Nimemlipia binti mahari lakini bado ananizungusha

Nimemlipia binti mahari lakini bado ananizungusha

Ndoa ipi ndg yangu kama mahali imeshalipwa na binti + wazazi wameridhia. Kwani hapo miaka ya nyuma kabla ya dini za wazungu na waarabh ndoa zinaendeshwaje
Ndoa ('Winga') kwa kinyamwezi ni utaratibu wa harusi za kijadi nilizozieleza, zilizokuwepo enzi na enzi kabla ya dini za mashariki ya kati kuletwa.
 
Wewe una matatizo domo zege yaani hadi leo unaenda kwa demi kutoa mahari haujaonja mbususu wala kuongea nae kabla.Kabla ya kuleta hii mada ungetuuliza namna ya kupata mke.Oa mwanamke anayekupenda yeye na sio unaempenda wewe utakuja kufa kabla ya muda wako.Huyo demu hakutaki na hata ukilazimisha kutokana na mahari atakutesa sana.Dai mahari yako hata ikibidi uende polisi na usigeuke nyuma.Huyo demu ana mtu wake anammega kiulainiii na mama yake anajua, wanakuchora tu kingo
Bro ata mimi nahisi hivyo kwa sababu apointment nyingi anakwepa na visingizio vingi na pia washawahi kufumaniwa kabla hapo kwao
 
Daaah sielewi hata, vipi sasa wamerudisha 2.5mil....
 
Nifupishe.....
Baba yangu anapesa ndo aliniongezea mahari mama yangu ni hali ya chini waliachana kitambo, Baba aliwasiliana na Mama nioe ndo nikachumbia familia ambayo baba mwenye mji ana wake wawili huyo kama alishamtelekeza na alishazalishwa na mwanaume watoto wawili,msichana anatabia nzuri tu ,tulifanya taratibu zote za ndoa za maadili tulitoa mahali tukiwa na mashahidi pande zote mbili,baada ya mahali tuliambiwa twaweza kumchukua mke nasi tukasema tukaandaye mazingira kwanza ya kufikia,walituelewa. Mda ulipo wadia Nilimpigia Babamkwe na kumwambia baba nataka nimwijie mwenza wangu yule babamkwe akasema ngoja niwasiliane nao alafu nitakupa jibu,nami nikasema sawa. Mida hiyo hiyo nilimcheki mwenza wangu kwenye simu nikaona yupo bize "inatumika simu yake" baadaye akanichek nikamwambia vp umewasiliana na baba akasema hapana ,nami nikamwambia nimemwambia nakuijia ,akasema hapana hajanambia ,nami nikasema sawa, akasema naumwa unaumwa nini homa umeaanza saa ngap mida tu ,ok pole nikaona kama drama tu kusikia
 
Ndo maana mama yangu akaanza kufatilia kwa mamamkwe vp mmefikia wapi, mama mkwe akajibu tumuage kwa kasherehe kadogo kwanza ,mama yangu akasema sisi sherehe baadaye maana inahitaji mda kidogo na garama ,wakakubaliana mama akaaga na kuondoka baada ya mda aliletewa simu hadi nyumbani na mamakwe, akapewa aongee na baba mkwe,alipoweka sikioni babamkwe akamtukana hivi wewe ndo unataka kukwamisha binti yangu asiolewe et nitakuja nikuue kwa moko moja tu acha ujinga na mimi sikufahamu wewe namfahamu huyo kijana na baba yake,mama alikata simu,mamamkwe akasema yaan mimi sikuzani kama mngefikia huko akaondoka mama alichukia na kusema wapo pamoja wanapeleka maneno kwa babamkwe ,tuliwasiliana na binti mara kwa mara lakini akawa hayupo sawa mi hadi sasa Babamkwe ajanipigia simu tena na miezi mitatu sasa imepita na mama hadi sasa anasema ukimuoa huyo mwanamke mimi si mama yako tafuta mwingine na baba yangu mzazi yeye kasema watayamaliza yataisha na nitamuoa. NIPO NJIA PANDA binti aliwahi nambia mama yake hataki mimi nilale
 
Nilale kwao baadaye yalipoibuka ya kutukanana na babamkwe nikamuuliza kwenye simu mama yako yupo akasema wanini? nikamwambia nataka nionge naye, alikataa unataka umwambie nini nami nikamwambia nataka nimuulize kuhusu kweli alikataa mimi kulala kwenu?Binti alisema hamna nilikudanganya tu akusema naomba unisamehe na pia alikuwa anataka uje ulale nyumbani lakini nilikwepesha,namimia nikamwambia sawa nimekusamehe ila ilikuwa sivyo .Hadi sasa mama kanikanya jana niachane na huyo binti, na wiki mbili sasa hatujawasiliana huyo binti,alikuwa anatuma sms za kunijulia hali kama wiki mbili kabla nikawa nazipotezea na kuziangalia tu .NAOMBENI USHAURI KAMA ULISOMA NILICHOANDIKA MWANZONI
 
Jitoe mapema upone. Utajuta. Nimebahatika kusoma habari yote.
Ushauri wangu ni huu.
Umeonyesha udhaifu mkubwa Sana
Na hayo Ndio madhara ya kulelewa na Single mother.
Umeombwa hela ya kusuka unakataa Je akiwa Mke? Elewa alikupima aone kama Dawa anayokupa imeingia Pale uliporeact ukakataa
Kutoa hela ya kusuka Ndipo alipokushinda
Dada ana akili kuliko wewe atakutesha
Angalia ulivyo na papara. Unataka tendo la ndoa kabla ya ndoa Bila kumpimia mtu ni wa namna gani Umeshajadiliwa familia haikutaki tena Ni vile tu wamekula mahari yako.

Fanya hivi
Tengeneza msuli wa uvumilivu
Nyamaza kimya, Usiulize chochote
Hakuna mtu atamuoa
Usidai pesa zako wala chochote
Malizia nyumba
Tafuta Mke mwingine.
Hii ndio akili ya mwanaume gaintoo broisser fata hii.
 
Wewe una matatizo domo zege yaani hadi leo unaenda kwa demi kutoa mahari haujaonja mbususu wala kuongea nae kabla.Kabla ya kuleta hii mada ungetuuliza namna ya kupata mke.Oa mwanamke anayekupenda yeye na sio unaempenda wewe utakuja kufa kabla ya muda wako.Huyo demu hakutaki na hata ukilazimisha kutokana na mahari atakutesa sana.Dai mahari yako hata ikibidi uende polisi na usigeuke nyuma.Huyo demu ana mtu wake anammega kiulainiii na mama yake anajua, wanakuchora tu kingo
Asante sana kwa ushauri naufanyia kazi
 
Wewe una matatizo domo zege yaani hadi leo unaenda kwa demi kutoa mahari haujaonja mbususu wala kuongea nae kabla.Kabla ya kuleta hii mada ungetuuliza namna ya kupata mke.Oa mwanamke anayekupenda yeye na sio unaempenda wewe utakuja kufa kabla ya muda wako.Huyo demu hakutaki na hata ukilazimisha kutokana na mahari atakutesa sana.Dai mahari yako hata ikibidi uende polisi na usigeuke nyuma.Huyo demu ana mtu wake anammega kiulainiii na mama yake anajua, wanakuchora tu kingo
Asante sana kwa ushauri naufanyia kazi
 
Wewe una matatizo domo zege yaani hadi leo unaenda kwa demi kutoa mahari haujaonja mbususu wala kuongea nae kabla.Kabla ya kuleta hii mada ungetuuliza namna ya kupata mke.Oa mwanamke anayekupenda yeye na sio unaempenda wewe utakuja kufa kabla ya muda wako.Huyo demu hakutaki na hata ukilazimisha kutokana na mahari atakutesa sana.Dai mahari yako hata ikibidi uende polisi na usigeuke nyuma.Huyo demu ana mtu wake anammega kiulainiii na mama yake anajua, wanakuchora tu kingo
Asante sana kwa ushauri naufanyia kazi
 
Habari wapedwa wa JF, mimi ni kijana wa miaka 33. Ninaishi kanda ya ziwa na ninaishi na mama yangu. Mama na baba waliachana nilipo maliza shule hadi form 4. Nilipomaliza, sikutaka kuendelea na masomo tena. Mwaka jana mwezi wa kwanza, mama akanambia umli umefika niende nikaoe na mwanamke yupo jirani tu na anapoishi.

Sikusita, nilienda hadi nyumbani kwa mama. Mama akasema, "Twende moja kwa moja kwao binti." Nilijiandaa na kwenda na mama hadi kwao yule binti. Tulikalibishwa vizuri na ghafla yule binti alipita, akatusalimia, akapita akaingia ndani.

Mama akanambia, "Vipi umemuona binti mwenyewe?" Nikamwambia, "Ndio mama, nimemuona, lakini sijajua kitabia yupo vizuri?" Mama akasema, "Bila shaka yupo vizuri sana." Nami nikasema, "Kama wewe umesema yupo vizuri, haina shida." Mama alimwita mama mwenye mji, akasema, "Si tumekuja kuchumbia kijana wangu huyu anataka kuoa kwenye hii familia." Mama mwenye mji akasema, "Haina shida, ngoja nimwite nimuulize." Basi mama akamuita, akaja, akaulizwa, "Huyu kijana amekuja kuchumbia hapa, vipi umekubaliana naye?" Yule binti akakubali.

Tukaachiwa muda tukapiga stori hadi muda fulani hivi, nikampa buku teni tukaaga na mama, tukasepa nyumbani. Nikamuuliza mama, "Vipi huyo yupo poa mama?" Mama akasema, "Yupo vizuri kitabia." Nami sikuwa na neno, nikamwambia, "Lini tunapeleka mahali?" Mama akasema, "Tuwasiliane na baba ndio tupange." Kweli baba alituambia ni jambo jema, si mshamchunguza? Yupo poa." Nikamwambia ndio.

Mwaka jana mwezi wa kumi na moja tulienda kutoa mahali 2.5M na kiasi kikubwa kilitolewa na baba. Walifanya sherehe kwao na binti siku hiyo ya mahali ilipita. Tulipewa muda wowote tu twaweza kwenda kumchukua binti kama hamna mambo ya sherehe. Tuliendelea kuchati na kuwasiliana na Jane na kupanga mara kwa mara.

Mwezi wa kumi na mbili nilienda kumtembelea Jane kwao. Nilienda na zawadi, hadi kwao nikakalibishwa vizuri. Nilipata muda wa kuongea na Jane. Nikamwambia, "Leo nimekuja kulala, vipi mazingira yapo poa?" Akastuka, akasema, "Acha utani basi." Nami nikamwambia, "Wala si utani, mimi na wewe tulishawahi kutaniana." Akasema, "Hapana." Akaropoka Jane, alisema, "Wewe mama, hataki kabisa kusikia hilo swala."

Nami sikuwa na pingamizi, nikamkubalia, nilikuja kuaga na kwenda zangu. Sikumuhoji sana, niondoka mida ya saa mbili usiku. Kumbuka, mimi ni Mnyamwezi na binti ni Mnyantuzu, mila za kwetu na baadhi ya makabila huwa na taratibu za kwenda kulala kwao binti, lakini sikufanikisha hivyo.

Baada ya siku mbili nilienda tena kwao na binti na zawadi, niliomba show tena, Jane alikataa, "Hivi si nilikwambia kuwa mama alikataa?" Nami nikasema, "Kweli, usijali, tulipiga stori, nikatambaa." Jane akanisindikiza, nikamuaga, nikasepa.

Mwezi wa kwanza, tarehe 2, nilimpigia simu baba yake na Jane, kuwa nataka nimuoe mwenza wangu. Baba mkwe akasema, "Ngoja niwasiliane nao, nitakupa jibu." Baadaye nilimtafuta binti, namba yake ikawa ina-busy kwa muda mrefu. Baadaye alinitumia ujumbe, mambo. Nikamwambia poa, vipi mzee kakwambia kuwa nakuijia. Jane akasema, "Hapana, ata sijawasiliana naye." Nikamwambia, "Sawa."

Akanambia, "Vipi, unanipeleka wapi?" Nikamwambia, "Ni kwa mama." Jane akasema, "Kwani nyumba haijakamilika uliyokuwa unajenga?" Nikamwambia, "Ndiyo, bado, ila soon." Nilikuwa na nyumba ambayo ipo mjini, haikuisha, ilikuwa yamebaki madirisha na milango tu, na Jane na wazazi wake walijua hilo.

Basi Jane tukaendelea kuchati. Naye akasema, "Nikija hapo mimi na wewe tutalalaje? Kama kwenu kuna vyumba viwili na sebule?" Nikamwambia, "Hayo yote sisi ndio tunapanga." Akasema, "Sawa, lakini mimi niliona nisubili tu hadi nyumba ikamilike ndio uniijie." Nikamwambia, "Haitawezekana, maana hata wazazi wako walikuwa wanataka nikuijie na tutaishi kwa muda kwa wazazi wetu tukipata baraka." Jane akasema, "Afu mi naumwa." Nikamuuliza, "Unaumwa nini?" Akasema, "Uchovu tu mwili wote." Nikamwambia, "Pole."

Visingizio vilikuwa vingi baada ya kusikia nataka nimpeleke nyumbani. Kesho yake niliaga nyumbani na kwenda job mbali na nyumbani, mkoa mwingine. Tokea jana sikupata mrejesho wowote kwa baba mkwe. Niliwasiliana na Jane mara kwa mara, akawa anasema, "Najua unanifikiria vibaya kuwa siumwi, ila kweli naumwa." Nikamwambia, "Mawazo yako tu." Akajibu, "Sawa." Kesho yake Jane akanipigia simu, nimtumie pesa ya kusuka.

Nikamwambia, "Sina kwa sasa." Akasema, "Sawa, kisa kilichotokea mama yako kutukanwa na baba, ndio maana hutaki kunidumia." Mimi nilijikuta naropoka, kwahyo sikumpa pesa za matumizi. Jane akasema, "Viela vyenyewe adi nikuombe." Nilipanda na hasira, nikamwamia, "Kuanzia leo agalamiwe na wazazi wake na siyo mimi." Jane akasema, "Sawa, na nakupenda sana. Kuna watu walikuja kunichumbia, nikawakataa, afu wewe huniheshimu, sawa tu." Nikamwambia, "Usidhani."
Itoshe kusema wewe ni nyumbu
 
Back
Top Bottom