipange vitu vya kuwashirikisha kabla hujapoteza heshima yako na sifa ya kukaa na hao majirani.
Tupate funzo wakuu,Bongo tegemea.kusikia yale ambayo hujawahi sikia au kufikiria.
Kumbuka hala hala jirani
 
Huyo jirani ana tabia ya kuombaomba?...Kama hayuko hivyo basi utakuwa haujamtendea haki..Kuna dharula nyingine inabidi kusaidiana
 
Swala la kuazima si baya kama endapo tu kile kinachoazimwa ni cha kawaida na si lazima sana kwa mtu kuwa nacho, ila kwa akili zetu huwa tunazidisha kuazima hata na visivyostahili Mazoea huwa yanajenga tabia siku zote.
Mkuu, umefanya vizuri kumnyima ili ajifunze na kuona umuhimu wa kuwa nacho hicho kibao.
 
Sawa kabisa atafute namna ya kukwangua nazi yake hat kwa vidole
kweli mkuu! kaamua kula wali wa nazi kwanini anifanye namimi nijue?! maswala mengine ni binafsi,mimi sitakiwi kujua anachotaka kupika au yeye ajue ya kwangu,havimhusu.
 
Kibao cha mbuzi ni km jembe, panga, sbb hata akikitumia hakiishi, ungempa tuu sioni shida miye
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom